Kitu gani umewahi kuona ukaamini uchawi upo?

Shida yao hawa watu wa sayansi wanataka kutuambia kuwa hapa duniani hakuna mapepo,kila kitu watakujibu kisayansi kwao
 
2017

Nimetoka hasubuhi naelekea miangaiko k/koo njiani kuelekea kituoni kupanda gari, nasimamishwa na dogo mmoja ambaye najuana naye palipokuwa mtaani tulipokuwa tunaishi

Dogo akaanza kunilalamikia kuhusu dogo mwenzake ambaye aliweka nae share kwenye biashara fulani, na biashara ilikubali sanaa , hiyo biashara waliyokuwa wanafanya.. walikuwa wanatoa matunda baadhi ya vijiji vilivyokuwepo karibu na dar na kuya supply katika supermarkt walisajili kabsa kampuni yao, aisee walikuwa wanakimbiza hatari

Dogo akawa ananiomba nikaongee na huyo mwenzake ambaye wameshare biashara, malalamiko yake kuwa huyo jamaa anamroga Kwa kigezo cha kutaka kumdhurumu pesa na biashara kiujumla, nikamuhoji sanaa dogo licha yakuwa nilikuwa nachelewa miangaiko,nilimuhoji kuwa kajuaje kama anarogwa akanielezea kuwa mama yake ana ostaz wake kuwa kila mwezi anakuja kumuombea dua mama yake na nyumba yao kiujumla kuwa yeye ndio kawaambia, nikamuuliza umechukua hatua zozote

Akanambia kuwa mama yake alijaribu kumtafuta jamaa akakataa kwenda, wakaamua kumpigia sim na kumwambia akakataa kuwa hafanyi hivyo

Akanambia ameona kuwa mimi vijana wengi wananiheshimu na kunifata kwa ushauri na nimewazidi kidogo tu umri ingekuwa rahisi kuyamaliza matatizo yao

Nikamuuliza kuwa yeye anatakaje, akasema anataka kama apewe share yake na amuache aendelee na biashara, kwa maelezo yake dogo walikuwa na kama m12 kwenye account yao ya biashara

Kiukweli nilijaribu kumtafuta yule dogo mwenzake na alikataa kuwa hajaweka share na mwenzake huyo aliyokuja kuniomba nikaongee naye, nikamtafuta dogo na kumuelezea alibaki kulia tu na kunambia bro jamaa ataniua

Sasa ni 2023, roho inaniuma sanaa nilipata kwenda hapo mtaani mwanzoni wa mwaka huu, nimemkuta yule dogo aliyekuja kunilalamikia kuwa anarogwa ni chiz kabsa wallah nililia machozi kama mtoto mdogo nilihisi nna tuhuma Kwa Mwenyezi Mungu

Kibaya zaidi kanikumbuka na akiwa akinikuta njian ananisimamisha tunaongea vizur tu na tukimaliza maongezi ananiomba pesa, huwa nampa niliyokuwa nayo

Watu wanashangaa sanaa naongea na kuelewana na mtu ambaye anaonekana ni mchafu mchafu na kama hana akili vizur na nilivyokuwa smart na simbagui na full kunikumbatia yaani ilee kupeana hug... usimdharau mtu yeyote huko barabarani

Hakika Mungu atatulipa kwa chochote tutachowafanyie wengine
 
Kuna Siku nililala ndani peke yangu, muda wa saa moja asubuhi najiandaa kuamka nikasikia kishindo juu ya bati kama mtu karusha bonge la jiwe . Nikaamka haraka haraka kwenda kuchungulia nje ni nani karusha hilo jiwe. Kwa bahati mbaya sijamkuta mtu. Nikazunguka nje nyumba nzima kulitafuta lilipodondokea sikuliona nikaangaza juu ya bati sikuliona. Nikaamua nirudi ndani kuendelea na ratiba zingine nakuta mlango umefungwa ndani kwa komeo. Nikaita nikidhani kuna mtu nilipishana naye kipindi nazunguka nyumba yeye kaingia ikawa kimya. Nikahisi jambo lisilo la kawaida ikabidi nitafute fundi tukafanikiwa kubomoa mlango. Tumekagua vyumba vyote hatukuona mtu.
 
Duh..
 
harafu mtu anasema kiama hakipo. sasa huyo dogo hii dhulma atalipwaje ? tumche Mungu sana .
 
Mzimu (ghost)
 

Attachments

  • VID-20221005-WA0006.mp4
    4 MB
Jaribu kula balanced diet, unatatizo kwenye hormone balance, Ubongo, mentally unfit, pale Ubongo wako ulikuwa unatafisiria vitu ambavyo havipo
 
Mabati yana kawaida ya kujikunja na kujikunjua kutokana na hali ya hewa joto au baridi... Ni kawaida kusikia sauti.

Then milango yetu hii ya kuunga unga hasa mageti vitasa vyake kujifunga ni kawaida sana ukibamiza...

Tena kama we ulitoka kasi ukauacha ujipige.. hakuna uchawi hapo.

Tufanye kazi
 
Uchawi upo lakn sio tunavyo elezea.Uchawi kutumia maarifa yasiyo ya kisanyansi ,kwa lengo kutoa msaada, ila unazuru bila kujua. Uchawi ni ukosefu elimu ya sanyansi. Mtu huwezi kupaa na upo,uongo physics inakataa
 
Dah! Uchawi upo jamani..!

2002 huko shule ya Bulyaga ya msingi, Wilaya ya Rungwe mkoani mbeya ilikuwa hivi ….
Nikiwa std five pale aisee nilisoma na jamaa anaitwa Baraka nani sijui jina la mwisho nimesahau, ilikuwa ikifika jumatano na ijumaa jamaa anateswa sana na mapepo sasa kuna siku ilikuwa ni kivumbii alikuwa yakiamsha siku hiyo anawatembezea kichapo balaaa alikuwa anakuwa na nguvu za ajabu yaani… baadae nilihama ile shule nkarud town sijui iliishiaje yule mwamba halafu alikuwaga na akili kinomaa yaan
 
Al kaaba...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…