Kitu gani umewahi kuona ukaamini uchawi upo?


Embu tazama hawa ni majirani wote ni watu wa arusha ni askari POLISi wote hawana cheo.
Wanapokea mshahara Sawa. Lakini huyu mmoja mbali na ufinyu wa muda, ana vibanda vya huduma za kifedha, ana pikipiki 2 zinazomletea hesabu ana kiwanja sehemu moja ipo chanika inaitwa zingiziwa na huwa anakopesha wenzake kwa riba. Huyo rafiki yake yeye ni pombe na pikipiki anayo lakini anasema hawezi kwenda kazini bila pikipiki Wana mwaka wa3 tangu waajiriwe.

Utofauti ni commitment yaani mmoja yupo radhi kuumia kwa muda mrefu kupata matunda endelevu lakini huyu mwingine hayupo tayari.

swali tutajuaje hao unaosema Wana juhudi na kweli wanaweza kuwa na juhudi kazini lakini wakakosa nidhamu, na commitment kwenye mishahara au pesa wanazozipata? Kwanini useme ni uchawi na tusikirie huenda kuna sababu ambazo ni logical?
 


Ni hivi uchawi ni stori za miujiza ya kufikirika mfano mtu kuyayuka gafla hilo haliwezi kuelezewa. Lakini tukiweza kulielezea haliwezi tena kuwa uchawi ambazo ni ignorance ya watu tu.

Nipe mfano wa mtu aliyefanikiwa kwa uchawi ambaye utajiri wake huwezi kuulezea in a logic form.

Kuhusu kufanya kazi Sawa na juhudi Sawa soma nilichoandika hapo juu

Au unataka nikupe mfano mwingine relevant?
 
🤣🤣🤣🤣Oa hii story umesoma kitabu gani
😁😁 hata mimi nilipokuwa kijana mdogo kama wewe, nilikuwa siamini kuhusiana na uchawi, nilikuwa silali hadi usiku wa manane, mda mwingine najificha nje labda kama ntaona kitu chochote, sijawahi kuona chochote, nilipotembea sasa huko duniani, nmekutana na mambo ambayo sikuyaona hapo kabla. Bado naendelea na uchunguzi kama ni uchawi au hallucination, japo kuna moja, unamwacha mtu nyumbani halafu unamkuta mbele ya safari, hii haikuwa hallucinations. Sidhani kama huo moyo wa kuwarekodi utaupata zaidi ya kufungulia turbo.
 
hakuna watu wanaofanya kazi kwa juhudi kama hao mnaosema wanatumia uchawi, wanafanya kazi kama punda.
Lakini miujiza ya uchawi ipo
 


Hahaha mkuu zacc
Pole sana hii stori yako inafurahisha.
sasa kama ulimuacha nyumbani ukakutana naye mbele ya safari hilo si jambo la kawaida mkuu.
 
Hizo si Mila potofu zenyewe. Ni argument from ignorance. Kitu hujui uliza. Of course sio kila mtu anafanikiwa Ila Kuna natural explanation, Kuna vitu vinatofautisha watu kuanzia muonekano, maadili, uongeaji etc. We unaweza usione hizi tofauti ukaconclude tu kuwa kafanikiwa kichawi ili upate jibu rahisi kwa swali gumu. It's stupidity. Ndo mwanzo wa uvivu na kuwa maskini kifikra na kifedha coz inajenga dhana kwamba unaweza fanya kazi Ila Kama huna uchawi unaweza usifanikiwe. Na since uchawi wenyewe haupo ndo unakuta mtu anaishia kutofanya jitihada za kufanikiwa
 
Kwani mi ni mzungu, wazazi wangu ni wazungu, Babu yangu ni mzungu. Ndo maana nakuambia ukiishi katika jamii inayoamini uchawi lazma na wewe ubongo wako utajenga hio picha ila in reality hicho kitu hakipo
Jamii kuamini uchawi na kutokuwa na uchawi hivyo ni vitu viwili tofauti, nimewataja hao wazungu kwa sababu watu kama nyie mnapouzungumzia huo uchawi mnauzungumzia kana kwamba mmezaliwa na mnaishi huko kwa wazungu ambako hakuna sana imani za kichawi na matukio yenye kuhusishwa na uchawi. Sasa watu kama nyie hapo pamoja na kuzaliwa na kuishi afrika ila nyie binafsi huwa hamjawahi kushuhudia matukio ya yenye kuhusishwa na uchawi na mkayafuatilia hadi mkagundia kuwa haikuwa uchawi bali ni kitu chengine.
 
Ni muda kidogo miaka ya 90 nilikua napita mitaa flani hivi Sinza usiku kama saa moja hivi. Sinza ya upande wa nyuma ya Hospital ya Palestine.

