Kitu gani umewahi kuona ukaamini uchawi upo?

2017

Nimetoka hasubuhi naelekea miangaiko k/koo njiani kuelekea kituoni kupanda gari, nasimamishwa na dogo mmoja ambaye najuana naye palipokuwa mtaani tulipokuwa tunaishi

Dogo akaanza kunilalamikia kuhusu dogo mwenzake ambaye aliweka nae share kwenye biashara fulani, na biashara ilikubali sanaa , hiyo biashara waliyokuwa wanafanya.. walikuwa wanatoa matunda baadhi ya vijiji vilivyokuwepo karibu na dar na kuya supply katika supermarkt walisajili kabsa kampuni yao, aisee walikuwa wanakimbiza hatari

Dogo akawa ananiomba nikaongee na huyo mwenzake ambaye wameshare biashara, malalamiko yake kuwa huyo jamaa anamroga Kwa kigezo cha kutaka kumdhurumu pesa na biashara kiujumla, nikamuhoji sanaa dogo licha yakuwa nilikuwa nachelewa miangaiko,nilimuhoji kuwa kajuaje kama anarogwa akanielezea kuwa mama yake ana ostaz wake kuwa kila mwezi anakuja kumuombea dua mama yake na nyumba yao kiujumla kuwa yeye ndio kawaambia, nikamuuliza umechukua hatua zozote

Akanambia kuwa mama yake alijaribu kumtafuta jamaa akakataa kwenda, wakaamua kumpigia sim na kumwambia akakataa kuwa hafanyi hivyo

Akanambia ameona kuwa mimi vijana wengi wananiheshimu na kunifata kwa ushauri na nimewazidi kidogo tu umri ingekuwa rahisi kuyamaliza matatizo yao

Nikamuuliza kuwa yeye anatakaje, akasema anataka kama apewe share yake na amuache aendelee na biashara, kwa maelezo yake dogo walikuwa na kama m12 kwenye account yao ya biashara

Kiukweli nilijaribu kumtafuta yule dogo mwenzake na alikataa kuwa hajaweka share na mwenzake huyo aliyokuja kuniomba nikaongee naye, nikamtafuta dogo na kumuelezea alibaki kulia tu na kunambia bro jamaa ataniua

Sasa ni 2023, roho inaniuma sanaa nilipata kwenda hapo mtaani mwanzoni wa mwaka huu, nimemkuta yule dogo aliyekuja kunilalamikia kuwa anarogwa ni chiz kabsa wallah nililia machozi kama mtoto mdogo nilihisi nna tuhuma Kwa Mwenyezi Mungu

Kibaya zaidi kanikumbuka na akiwa akinikuta njian ananisimamisha tunaongea vizur tu na tukimaliza maongezi ananiomba pesa, huwa nampa niliyokuwa nayo

Hakika Mungu atatulipa kwa chochote tutachowafanyie wengine
Like seriously 🤔
 
Uchawi upo ndugu zangu.

Kuna rafiki yangu mmoja alikuwa anagombea kiwanja cha babu yake yeye na mjomba wake, dogo babu yake alimkatia eneo kubwa tu na akafanikiwa kujenga.

mjomba wake akajiapiza wewe dogo si babu yako anakupenda sana sasa utaona.

Hivi sasa dogo ni kichaa dah, yaani inasikitisha watu wameangaika sana kumtibu lakini wapi ukumuona utamuonea huruma.
mimi nilitongoza pisi kali TANGA barabara ya 11,nikaenda nae nyumba ya wageni,wakati namwingilia {tulikuwa tumezima taa} nikahisi harufu kali ya mbuzi na ikawa kama nimelalia sufi,nikachoma fasta kuwasha taa nikaona mbuzi kalala kitandani alaf nikasikia bonge la sonyo kutoka darin,nilivaa nguo suruali bila chupi nikatoka nduki kifua wazi!!.....kaunta alibaki kushangaa,mlinzi nae akabaki kunsema,,,hii ndo tanga bhana lazima "jamaa kakutana na kioja"
 
🤣Story za watoto
 
Kuna siku nilikuwa natoka kwenye mihangaiko yangu. Sasa kufika maeneo ya njia panda ya Mwenge nikawa navuka barabara. Wakati navuka, kuna jamaa naye akawa anavuka in opposite direction (tukawa tunaangaliana).

Sasa tukawa kama tunataka kupamiana. Maana nikienda kushoto, jamaa nae anaenda kushoto. Nikienda kulia, jamaa nae anaenda kulia, hadi tukawa tumekaribiana kabisa. Nikaganda kidogo ili kumruhusu yeye afanye uhamuzi, then tupishane, jamaa nae akawa kama vile ananisikilizia Mimi ndo nifanye uhamuzi. Haya yote yalitokea kwa haraka sana, ndani ya muda mfupi, na muda huo kuna cruiser ipo speed inatokea uelekeo wa Kawe inakuja uelekeo wetu Mimi na yule jamaa maana tupo katikati ya barabara, na muda huo zimeruhusiwa gari zinazotoka upande wa Kawe kwenda makumbusho na zinazokata Kona kwenda mawasiliano, za kutokea Makumbusho zimepigwa pini.

