Kitu gani umewahi kuona ukaamini uchawi upo?

Kitu gani umewahi kuona ukaamini uchawi upo?

Kuna siku nilikuwa natoka kwenye mihangaiko yangu. Sasa kufika maeneo ya njia panda ya Mwenge nikawa navuka barabara. Wakati navuka, kuna jamaa naye akawa anavuka in opposite direction (tukawa tunaangaliana).

Sasa tukawa kama tunataka kupamiana. Maana nikienda kushoto, jamaa nae anaenda kushoto. Nikienda kulia, jamaa nae anaenda kulia, hadi tukawa tumekaribiana kabisa. Nikaganda kidogo ili kumruhusu yeye afanye uhamuzi, then tupishane, jamaa nae akawa kama vile ananisikilizia Mimi ndo nifanye uhamuzi. Haya yote yalitokea kwa haraka sana, ndani ya muda mfupi, na muda huo kuna cruiser ipo speed inatokea uelekeo wa Kawe inakuja uelekeo wetu Mimi na yule jamaa maana tupo katikati ya barabara, na muda huo zimeruhusiwa gari zinazotoka upande wa Kawe kwenda makumbusho na zinazokata Kona kwenda mawasiliano, za kutokea Makumbusho zimepigwa pini.

Baada ya kuona yule jamaa nae kasimama hanipishi, nikaamua kupita kushoto kwake, ili yeye apite kulia, cha ajabu na yeye akaja upande ule ule, tukawa tumekaribiana kabisa. Baada ya kuhisi hapa tutagongwa na Ile cruiser kwa uzembe, nilijikusanya nguvu zangu zote, nikaamua kumpiga push yule jamaa ili wote tuangukie upande wake, maana sikuwa tena na namna.

Ajabu ni kwamba nilivyojipeleka kumpush, nilijikuta napush hewa, alaf nikaangukia upande wa pili, yule jamaa hakuwepo aisee. Kile kitendo cha kuanguka, Ile cruiser ilipita speed, ikanikosa kidogo sana na haikusimama Wala kupunguza mwendo. Watu waliokuwa maeneo Yale walijua nijirusha kukwepa Ile cruiser, kumbe Mimi nilikuwa nataka kumpush mtu, na wao hawakuona mtu yoyote.
Nani huyo alitaka kunitolea mchumba kafara😔
 
Kuna Profesa mmoja wa Chuo Kikuu Fulani hapa Tanzania alikuja Wilaya fulani niliyokuwa nafanyia kazi kuja kugombea Ubunge.

Wilaya ile ilikuwa inaongozwa na Mbunge fulani ambaye alikuwa ameshahudumu Kwa nafasi yake miaka 10, kwahiyo wakati Profesa anakuja kugombea jamaa alikuwa anataka kugombea Msimu wake wa 3.

Baada ya kuchukua fomu za kuwania, Chamani, Profesa akaanza kutafuta kuungwa Mkono na Wajumbe kwanza.

Kwahiyo alikuwa na waratibu wake kwaajili ya kumkutanisha na Wajumbe.

Kikao kikafanyika, kwenye Ukumbi wa Shule moja ya Sekondari. Wajumbe baada ya kutafutiwa 10k za Posho, wakajaa kama wote kumsikiliza Profesa Mtia Nia.

Ajabu baada ya Profesa kuingia Ukumbini ili aanze kuongea na Wajumbe, ghafla akaanza kuwaona Wajumbe wamegeuka kuwa Nyani.

Yaani Kila akijaribu kujikaza kuongea nao, anaona Nyani wanamcheka/wanampigia makofi ...

Profesa akatoka mbio, kuingia Kwenye gari na safari ya kurudi DSM Kazini kwake ikaanza.

Ndiyo ikawa mwanzo na mwisho wa Profesa kujihusisha na Siasa.

Ushahidi, NIAMINI BRO [emoji847]
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]mmk
 
Ushahidi, NIAMINI BRO 🤗
🤣🤣🤣Dunia hii
 
Uchawi upo ndugu zangu.

Kuna rafiki yangu mmoja alikuwa anagombea kiwanja cha babu yake yeye na mjomba wake, dogo babu yake alimkatia eneo kubwa tu na akafanikiwa kujenga.