Sasa mtaa nliokua napita nyumba zilikua mbali kidogo na barabara. Yaani kuna safu za nyumba, mbele yake kama open space hivi kisha ndio barabara ya mtaa.

Mida hiyo kulikua na kama ka upepo hivi hivyo wakati natembea niliona Kwa mbali kama mita 20 - 30 kitu kama nylon (mfuko ya rambo) au karatasi jeupe linaburuzwa na upepo kutokea kwenye hizo nyumba kuja kati kati.

Sasa navyozidi kutembea kuelekea mbele nacho ndio kinavyozidi kusogea kuja barabarani, upepo ukikata nacho kinasimama. Kama vile imepangwa tukutane katikati. Yaani kinatembea kinasimama, kinatembea kinasimama.

Kenyewe kilianza kufika katikati ya barabara kabla yangu kikasimama kama kawaida yake. Sikukitilia maanani sana sababu nilijua ni upepo tu na nylon au karatasi kupeperushwa au kuburuzwa na upepo sio ajabu.

Ila Cha ajabu baada ya kukikaribia pale katikati ya barabara kiliposimama na kukiona vizuri nikashangaa kukuta ni kipande Cha tofali!!!. Sijawahi kuelewa mpaka leo hii kitu.
 
Ni wachache Sana ambao hawana elimu. That's the point..kwani point yangu ni kwamba hamna mzungu anayeamini ujinga. Wapo kibao ila ni wachache compared to us kwa sababu jamii zao zimeendelezwa kisayansi na kielimu
 
hakuna watu wanaofanya kazi kwa juhudi kama hao mnaosema wanatumia uchawi, wanafanya kazi kama punda.
Lakini miujiza ya uchawi ipo

Mkuu zacc
Hiyo miujiza ya uchawi ndio inasababisha wengine kufanikiwa zaidi na wengine kidogo regardless wote Wana juhudi Sawa.
 
Ushasema usiku.. ulikuwa umechoka ubongo unakuletea hallucinations. It's normal biology
 
jamaa hakulazimishi uamini uchawi, anakupa tips, we bado upo level 1, wanaposema kua uyaone sio maghorofa
🤣Mbona Kuna watu mpaka wanazeeka hawajawi ona mauchawi Kama Babu yangu na baba angu. Afu we katika ujana wako na utoto uone. Au wachawi wanachagua wajinga. Nipe hoja ya msingi, Kuna umri wa kuona wachawi ukifikia utaona au..? 🤣Na nikifika nisipoona utanipa kisingizio gani Sina macho ya kiroho ama
 
Sawa so solution sio uchawi ..hii ni argument from ignorance. Kitu hukielewi so jibu lake ni uchawi. Ndo tofauti, wenzetu wanatafuta majibu ya maswali we unahangaika kuwaza mauchawi ndo maana hatuendelei
Mimi sijasema kwamba kila mafanikio ni uchawi tu. Hao wenzetu kwenye kutafuta kwao majibu washawahi kuchunguza kwenye kuhusu uchawi au wanapinga tu na kuhitimisha hauwezi kuthibitishika?
 
Haina shida. Unataka kila mtu awe bill gates au...Ila kufanikiwa kwa mmoja na kutokufanikiwa kwa mwingine ni mambo ya basic economics tu sio lazma uweke uchawi..kuweka uchawi ni kuforce ujinga katika mada ya kisomi Kama uchumi na income inequality in nations..unakuwa hausolve tatizo kwa kusema tu "ni uchawi" ndo maana nasema approach yako ni ya kitoto
 
Mimi sijasema kwamba kila mafanikio ni uchawi tu. Hao wenzetu kwenye kutafuta kwao majibu washawahi kuchunguza kwenye kuhusu uchawi au wanapinga tu na kuhitimisha hauwezi kuthibitishika?
Washawahi kuchunguza ndo wakajua it's fake shit. Coz wao pia waliamini. Walikuwa wanachoma wachawi moto miaka ya 1500 mpaka 1700 Ila baada ya technology na elimu kukua wameacha coz wanaelewa. Sasa sisi tuliochelewa ndo tunaamini bado ila na sisi tutapita hio stage ni maendeleo tu... maendeleo sio barabara na majengo Ila fikra na tamaduni pia
 
Unafuu upo katika kutafuta ukweli na uhalisia wa mambo, kwa kufanya tafiti na tafakari juu ya maisha na kubuni mbinu Bora za kutatua maisha yako
Wewe ushawahi kufanyia utafiti uchawi na ukapata majibu ya kuwa uchawi kiuhalisia haupo?
 
Vitu si vipo...kwani we unajuaje Biden ni rais wa marekani, kwani umeishi marekani. Maswali mengine unauliza ya kijinga Sana hebu kua bac
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…