Baada ya kuona yule jamaa nae kasimama hanipishi, nikaamua kupita kushoto kwake, ili yeye apite kulia, cha ajabu na yeye akaja upande ule ule, tukawa tumekaribiana kabisa. Baada ya kuhisi hapa tutagongwa na Ile cruiser kwa uzembe, nilijikusanya nguvu zangu zote, nikaamua kumpiga push yule jamaa ili wote tuangukie upande wake, maana sikuwa tena na namna.

Ajabu ni kwamba nilivyojipeleka kumpush, nilijikuta napush hewa, alaf nikaangukia upande wa pili, yule jamaa hakuwepo aisee. Kile kitendo cha kuanguka, Ile cruiser ilipita speed, ikanikosa kidogo sana na haikusimama Wala kupunguza mwendo. Watu waliokuwa maeneo Yale walijua nijirusha kukwepa Ile cruiser, kumbe Mimi nilikuwa nataka kumpush mtu, na wao hawakuona mtu yoyote.
duuuuh!! kumbe kweli haya mambo yapo ee ... pole na hongera kwa kupona
 
Kuna mahali nimeandika huyo aliyerogwa alikuwa Ni mjinga Hana elimu? Mbona unakurupuka kurupuka hivyo?

Sijakuforce uamini nilichokiandika sawa?
It's not real...mbona inawatokea watu wachache na watu wasio na elimu na wenye maisha duni..mbona watu wanazaliwa mpaka kufa na miaka zaidi ya 50 wasione hivi vitu. Au uchawi unachagua wajinga tu
 
Mkuu Umenikumbusha mbali nipo boarding.
Baadhi tuliosoma boarding tulipata sikia stori za miss corridor.

sasa huyu miss corridor ni moja ya hallucinations ambazo wengi tulipitia tulipokuwa shule, mfano ukitoa usiku saa7 au saa8 haja ndogo unasikia kama heels sound vya mwanamke kwenye veranda and out of the blue ile sauti inapotea. Hii ilitokea baada ya kusikia stori kwamba ukienda chooni usiku lazima usikie anatembea.

BAsi ubongo ukawa unaprocess hizo taarifa kila nitapotoka haja ndogo lazima nisikie heels kwenye veranda zikitembea.

Shida huwa watu wanaelezea hizi stori kwenye hali ambayo inataka kujustify wanachokiamini wao ndicho hicho.
Pale mwanza lilipo jengo la NSSF kwa sasa kulikua na bibi anamiliki eneo hilo yule bibi alikataa kutoka eneo hilo kupisha ujenzi pamoja jitihada zote za kumubembeleza zilishimdikaana ikabidi watumie nguvu huwezi amini bulldozer, excavator, wheel loader zote zilishishindwa kuvuja nyumba ya yule bibi inakitoka huko ikiwa nzima ikifika pale inapata breakdown kufupisha story yule bibi walimkalisha chini na kumsihi sana ndio akakubali nnacho kwambia sio story ya kusikia nlikua Mwanza miaka hio kaulize hio story

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Najua hii ingeenda viral share nami link ya video nikaangalie.

Halafu watu wangapi wamevunjiwa kwa kutolewa kwa nguvu na pesa wengine hawakulipwa na hatujasikia hizo stori? Unafikiri kungekuwa na mechanism ambayo inaweza kuzuia jambo kama hilo wangapi wangezuia?
 
Hauja ijua dunia, sijui umri wako ila nahisi bado mdogo

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app

Tuletee huyo mtu aliyefanikiwa kisa uchawi.
Maana tunafahamu uchawi ni vitu vya maajabu ajabu ambavyo kwangu ni stori tu na huwezi thibitisha.
Ok, tuletee mtu yoyote duniani ambaye yuko na mafanikio makubwa kwa ajili ya uchawi.
Ukianza kusema diamond mchawi, au bill gates au elon musk tutakukatalia maana hao wote wanafanya kazi kwa juhudi kubwa hivyo wote hao wana kamilisha kanuni za kiuchumi kama vile ni biashara BAsi ina

.ku embrace technology, innovation na creativity,
. customer satisfaction
.risk na uncertainties
Buying and selling

Embu tupe mfano wa mtu ambaye kafanikiwa kwa uchawi?
 
Najua hii ingeenda viral share nami link ya video nikaangalie.

