Kitu gani umewahi kuona ukaamini uchawi upo?

Kitu gani umewahi kuona ukaamini uchawi upo?

Vitabu vya dini biblia na qurani vimeeleza kuhusu uchawi...
Nimekuambia Usiniletee hizo hekaya....Zina maujinga mengi zimeandikwa na watu ambao hawakujua jua linaenda wapi usiku...so huwezi tumia kitabu hicho Kama evidence... thibitisha uchawi empirically sio kwa hadithi za mababu washirikina...wa kiyahudi na kiarabu
 
mi nasoma tu comment za watu humu wanaosema eti uchawi haupo,watu tushakutana na mengi sana hii dunia....yani kwa kifupi tu ni kwamba
UCHAWI UPO
Upo kwako wewe na wauni wenzako ila kama kitu kipo kipo kwa wote hakibagui...jua lipo mvua ipo Simba wapo ila dragons hawapo malaika hawapo majini hawapo no matter wat u think u see or hear Itabaki akilini kwako na wenzako tu ila huwezi prove chochote
 
Kama hao binashetani wanasumbua hebu weka ndoo ya maji mlango kwenye chumba unacholala hiyo ndio ijae maji hrf simamisha kisu ndan ya maji yaan ile sehem ya ncha iguse maji chin ya ndoo hrf hiyo ndio weka mlangon kwako! Huyo anayejiita mchawi kama hawata mzika bas atajuta kuzaliwa!
 
Kuna siku nilikuwa natoka kwenye mihangaiko yangu. Sasa kufika maeneo ya njia panda ya Mwenge nikawa navuka barabara. Wakati navuka, kuna jamaa naye akawa anavuka in opposite direction (tukawa tunaangaliana).

Sasa tukawa kama tunataka kupamiana. Maana nikienda kushoto, jamaa nae anaenda kushoto. Nikienda kulia, jamaa nae anaenda kulia, hadi tukawa tumekaribiana kabisa. Nikaganda kidogo ili kumruhusu yeye afanye uhamuzi, then tupishane, jamaa nae akawa kama vile ananisikilizia Mimi ndo nifanye uhamuzi. Haya yote yalitokea kwa haraka sana, ndani ya muda mfupi, na muda huo kuna cruiser ipo speed inatokea uelekeo wa Kawe inakuja uelekeo wetu Mimi na yule jamaa maana tupo katikati ya barabara, na muda huo zimeruhusiwa gari zinazotoka upande wa Kawe kwenda makumbusho na zinazokata Kona kwenda mawasiliano, za kutokea Makumbusho zimepigwa pini.

Baada ya kuona yule jamaa nae kasimama hanipishi, nikaamua kupita kushoto kwake, ili yeye apite kulia, cha ajabu na yeye akaja upande ule ule, tukawa tumekaribiana kabisa. Baada ya kuhisi hapa tutagongwa na Ile cruiser kwa uzembe, nilijikusanya nguvu zangu zote, nikaamua kumpiga push yule jamaa ili wote tuangukie upande wake, maana sikuwa tena na namna.

Ajabu ni kwamba nilivyojipeleka kumpush, nilijikuta napush hewa, alaf nikaangukia upande wa pili, yule jamaa hakuwepo aisee. Kile kitendo cha kuanguka, Ile cruiser ilipita speed, ikanikosa kidogo sana na haikusimama Wala kupunguza mwendo. Watu waliokuwa maeneo Yale walijua nijirusha kukwepa Ile cruiser, kumbe Mimi nilikuwa nataka kumpush mtu, na wao hawakuona mtu yoyote.
Kuna mijitu itasema stori
 
Bahati yako ulimuwai kumpush sijui kama angekuwai ingekuweje
 
Kuna imani na hadithi mbalimbali katika jamii ambazo zinahusiana na uchawi, majini, na mapepo. Watu wengine wanasema kuwa wameona au kushuhudia vitu hivi, kama vile kukutana na marehemu, kubadilishiwa sehemu ya kulala, au matukio mengine ya kushangaza. Hata hivyo, ni muhimu kutambua kwamba masuala haya yanahusisha imani za kiroho na utamaduni, na kila mtu anaweza kuwa na maoni tofauti.

Katika kujibu swali lako, ni muhimu kutofautisha kati ya imani za kiroho na sayansi. Elimu ya biolojia inaweza kutoa ufafanuzi wa kisayansi juu ya mambo mengi yanayotokea katika maisha yetu. Kwa mfano, watu wanapokumbana na uzoefu wa kuona au kusikia vitu ambavyo havipo kimwili, inawezekana kuwa hii ni matokeo ya shughuli za ubongo ambazo zinaweza kuathiriwa na sababu mbalimbali kama vile matumizi ya dawa au magonjwa ya akili.

Hali duni ya maisha pia inaweza kuathiri jinsi watu wanavyoelewa mambo yanayotokea katika maisha yao. Umaskini, ukosefu wa elimu, na mazingira magumu yanaweza kuchochea imani za ushirikina au kuamini katika vitu ambavyo havina msingi wa kisayansi. Watu wanaweza kutafuta maelezo ya kiroho au ya kichawi kwa matukio ambayo hawawezi kuyaelewa kikamilifu kutokana na mazingira yao.

