Kitu gani umewahi kuona ukaamini uchawi upo?

Kitu gani umewahi kuona ukaamini uchawi upo?

Mabati yana kawaida ya kujikunja na kujikunjua kutokana na hali ya hewa joto au baridi... Ni kawaida kusikia sauti.

Then milango yetu hii ya kuunga unga hasa mageti vitasa vyake kujifunga ni kawaida sana ukibamiza...

Tena kama we ulitoka kasi ukauacha ujipige.. hakuna uchawi hapo.

Tufanye kazi

Kweli kabisa umenikumbusha mbali sana. kuna mwaka1 kijijini kwetu kaka yangu alikua ana mchezo wakujenga nyumba alafu anauza baada yamuda anaenda usiku anarusha mwawe kwenye bati na kuchimba elizi zaungo nakweli mlangoni baada ya myezi mitatu watu wanaisusa nyumba kwa kuiuza kwabei cheee kabisa alafu broo anainunua tena kupitia mtu mwingine kwabei cheee[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Kuna Siku nililala ndani peke yangu, muda wa saa moja asubuhi najiandaa kuamka nikasikia kishindo juu ya bati kama mtu karusha bonge la jiwe . Nikaamka haraka haraka kwenda kuchungulia nje ni nani karusha hilo jiwe. Kwa bahati mbaya sijamkuta mtu. Nikazunguka nje nyumba nzima kulitafuta lilipodondokea sikuliona nikaangaza juu ya bati sikuliona. Nikaamua nirudi ndani kuendelea na ratiba zingine nakuta mlango umefungwa ndani kwa komeo. Nikaita nikidhani kuna mtu nilipishana naye kipindi nazunguka nyumba yeye kaingia ikawa kimya. Nikahisi jambo lisilo la kawaida ikabidi nitafute fundi tukafanikiwa kubomoa mlango. Tumekagua vyumba vyote hatukuona mtu.
Vipi uliendelea kukaa hmo?
 
Niliwahi date na mtoto wa mama mganga. Kila akitaka kuja nyumbani amsalimie bimkubwa namzungusha. Siku hiyo tumepanga ahadi vizuri kuwa atakuja home kumsalimia bimkubwa.
Nikamwitikia nikalala zangu. Usingizi ukanichukua ebwanawee naamshwa na milio ya nyuki kibao dirishani kuhamaki na haooo wanaishia akili haijakaa sawa simu inaingia. 'Niko njiani nakaribia'.
Nilikua puzzled kama dakika kadhaa hivi. Nabungaa hawa nyuki wametokea wapi mjini daslam!
 
Uchawi upo ndugu zangu

Kuna rafiki yangu mmoja alikuwa anagombea kiwanja cha babu yake yeye na mjomba wake, dogo babu yake alimkatia eneo kubwa tu na akafanikiwa kujenga.

mjomba wake akajiapiza wewe dogo si babu yako anakupenda sana sasa utaona.

Hivi sasa dogo ni kichaa dah, yaani inasikitisha watu wameangaika sana kumtibu lakini wapi ukumuona utamuonea huruma.
huyo dogo angeongea na mzimu wa babu yake, simplem
 
Mabati yana kawaida ya kujikunja na kujikunjua kutokana na hali ya hewa joto au baridi... Ni kawaida kusikia sauti.

Then milango yetu hii ya kuunga unga hasa mageti vitasa vyake kujifunga ni kawaida sana ukibamiza...

Tena kama we ulitoka kasi ukauacha ujipige.. hakuna uchawi hapo.

Tufanye kazi

Mkuu Umenikumbusha mbali nipo boarding.
Baadhi tuliosoma boarding tulipata sikia stori za miss corridor.

sasa huyu miss corridor ni moja ya hallucinations ambazo wengi tulipitia tulipokuwa shule, mfano ukitoa usiku saa7 au saa8 haja ndogo unasikia kama heels sound vya mwanamke kwenye veranda and out of the blue ile sauti inapotea. Hii ilitokea baada ya kusikia stori kwamba ukienda chooni usiku lazima usikie anatembea.

BAsi ubongo ukawa unaprocess hizo taarifa kila nitapotoka haja ndogo lazima nisikie heels kwenye veranda zikitembea.

Shida huwa watu wanaelezea hizi stori kwenye hali ambayo inataka kujustify wanachokiamini wao ndicho hicho.
 