Halafu watu wangapi wamevunjiwa kwa kutolewa kwa nguvu na pesa wengine hawakulipwa na hatujasikia hizo stori? Unafikiri kungekuwa na mechanism ambayo inaweza kuzuia jambo kama hilo wangapi wangezuia?
Kama upo mjini. Nenda pale mbuyuni, kama unaenda salender bridge ukaambiwe story ya ule mbuyu
 
2017

Nimetoka hasubuhi naelekea miangaiko k/koo njiani kuelekea kituoni kupanda gari, nasimamishwa na dogo mmoja ambaye najuana naye palipokuwa mtaani tulipokuwa tunaishi

Dogo akaanza kunilalamikia kuhusu dogo mwenzake ambaye aliweka nae share kwenye biashara fulani, na biashara ilikubali sanaa , hiyo biashara waliyokuwa wanafanya.. walikuwa wanatoa matunda baadhi ya vijiji vilivyokuwepo karibu na dar na kuya supply katika supermarkt walisajili kabsa kampuni yao, aisee walikuwa wanakimbiza hatari

Dogo akawa ananiomba nikaongee na huyo mwenzake ambaye wameshare biashara, malalamiko yake kuwa huyo jamaa anamroga Kwa kigezo cha kutaka kumdhurumu pesa na biashara kiujumla, nikamuhoji sanaa dogo licha yakuwa nilikuwa nachelewa miangaiko,nilimuhoji kuwa kajuaje kama anarogwa akanielezea kuwa mama yake ana ostaz wake kuwa kila mwezi anakuja kumuombea dua mama yake na nyumba yao kiujumla kuwa yeye ndio kawaambia, nikamuuliza umechukua hatua zozote

Akanambia kuwa mama yake alijaribu kumtafuta jamaa akakataa kwenda, wakaamua kumpigia sim na kumwambia akakataa kuwa hafanyi hivyo

Akanambia ameona kuwa mimi vijana wengi wananiheshimu na kunifata kwa ushauri na nimewazidi kidogo tu umri ingekuwa rahisi kuyamaliza matatizo yao

Nikamuuliza kuwa yeye anatakaje, akasema anataka kama apewe share yake na amuache aendelee na biashara, kwa maelezo yake dogo walikuwa na kama m12 kwenye account yao ya biashara

Kiukweli nilijaribu kumtafuta yule dogo mwenzake na alikataa kuwa hajaweka share na mwenzake huyo aliyokuja kuniomba nikaongee naye, nikamtafuta dogo na kumuelezea alibaki kulia tu na kunambia bro jamaa ataniua

Sasa ni 2023, roho inaniuma sanaa nilipata kwenda hapo mtaani mwanzoni wa mwaka huu, nimemkuta yule dogo aliyekuja kunilalamikia kuwa anarogwa ni chiz kabsa wallah nililia machozi kama mtoto mdogo nilihisi nna tuhuma Kwa Mwenyezi Mungu

Kibaya zaidi kanikumbuka na akiwa akinikuta njian ananisimamisha tunaongea vizur tu na tukimaliza maongezi ananiomba pesa, huwa nampa niliyokuwa nayo

Hakika Mungu atatulipa kwa chochote tutachowafanyie wengine
Dahh, Still unaeza fanya jambo mkuu, ila hilo jambo mshirikishe Mungu.
 
Najua hii ingeenda viral share nami link ya video nikaangalie.

Halafu watu wangapi wamevunjiwa kwa kutolewa kwa nguvu na pesa wengine hawakulipwa na hatujasikia hizo stori? Unafikiri kungekuwa na mechanism ambayo inaweza kuzuia jambo kama hilo wangapi wangezuia?
Inge enda viral bila social media? miaka ya mwanzoni 2000 kulikua story ni magazeti na radio

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Tuletee huyo mtu aliyefanikiwa kisa uchawi.
Maana tunafahamu uchawi ni vitu vya maajabu ajabu ambavyo kwangu ni stori tu na huwezi thibitisha.
Ok, tuletee mtu yoyote duniani ambaye yuko na mafanikio makubwa kwa ajili ya uchawi.
Ukianza kusema diamond mchawi, au bill gates au elon musk tutakukatalia maana hao wote wanafanya kazi kwa juhudi kubwa hivyo wote hao wana kamilisha kanuni za kiuchumi kama vile ni biashara BAsi ina

.ku embrace technology, innovation na creativity,
. customer satisfaction
.risk na uncertainties
Buying and selling

Embu tupe mfano wa mtu ambaye kafanikiwa kwa uchawi?
Hao uli mention una lala nao 24 hours unajua behind their backs? kama umeamua kukataa hata nikitaja utaleta ubishi tufanye umeshinda

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Inge enda viral bila social media? miaka ya mwanzoni 2000 kulikua story ni magazeti na radio

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app

Ok hiyo ni stori YAKO binafsi ILI ku justify stori yako.

Halafu mimi nilikuwa nazungumzia hallucinations na entoptic phenomena, wewe umeleta stori za kufikirika sijajua point yako ilikuwa ni nini.
 
Hao uli mention una lala nao 24 hours unajua behind their backs? kama umeamua kukataa hata nikitaja utaleta ubishi tufanye umeshinda

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Kulala nao 24hrs ni maneno yako si yangu.
Nimesema wanafanya kazi kwa juhudi, sidhani kama diamond, hamronize wanalala tu halafu asubuhi wanakuta nyimbo zipo utube zinaenda viral.

sina la nyongeza zaidi ya kukubali kushindwa kwako.
 
Back
Top Bottom