Kitu gani umewahi kuona ukaamini uchawi upo?

Kitu gani umewahi kuona ukaamini uchawi upo?

Nilikuwa nasafiri usiku kama saa 9 hivi na Lori niko peke yangu.
Nilipofika maeneo ya michungwani Tanga nikamuona binti mzuri kiasi anasimamisha gari.
Niliamua kutosimama lakini baada ya kufika kwedikwazu nikamuona binti yule yule na ghafla gari ikaanza kukosa nguvu na hatimae ikazima.
Binti akawa analisogelea gari....Sasa huo ni uchawi au ujini????
Huyo ni wewe kukosa nguvu za kifikra kutokana na uchovu usingizi na Giza la usiku...hizi ni hallucinations, ni product ya ubongo wako.
 
d
Kuna siku nilikuwa natoka kwenye mihangaiko yangu. Sasa kufika maeneo ya njia panda ya Mwenge nikawa navuka barabara. Wakati navuka, kuna jamaa naye akawa anavuka in opposite direction (tukawa tunaangaliana).

Sasa tukawa kama tunataka kupamiana. Maana nikienda kushoto, jamaa nae anaenda kushoto. Nikienda kulia, jamaa nae anaenda kulia, hadi tukawa tumekaribiana kabisa. Nikaganda kidogo ili kumruhusu yeye afanye uhamuzi, then tupishane, jamaa nae akawa kama vile ananisikilizia Mimi ndo nifanye uhamuzi. Haya yote yalitokea kwa haraka sana, ndani ya muda mfupi, na muda huo kuna cruiser ipo speed inatokea uelekeo wa Kawe inakuja uelekeo wetu Mimi na yule jamaa maana tupo katikati ya barabara, na muda huo zimeruhusiwa gari zinazotoka upande wa Kawe kwenda makumbusho na zinazokata Kona kwenda mawasiliano, za kutokea Makumbusho zimepigwa pini.

Baada ya kuona yule jamaa nae kasimama hanipishi, nikaamua kupita kushoto kwake, ili yeye apite kulia, cha ajabu na yeye akaja upande ule ule, tukawa tumekaribiana kabisa. Baada ya kuhisi hapa tutagongwa na Ile cruiser kwa uzembe, nilijikusanya nguvu zangu zote, nikaamua kumpiga push yule jamaa ili wote tuangukie upande wake, maana sikuwa tena na namna.

Ajabu ni kwamba nilivyojipeleka kumpush, nilijikuta napush hewa, alaf nikaangukia upande wa pili, yule jamaa hakuwepo aisee. Kile kitendo cha kuanguka, Ile cruiser ilipita speed, ikanikosa kidogo sana na haikusimama Wala kupunguza mwendo. Watu waliokuwa maeneo Yale walijua nijirusha kukwepa Ile cruiser, kumbe Mimi nilikuwa nataka kumpush mtu, na wao hawakuona mtu yoyote.
duuuu aise ilikua balaa sn
 
Hujawahi kuona mtu aliyefanikiwa kichawi? Kama wewe bado ni kijana "kuwa uyaone" na kama umri umekwenda unayaona Ila unafumba macho.
🤣Toa mfano leta data zenye uthibitisho sio unaongea kwa hisia..acha fikra za kimaskini...fanya kazi maisha yako yote ndo utafanikiwa. Acha wivu kwa watu, uchawi haupo, ungekuwepo na ungekuwa na maendeleo si kila mtu angeenda huko.
 
Kuna imani na hadithi mbalimbali katika jamii ambazo zinahusiana na uchawi, majini, na mapepo. Watu wengine wanasema kuwa wameona au kushuhudia vitu hivi, kama vile kukutana na marehemu, kubadilishiwa sehemu ya kulala, au matukio mengine ya kushangaza. Hata hivyo, ni muhimu kutambua kwamba masuala haya yanahusisha imani za kiroho na utamaduni, na kila mtu anaweza kuwa na maoni tofauti.

Katika kujibu swali lako, ni muhimu kutofautisha kati ya imani za kiroho na sayansi. Elimu ya biolojia inaweza kutoa ufafanuzi wa kisayansi juu ya mambo mengi yanayotokea katika maisha yetu. Kwa mfano, watu wanapokumbana na uzoefu wa kuona au kusikia vitu ambavyo havipo kimwili, inawezekana kuwa hii ni matokeo ya shughuli za ubongo ambazo zinaweza kuathiriwa na sababu mbalimbali kama vile matumizi ya dawa au magonjwa ya akili.

Hali duni ya maisha pia inaweza kuathiri jinsi watu wanavyoelewa mambo yanayotokea katika maisha yao. Umaskini, ukosefu wa elimu, na mazingira magumu yanaweza kuchochea imani za ushirikina au kuamini katika vitu ambavyo havina msingi wa kisayansi. Watu wanaweza kutafuta maelezo ya kiroho au ya kichawi kwa matukio ambayo hawawezi kuyaelewa kikamilifu kutokana na mazingira yao.

Hata hivyo, ni muhimu pia kuzingatia kwamba imani za kiroho na utamaduni zina umuhimu mkubwa katika maisha ya watu. Kwa baadhi ya watu, uzoefu wa kuona au kushuhudia vitu vya kiroho ni sehemu ya imani yao na ina umuhimu wa kipekee kwao. Hii inaweza kuwa njia ya kuunganisha na ulimwengu wa kiroho au kuwasaidia kupata maana katika maisha yao.

Ni vigumu sana kutoa jibu la moja kwa moja juu ya iwapo vitu kama uchawi, majini, na mapepo vipo au la. Sayansi haiwezi kukabiliana na mambo yote yanayohusiana na imani za kiroho, na imani za kiroho zinategemea mambo ambayo hayawezi kupimwa au kuonekana kimwili. Kila mtu ana uhuru wa kuamini au kutokubaliana na mambo haya, na ni muhimu kulinda uhuru huo wa kidini na maoni tofauti.

Kwa hiyo, jibu la swali lako linaweza kuwa kwamba imani za uchawi, majini, na mapepo zinaweza kuwa sehemu ya utamaduni na imani za kiroho za watu, na zinaweza kuathiriwa na elimu ya biolojia na hali duni ya maisha. Hata hivyo, ni muhimu kuheshimu maoni na imani za wengine na kutambua kwamba sayansi haiwezi kutoa majibu kamili kwa masuala yote ya kiroho.
 
Kwetu vijijini Kuna mzee aliangusha kibunda chake Cha pesa na akajua mtu aliyeziokota.Mzee alimwambia huyo jamaa Kama hataki nongwa amrudishie tu hela zake Jamaa akamkatalia kbsa akasema hakuokota pesa yoyote.

Mzee aliamua kuachana naye ila kabla ya kuondoka alimwambia atapata majibu.Aisee kilichomkuta huyo jamaa aliyeokota pesa huwezi amini.Alifiqa na wanawe 2 pamoja na mjukuu mmoja chini ya Mwezi mmoja.
 
Kwetu vijijini Kuna mzee aliangusha kibunda chake Cha pesa na akajua mtu aliyeziokota.Mzee alimwambia huyo jamaa Kama hataki nongwa amrudishie tu hela zake Jamaa akamkatalia kbsa akasema hakuokota pesa yoyote.

Mzee aliamua kuachana naye ila kabla ya kuondoka alimwambia atapata majibu.Aisee kilichomkuta huyo jamaa aliyeokota pesa huwezi amini.Alifiqa na wanawe 2 pamoja na mjukuu mmoja chini ya Mwezi mmoja.
So... What's ur point
 
Back
Top Bottom