Kitu gani umewahi kuona ukaamini uchawi upo?

Kitu gani umewahi kuona ukaamini uchawi upo?

Qur'an 2:102.
Na wakafuata yale waliyo zua mashet'ani kuuzulia ufalme wa Su leiman. Na wala Suleiman hakukufuru, bali mashet'ani ndio walio kufuru, wakiwafundisha watu uchawi,...
Hivi vitabu vimeandikwa na wapuuzi ambao hawakujua dunia inazunguka jua. Ukiishi kwa akili za Hawa watu utaishia kuamini vitu ambavyo havipo ndo maana tunaenda shule. Ingekuwa Quran ni elimu tungeisoma mashuleni kwa lazima Kama sayansi
 
Kuna Mwana mwalimu wa A level alitupwa na tamisemi shule moja ya wanawake huko kusini mwa Tanzania, jamaa akajiona rijali akawa anawatembzea mashine wanafunzi wake siku moja akajikuta Yuko nje ya geti la kuingilia shule majira ya Saa 1 asubhi wakat alilala ndani kwake usiku wa Jana yake, ikabidi aombe uamisho kutokana na aibu aliyoipata kutoka kwa wanafunzi wake.
Hizi story za mtaani hazina udhibitisho wowote ndo maana hazitangazwi kwenye vyombo vya habari zinaishia huko mtaani
 
Aise
Kuna siku nilikuwa natoka kwenye mihangaiko yangu. Sasa kufika maeneo ya njia panda ya Mwenge nikawa navuka barabara. Wakati navuka, kuna jamaa naye akawa anavuka in opposite direction (tukawa tunaangaliana).

Sasa tukawa kama tunataka kupamiana. Maana nikienda kushoto, jamaa nae anaenda kushoto. Nikienda kulia, jamaa nae anaenda kulia, hadi tukawa tumekaribiana kabisa. Nikaganda kidogo ili kumruhusu yeye afanye uhamuzi, then tupishane, jamaa nae akawa kama vile ananisikilizia Mimi ndo nifanye uhamuzi. Haya yote yalitokea kwa haraka sana, ndani ya muda mfupi, na muda huo kuna cruiser ipo speed inatokea uelekeo wa Kawe inakuja uelekeo wetu Mimi na yule jamaa maana tupo katikati ya barabara, na muda huo zimeruhusiwa gari zinazotoka upande wa Kawe kwenda makumbusho na zinazokata Kona kwenda mawasiliano, za kutokea Makumbusho zimepigwa pini.

Baada ya kuona yule jamaa nae kasimama hanipishi, nikaamua kupita kushoto kwake, ili yeye apite kulia, cha ajabu na yeye akaja upande ule ule, tukawa tumekaribiana kabisa. Baada ya kuhisi hapa tutagongwa na Ile cruiser kwa uzembe, nilijikusanya nguvu zangu zote, nikaamua kumpiga push yule jamaa ili wote tuangukie upande wake, maana sikuwa tena na namna.

Ajabu ni kwamba nilivyojipeleka kumpush, nilijikuta napush hewa, alaf nikaangukia upande wa pili, yule jamaa hakuwepo aisee. Kile kitendo cha kuanguka, Ile cruiser ilipita speed, ikanikosa kidogo sana na haikusimama Wala kupunguza mwendo. Watu waliokuwa maeneo Yale walijua nijirusha kukwepa Ile cruiser, kumbe Mimi nilikuwa nataka kumpush mtu, na wao hawakuona mtu yoyote.
aise is it true dah hiyo balaa
 
Aise

aise is it true dah hiyo balaa
Muulize ana uthibitisho gani wa hizo story. Yaani hizi story Kama una akili timamu utaskia tu Mara huyu katokewa na Nini unajiuliza mbona hayakutokei kumbe ni vitu ndani ya fikra tu. Uchawi ungekuwepo watu wote wangeuona, kwa Nini Wanaona watu wachache Tena watu ambao ni duni na wasio na elimu ya mazingira na Sayansi. Ni rahisi kufikiria kitu ni uchawi Kama hukielewi, ni rahisi kuona mauza uza Kama ndo kitu ambacho kinajazwa akilini kwako na watu unaoishi.
 
Muulize ana uthibitisho gani wa hizo story. Yaani hizi story Kama una akili timamu utaskia tu Mara huyu katokewa na Nini unajiuliza mbona hayakutokei kumbe ni vitu ndani ya fikra tu. Uchawi ungekuwepo watu wote wangeuona, kwa Nini Wanaona watu wachache Tena watu ambao ni duni na wasio na elimu ya mazingira na Sayansi. Ni rahisi kufikiria kitu ni uchawi Kama hukielewi, ni rahisi kuona mauza uza Kama ndo kitu ambacho kinajazwa akilini kwako na watu unaoishi.
Uko sahihi
 
Kwan Kila kinachotangazwa na vyombo vya habar unakiamini? Huyo ni mtu wangu wa karibu na Huwa Sina matani naye kiivyo na hapo alikuwa ananielezea kwann aliondoka Lindi
🤣Sasa hapo ndo umethibitisha...mi Nikiwa mdau wako nikakuambia nimeamka mwezini asubuhi itakuwa kweli kisa mi rafiki yako au...vitu vingine tumia akili yako tu...na ndio taarifa ya habari inapitia vitu vingi mpaka ije kuwekwa pale. Ndo maana huwezi ona habari za uwongo au za kimbea mbea labda ziwe taarifa za udaku na uswahilini..
 
Back
Top Bottom