Walimpoteza mdogo wangu mara 3 siku waliompoteza mara ya 3 walimrudisha uchi Hadi leo nguo zake hatujazipata na akili ya kusoma ikapotea kabisa pia sitosahau siku nilipoiona meli imetia nanga uwanja wa mpira usiku Zanzibar nao hawajambo
 
Kuna siku nilikuwa natoka kwenye mihangaiko yangu. Sasa kufika maeneo ya njia panda ya Mwenge nikawa navuka barabara. Wakati navuka, kuna jamaa naye akawa anavuka in opposite direction (tukawa tunaangaliana).

Sasa tukawa kama tunataka kupamiana. Maana nikienda kushoto, jamaa nae anaenda kushoto. Nikienda kulia, jamaa nae anaenda kulia, hadi tukawa tumekaribiana kabisa. Nikaganda kidogo ili kumruhusu yeye afanye uhamuzi, then tupishane, jamaa nae akawa kama vile ananisikilizia Mimi ndo nifanye uhamuzi. Haya yote yalitokea kwa haraka sana, ndani ya muda mfupi, na muda huo kuna cruiser ipo speed inatokea uelekeo wa Kawe inakuja uelekeo wetu Mimi na yule jamaa maana tupo katikati ya barabara, na muda huo zimeruhusiwa gari zinazotoka upande wa Kawe kwenda makumbusho na zinazokata Kona kwenda mawasiliano, za kutokea Makumbusho zimepigwa pini.

Baada ya kuona yule jamaa nae kasimama hanipishi, nikaamua kupita kushoto kwake, ili yeye apite kulia, cha ajabu na yeye akaja upande ule ule, tukawa tumekaribiana kabisa. Baada ya kuhisi hapa tutagongwa na Ile cruiser kwa uzembe, nilijikusanya nguvu zangu zote, nikaamua kumpiga push yule jamaa ili wote tuangukie upande wake, maana sikuwa tena na namna.

Ajabu ni kwamba nilivyojipeleka kumpush, nilijikuta napush hewa, alaf nikaangukia upande wa pili, yule jamaa hakuwepo aisee. Kile kitendo cha kuanguka, Ile cruiser ilipita speed, ikanikosa kidogo sana na haikusimama Wala kupunguza mwendo. Watu waliokuwa maeneo Yale walijua nijirusha kukwepa Ile cruiser, kumbe Mimi nilikuwa nataka kumpush mtu, na wao hawakuona mtu yoyote.
Wengine watasema ulikuwa na tatizo la Kisaikolojia, lakini ukweli ni kwamba hayo mambo yapo.
 
Uchawi upo ndugu zangu.

Kuna rafiki yangu mmoja alikuwa anagombea kiwanja cha babu yake yeye na mjomba wake, dogo babu yake alimkatia eneo kubwa tu na akafanikiwa kujenga.

mjomba wake akajiapiza wewe dogo si babu yako anakupenda sana sasa utaona.

Hivi sasa dogo ni kichaa dah, yaani inasikitisha watu wameangaika sana kumtibu lakini wapi ukumuona utamuonea huruma.
Kuona mkataba wa DP World unapitishwa na Bunge bila hata kuhoji wala tafakuri.

Uchawi upo
 
Uchawi upo ndugu zangu.

Kuna rafiki yangu mmoja alikuwa anagombea kiwanja cha babu yake yeye na mjomba wake, dogo babu yake alimkatia eneo kubwa tu na akafanikiwa kujenga.

mjomba wake akajiapiza wewe dogo si babu yako anakupenda sana sasa utaona.

Hivi sasa dogo ni kichaa dah, yaani inasikitisha watu wameangaika sana kumtibu lakini wapi ukumuona utamuonea huruma.
Ule moshi magufuli alipuliziwa kule kusini kwa majaliwa asee siku ile niliogopa wiki 2 pua kama kuna pilipili
 
Uchawi upo ndugu zangu.

Kuna rafiki yangu mmoja alikuwa anagombea kiwanja cha babu yake yeye na mjomba wake, dogo babu yake alimkatia eneo kubwa tu na akafanikiwa kujenga.

mjomba wake akajiapiza wewe dogo si babu yako anakupenda sana sasa utaona.

Hivi sasa dogo ni kichaa dah, yaani inasikitisha watu wameangaika sana kumtibu lakini wapi ukumuona utamuonea huruma.
Kuna Mwana mwalimu wa A level alitupwa na tamisemi shule moja ya wanawake huko kusini mwa Tanzania, jamaa akajiona rijali akawa anawatembzea mashine wanafunzi wake siku moja akajikuta Yuko nje ya geti la kuingilia shule majira ya Saa 1 asubhi wakat alilala ndani kwake usiku wa Jana yake, ikabidi aombe uamisho kutokana na aibu aliyoipata kutoka kwa wanafunzi wake.
 
Back
Top Bottom