Kitu gani umewahi kuona ukaamini uchawi upo?

Kitu gani umewahi kuona ukaamini uchawi upo?

[emoji1787]Mbona unaone mwenyewe na wajinga wenzako au una dunia yako. Water is real, hatuwezi kubishana water is real or fake coz kila mtu mwenye macho anaona maji, same as fire same as trees etc [emoji1787]kitu ambacho mtu mmoja mmoja anakiona hizo ni hallucinations ndo maana tukilala hatuna ndoto sawa. Mwingine ataota uchawi mwingine ataota utajiri hivyo
Yaani waafrika mkisoma ndio mnakua wajinga zaidi

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Mkuu alinitoka bila kujua tena Alikua kwenye kiboksi...
Uchawi upo tena unafanya kazi...
Ukicheza tu wamekuua

Hahahaha
Mkuu,
Smart gang pole sana ILA hapo ungeenda tu kupigwa pesa.
Kwanza dada yako alikuwa kwenye desperate situation kwamba unadai alirogwa.
Huenda ulikuwa depressed kiasi cha kushindwa kufocus hivyo ndege wako akaruka wewe ukiwa umejawa mawazo.
Na umekiri kwamba alikutoka na siyo kuyayuka hio ni hali ya kawaida tu wala si uchawi.
 
Kwetu vijijini Kuna mzee aliangusha kibunda chake Cha pesa na akajua mtu aliyeziokota.Mzee alimwambia huyo jamaa Kama hataki nongwa amrudishie tu hela zake Jamaa akamkatalia kbsa akasema hakuokota pesa yoyote.

Mzee aliamua kuachana naye ila kabla ya kuondoka alimwambia atapata majibu.Aisee kilichomkuta huyo jamaa aliyeokota pesa huwezi amini.Alifiqa na wanawe 2 pamoja na mjukuu mmoja chini ya Mwezi mmoja.
Kwani ilibidi afiwe ndani ya muda gani?
 
Kuna siku nilikuwa natoka kwenye mihangaiko yangu. Sasa kufika maeneo ya njia panda ya Mwenge nikawa navuka barabara. Wakati navuka, kuna jamaa naye akawa anavuka in opposite direction (tukawa tunaangaliana).

Sasa tukawa kama tunataka kupamiana. Maana nikienda kushoto, jamaa nae anaenda kushoto. Nikienda kulia, jamaa nae anaenda kulia, hadi tukawa tumekaribiana kabisa. Nikaganda kidogo ili kumruhusu yeye afanye uhamuzi, then tupishane, jamaa nae akawa kama vile ananisikilizia Mimi ndo nifanye uhamuzi. Haya yote yalitokea kwa haraka sana, ndani ya muda mfupi, na muda huo kuna cruiser ipo speed inatokea uelekeo wa Kawe inakuja uelekeo wetu Mimi na yule jamaa maana tupo katikati ya barabara, na muda huo zimeruhusiwa gari zinazotoka upande wa Kawe kwenda makumbusho na zinazokata Kona kwenda mawasiliano, za kutokea Makumbusho zimepigwa pini.

Baada ya kuona yule jamaa nae kasimama hanipishi, nikaamua kupita kushoto kwake, ili yeye apite kulia, cha ajabu na yeye akaja upande ule ule, tukawa tumekaribiana kabisa. Baada ya kuhisi hapa tutagongwa na Ile cruiser kwa uzembe, nilijikusanya nguvu zangu zote, nikaamua kumpiga push yule jamaa ili wote tuangukie upande wake, maana sikuwa tena na namna.

Ajabu ni kwamba nilivyojipeleka kumpush, nilijikuta napush hewa, alaf nikaangukia upande wa pili, yule jamaa hakuwepo aisee. Kile kitendo cha kuanguka, Ile cruiser ilipita speed, ikanikosa kidogo sana na haikusimama Wala kupunguza mwendo. Watu waliokuwa maeneo Yale walijua nijirusha kukwepa Ile cruiser, kumbe Mimi nilikuwa nataka kumpush mtu, na wao hawakuona mtu yoyote.
Damn

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahaha
Mkuu,
Smart gang pole sana ILA hapo ungeenda tu kupigwa pesa.
Kwanza dada yako alikuwa kwenye desperate situation kwamba unadai alirogwa.
Huenda ulikuwa depressed kiasi cha kushindwa kufocus hivyo ndege wako akaruka wewe ukiwa umejawa mawazo.
Na umekiri kwamba alikutoka na siyo kuyayuka hio ni hali ya kawaida tu wala si uchawi.
Walikua wamemzingua Mkuu Wangu.
Ndugu ni hatari kuliko unavowadhania
Yakikukuta ndo utaelewa.
Alipona lakini
 
Back
Top Bottom