Hata hivyo, ni muhimu pia kuzingatia kwamba imani za kiroho na utamaduni zina umuhimu mkubwa katika maisha ya watu. Kwa baadhi ya watu, uzoefu wa kuona au kushuhudia vitu vya kiroho ni sehemu ya imani yao na ina umuhimu wa kipekee kwao. Hii inaweza kuwa njia ya kuunganisha na ulimwengu wa kiroho au kuwasaidia kupata maana katika maisha yao.

Ni vigumu sana kutoa jibu la moja kwa moja juu ya iwapo vitu kama uchawi, majini, na mapepo vipo au la. Sayansi haiwezi kukabiliana na mambo yote yanayohusiana na imani za kiroho, na imani za kiroho zinategemea mambo ambayo hayawezi kupimwa au kuonekana kimwili. Kila mtu ana uhuru wa kuamini au kutokubaliana na mambo haya, na ni muhimu kulinda uhuru huo wa kidini na maoni tofauti.

Kwa hiyo, jibu la swali lako linaweza kuwa kwamba imani za uchawi, majini, na mapepo zinaweza kuwa sehemu ya utamaduni na imani za kiroho za watu, na zinaweza kuathiriwa na elimu ya biolojia na hali duni ya maisha. Hata hivyo, ni muhimu kuheshimu maoni na imani za wengine na kutambua kwamba sayansi haiwezi kutoa majibu kamili kwa masuala yote ya kiroho.
Hivi ile ndege ya Malaysia kisayansi ilipotelea wapi?
 
Pale mwanza lilipo jengo la NSSF kwa sasa kulikua na bibi anamiliki eneo hilo yule bibi alikataa kutoka eneo hilo kupisha ujenzi pamoja jitihada zote za kumubembeleza zilishimdikaana ikabidi watumie nguvu huwezi amini bulldozer, excavator, wheel loader zote zilishishindwa kuvuja nyumba ya yule bibi inakitoka huko ikiwa nzima ikifika pale inapata breakdown kufupisha story yule bibi walimkalisha chini na kumsihi sana ndio akakubali nnacho kwambia sio story ya kusikia nlikua Mwanza miaka hio kaulize hio story

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Hapo iringa kuna sehemu ina kaburi la mzee nani sijui. Tanesco kila wakijaribu kupitisha line juu umeme ng'ambo ya pili hauwaki.wakileta greda kuhamisha kaburi full nyuki hawajulkani walikotoka. Je nayo ni illucination
 
Siwezi go in deep sababu sijafika hizo level in a nutshell mafanikio inahitaji jitihada kubwa ambapo wengi we are not ready for commitment and consistency.
Kufanikiwa ni kufata kanuni sababu kila mtu aliyefanikiwa alifanya KAZI na hiyo ndio basic foundation ya mafanikio.

Nilicho argue ni mtu anasema kufanikiwa ni uchawi ambapo naelewa uchawi ni vitu vya miujiza ya kufikirika tu ambavyo havina uhalisia
Ndo nilihitaji reference ya mtu aliyefanikiwa kwa namna hiyo ambaye hafanyi kazi na amefanikiwa.

Ukishafanya KAZI na una biashara hiyo tunaweza kuielezea katika kanuni za uchumi.
Labda mkuu nisaidie nani aliyefanikiwa kwa uchawi unayemfahamu?
BASHITE
 
Hivi ile ndege ya Malaysia kisayansi ilipotelea wapi?
We don't know...na kisa me sijui au watu hawajui doesn't mean unaweza kutunga kwamba majini ya uarabuni yaitwao the supernaturals waliiteka nyara kiroho na kupeleka katika dunia ya 7 afu me nikuamini tu kisa Sina majibu ya maswali yako...wat u r doing nikufill gaps in knowledge na superstitious beliefs kisa hujui kitu unasema uchawi...zamani watu walisema ukimwi uchawi ila wakaelimishwa na maambukizi yakapungua...kuamini katika uchawi hautatui tatizo coz hauleti maelezo yoyote kuhusu chanzo na suluhisho la tatizo coz mtu yoyote anaweza jitungia na kusema ni mambo ya kiroho
 
Usituletee novel na hekaya Kama evidence...kitabu hicho kinaamini punda na nyoka anayeongea...dunia ni flat..jua linazunguka dunia na linaweza kusimama..nyota ni ndogo kuliko mwezi na zinaweza anguka duniani...etc.. so Tuletee uthibitisho wa maana
umeandika maelezo mengi yasiyoeleweka sawa na ujinga.
 
Uchawi upo ndugu zangu.

Kuna rafiki yangu mmoja alikuwa anagombea kiwanja cha babu yake yeye na mjomba wake, dogo babu yake alimkatia eneo kubwa tu na akafanikiwa kujenga.

Mjomba wake akajiapiza wewe dogo si babu yako anakupenda sana sasa utaona.

Hivi sasa dogo ni kichaa dah, yaani inasikitisha watu wameangaika sana kumtibu lakini wapi ukumuona utamuonea huruma.
Uchawi upo kwa sababu ni asili na jadi ya Muafrika, ila kwa sasa wengi wanapata matatizo ya afya ya akili na kwa kukosa elimu na ufahamu wa jambo hili huishia kuamini kulogwa. Nina mdogo wangu alipata shida hiyo akawq chizi kabisa na tukahangaika sana ila mwisho aliponea hospitali na mpaka sasa anaendelea na dawa ila kwa alivyokuwa na sasa tunasema ni mzima.
 
Back
Top Bottom