Kitu gani umewahi kuona ukaamini uchawi upo?

Kitu gani umewahi kuona ukaamini uchawi upo?

Kuna siku nilikuwa natoka kwenye mihangaiko yangu. Sasa kufika maeneo ya njia panda ya Mwenge nikawa navuka barabara. Wakati navuka, kuna jamaa naye akawa anavuka in opposite direction (tukawa tunaangaliana).

Sasa tukawa kama tunataka kupamiana. Maana nikienda kushoto, jamaa nae anaenda kushoto. Nikienda kulia, jamaa nae anaenda kulia, hadi tukawa tumekaribiana kabisa. Nikaganda kidogo ili kumruhusu yeye afanye uhamuzi, then tupishane, jamaa nae akawa kama vile ananisikilizia Mimi ndo nifanye uhamuzi. Haya yote yalitokea kwa haraka sana, ndani ya muda mfupi, na muda huo kuna cruiser ipo speed inatokea uelekeo wa Kawe inakuja uelekeo wetu Mimi na yule jamaa maana tupo katikati ya barabara, na muda huo zimeruhusiwa gari zinazotoka upande wa Kawe kwenda makumbusho na zinazokata Kona kwenda mawasiliano, za kutokea Makumbusho zimepigwa pini.

Baada ya kuona yule jamaa nae kasimama hanipishi, nikaamua kupita kushoto kwake, ili yeye apite kulia, cha ajabu na yeye akaja upande ule ule, tukawa tumekaribiana kabisa. Baada ya kuhisi hapa tutagongwa na Ile cruiser kwa uzembe, nilijikusanya nguvu zangu zote, nikaamua kumpiga push yule jamaa ili wote tuangukie upande wake, maana sikuwa tena na namna.

Ajabu ni kwamba nilivyojipeleka kumpush, nilijikuta napush hewa, alaf nikaangukia upande wa pili, yule jamaa hakuwepo aisee. Kile kitendo cha kuanguka, Ile cruiser ilipita speed, ikanikosa kidogo sana na haikusimama Wala kupunguza mwendo. Watu waliokuwa maeneo Yale walijua nijirusha kukwepa Ile cruiser, kumbe Mimi nilikuwa nataka kumpush mtu, na wao hawakuona mtu yoyote.

Pole mkuu lakini uchawi hakuna ni stori.
Hii kitu imetokea watu wengi ulishawahi sikia kitu kinaitwa entoptic phenomena?
 
Ndio nini hiyo? Elezea

Mkuu hii kitu kwako haifit entoptic phenomena ILA hii ni hallucinations.
Mfano kusikia sauti ya mtu analia au anaongea lakini hakuna mtu huyo.
Au kuona mtu au vitu ambavyo hakuna mtu mwingine anayeviona kama vile kuona mtu amesimama karibu nawe lakini kiuhalisia hakuna huyo mtum

Hallucinations huwa inasababishwa na vtu vingi mojawapo ni magonjwa ya akili
Ila entoptic phenomena huwa inasababishwa na muundo wa ndani wa jicho lako.
 
Nafahamu hallucinations zinavyokuwa, ila naweza kukuthibitishia kwangu haikuwa hallucination.
 
Kilitoweka mbele yangu, hakikuwepo tena
Ndivyo hallucinations ilivyo.

Rafiki yangu alipoteza mama yake mzazi, nilienda kulala kwake kama kumfariji kama week mbili baadae baada ya kifo cha mama yake.

Nakumbuka tupo tuna watch WWE kwenye Tv akasimama gafla anaongea Mama halafu yupo anatabasamu huku anafuata uelekeo wa kutoka nje.

Ikabidi nimshtue anaendelea kuita mama mpaka anafika nje ya geti ndo namshika kwa nguvu ananiambia kapotea alikuwepo hapa na kilio juu.

Yupo mama mitaa ya ukonga mombasa, kapoteza mtoto wake wa kiume, yule jamaa alikuwa anauza genge barabarani huyu mama mpaka sasa anaweza akatoka kwake akasimama upande wa pili wa barabara anaita jina la mwanae ile sehemu ambapo genge lipo na mpaka sasa lipo. Anamwita jina lake halafu anamwambia mwanangu niletee machungwa. Na mtoto alishafariki miezi3 inakaribia.

Hiyo ni mifano michache hakuna uchawi hapo.
Nenda soma serer mythology za senegal na gambia.
 