Mjomba wake akajiapiza wewe dogo si babu yako anakupenda sana sasa utaona.

Hivi sasa dogo ni kichaa dah, yaani inasikitisha watu wameangaika sana kumtibu lakini wapi ukumuona utamuonea huruma.
Ufukara mkubwa kwenye maeneo yote CCM walipoweka "ngome!

"Utajiri"mkubwa maeneo ya wapinzani!
 
Wanangu nisiwe muongo me nilikuwa miongoni mwa matomaso mpaka leo hii muda huu...
Leo yamenikuta muda uuu ninao type naogopa ata kulala.
Iko ivi...

Nimelala vizuri usiku huu mida kama saa nane nikashtuka chumba changu nimetoka kumuota mtu flan ndugu wa nyumban ambae hatuna mazoea yeyote na mimi basi nikashtuka nikachukua simu yangu nikaingia wasap nikaangalia baadhi ya message nikaiweka pembeni ghafla nkaanza kuskia mwili mzima unasisimka alf ukafa ganzi mind you am still up taa zinawaka na macho nimefumbua...nisiwe muongo nikaanza kusoma quran mapema nikamuona mtu kaingia na kaniki japo sura siioni anataka kunigusa lakn ninavyozidi kusoma quran naona anashindwa kufikisha mkono badae akatoeka
Mnisamee naandika kwa mawenge maana ni jambo limetokea ata lisaa halijapita
 
Mmbo yanazidi kupamba moto😂😂
 
Attachments

  • Screenshot_20240815-073220.jpg
    Screenshot_20240815-073220.jpg
    178.4 KB · Views: 12
Uchawi upo ndugu zangu.

Kuna rafiki yangu mmoja alikuwa anagombea kiwanja cha babu yake yeye na mjomba wake, dogo babu yake alimkatia eneo kubwa tu na akafanikiwa kujenga.

Mjomba wake akajiapiza wewe dogo si babu yako anakupenda sana sasa utaona.

Hivi sasa dogo ni kichaa dah, yaani inasikitisha watu wameangaika sana kumtibu lakini wapi ukumuona utamuonea huruma.
Vichaa wote waliuziwa viwanja na babu zao ?

In short kuna kitu kinaitwa mind over matter (mfano wewe leo ukimpiga baba yako, kila utakachofanya kikienda kombo utasema laana ya baba, mwisho wa siku utakosa confidence na utakuwa unajiuliza mara mbili kabla ya kufanya lolote) ukiendelea hivyo na overthinking lazima utapata stress na kupelekea kuwa kichaa...

Binafsi napenda watu wanaohoji kila kitu kama hujui kitu unasema sijui na sio kuja na jibu la haraka haraka la uchawi...
 
Binafsi napenda watu wanaohoji kila kitu kama hujui kitu unasema sijui na sio kuja na jibu la haraka haraka la uchawi...a

Vichaa wote waliuziwa viwanja na babu zao ?

In short kuna kitu kinaitwa mind over matter (mfano wewe leo ukimpiga baba yako, kila utakachofanya kikienda kombo utasema laana ya baba, mwisho wa siku utakosa confidence na utakuwa unajiuliza mara mbili kabla ya kufanya lolote) ukiendelea hivyo na overthinking lazima utapata stress na kupelekea kuwa kichaa...

Binafsi napenda watu wanaohoji kila kitu kama hujui kitu unasema sijui na sio kuja na jibu la haraka haraka la uchawi...
Nigaa aya mambo hayaelezeki
 
Nigaa aya mambo hayaelezeki
Sasa jibu ni kwamba hatuyaelewi na sio uchawi..., sasa kama huyaelewi unajuaje kama ni uchawi au Uchawi ni nini labda tuanzie hapo ?

Kwangu mimi Uchawi ni hawa watumishi wetu walamba asali ambao wanakula Kodi zetu hakuna wanachofanya na bado wanaweka rehani mali za kizazi kijacho (kama ndivyo basi uchawi upo) ila kama ni super natural powers huenda tunadhani ni super sababu hatuelewi... au tuna miss define au tunapigwa changa la macho au ni coincidence...
 
Back
Top Bottom