Sikuwa na majonzi, sikuwa stressed kiivyo, kwanini ni hallucinate? Alaf mtu niliyemuona, sikuwa na mfahamu hapo kabla na sikuwahi kumuona tena
 
Sikuwa na majonzi, sikuwa stressed kiivyo, kwanini ni hallucinate? Alaf mtu niliyemuona, sikuwa na mfahamu hapo kabla na sikuwahi kumuona tena

Hallucinations ni uzoefu usio wa kawaida wa kuona, kusikia, au kuhisi vitu ambavyo havipo kimwili au kwenye mazingira halisi.
Halafu tazama sentensi yako sikuwa "stressed kihivyo"
Mkuu analyse mimi binafsi huwa siamini uchawi wala uwepo wa mungu.
Hata mimi hallucinations nisha experience na siyo lazima uwe stressed unaweza kuwa kuwa ecstatic na BADO hii hali ikakupata.
Na wachache naowafahamu waliopitia HALI hii huwa kuna vitu vinaendelea kwenye maisha yao havipo Sawa.
 
Niliishi nyumba moja magomeni mikumi kwa miaka 7 na wenye nyumba ni wachawi bibi na babu, usiku wa manane nikiamka kwenda uani (kilikua choo cha nje) naskia wanacheza ngoma na kuimba hapo sebuleni kwao,
Siku moja bibi akaniambia wameletewa nyama pori wakanipa hapo sikula kile chakula nkakiweka ili asubuhi niweke kwa mfuko nkamwage maana sikuzielewa zile nyama zilikua kama zimekaushwa hivi ila ukiipasua kati ni mbichi kabisa na waliniwekea nyama nyingi sana, asibuhi mapema naamka nimwage chakula nkakuta nyama zote hazipo na hakukua na panya mle ndani,
Siku nyingine nilisafiri kwenda kijijini nkamuomba babu alale chumbani kwangu ili kusiibiwe (chumba kilikua cha nje) kipindi hicho vibaka wa usiku walikua wanaiba sana, na mara nyingi nilikua nawaona wanachungulia dirishani,
Sasa kurudi safari nilikaa huko kama wiki 2 nkakuta kapeti limetoboka toboka sanaa kama mtu karukaruka na viatu vyenye ncha kali sana nkajua tu hawa washenzi walihamishia ngoma zao chumbani kwangu nkavunga tu wala sikuuliza maisha yakaendelea.
Aisee dunia inamambo mengi eeh...
 
Hallucinations ni uzoefu usio wa kawaida wa kuona, kusikia, au kuhisi vitu ambavyo havipo kimwili au kwenye mazingira halisi.
Halafu tazama sentensi yako sikuwa "stressed kihivyo"
Mkuu analyse mimi binafsi huwa siamini uchawi wala uwepo wa mungu.
Hata mimi hallucinations nisha experience na siyo lazima uwe stressed unaweza kuwa kuwa ecstatic na BADO hii hali ikakupata.
Na wachache naowafahamu waliopitia HALI hii huwa kuna vitu vinaendelea kwenye maisha yao havipo Sawa.
Nilijua lazima ungeshikiria hii sehemu. Nimesema sikuwa stressed kivile, kutokana na kwamba, life letu kwa ujumla ni stress tu. Kwahiyo nilikuwa under normal circumstances (Tz life)
 
Uchawi upo ndugu zangu.

Kuna rafiki yangu mmoja alikuwa anagombea kiwanja cha babu yake yeye na mjomba wake, dogo babu yake alimkatia eneo kubwa tu na akafanikiwa kujenga.

mjomba wake akajiapiza wewe dogo si babu yako anakupenda sana sasa utaona.

Hivi sasa dogo ni kichaa dah, yaani inasikitisha watu wameangaika sana kumtibu lakini wapi ukumuona utamuonea huruma.
359ec69df741e21c66c97ec9f12363ec.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilijua lazima ungeshikiria hii sehemu. Nimesema sikuwa stressed kivile, kutokana na kwamba, life letu kwa ujumla ni stress tu. Kwahiyo nilikuwa under normal circumstances (Tz life)

Hapana mkuu sijatazama hapo tu.

Ungemalizia na huko chini kabisa, unaweza kuwa ecstatic na BADO hali hii ya hallucinations ikakupata.

Mimi binafsi huwa sina shida na imani za watu ILA kwenye swala la kuthibisha ndo huwa kuna matatizo. Naheshimu imani YAKO.
 
Back
Top Bottom