Kitu gani umewahi kuona ukaamini uchawi upo?

Kitu gani umewahi kuona ukaamini uchawi upo?

We hunielimishi...unanipa story, story ambazo unajua wewe tu na kijiwe chako...huo sio ushahidi. 🤣🤣Leta ushahidi ambao unaeleweka. Mbona hatubishani kama maji au moto au mbwa wapo?
Tuje kwenye sayansi, kwanini sayansi imeshindwa kutuonyesha upepo upoje ni unavuma tu sayansi haiwezi kufanya chochote kuhusu upepo, kwanini tusiifanye dunia ikawa usiku tu au ikawa mchana tu, au tukasimamisha mda au tuurudishe mda nyuma. Hatuwezi kufanya jua lichomoze magharibi? why science has nothing to do with this?
(Nb usije ukasema hiyo yenyewe ni sayansi)
 
🤣🤣🤣Kama Nini? Wewe uchawi usikuweke ukomo. Ungeamini mauchawi si usingeenda shule, ungeenda kwa hao waganga kwa ajili ya elimu, kwa ajili ya sawa ukiumwa, mbona unatumia Simu si Sayansi hio, mbona una chanjo kibao mwilini si Sayansi hio...amini mauchawi yako tuone ka utamaliza siku. Sisi sio watu wa porini.
Sayansi yenyewe inatokana na uchawi unajuwa hilo?
 
Imani haiwezi kuwa kweli ndo maana inaitwa Imani..nikiamini Mimi ni ng'ombe hata niamini vipi siwezi kuwa ng'ombe same as majini yenu it doesn't matter how strong u believe hayapo na hayatakuwepo
hiyo ni siasa, me naweza kusema wewe ni wa kike na nikaja na evidence😁
 
Last born wetu aliumwa sana mika ile, yaani aliumwa sana. Mwisho mama akaamua aende kwa kaka yake Dar hapo sinza ili amuunganishe na jirani yake aende muhimbili. Bahati nzuri alimungqnisha na Dr mwingine aliyekuwa anafanya Tumaini hosp ile iliyokuwa karibu na diamond hall pale. Pale alichomwa sindano nyingi tuu na madawa kibao miezi mitatu mtoto akapona vizuri. Baadae wakafunga safari wakarudi home miye teena na kiherehere changu nikachukua wembe nikamnyoa nywele. Maana nywele zikuwa nyekunduku km mtu kapaka ina. Nilimnyolea nje basi upepo ulipokuwa unapuliza kwenye kile kiapara yakaanza kutoka pamba, pamba kabisa. Nilitoka nduki mpk ndani kwa Mama na Baba nikasema oneni mtoto anatoka pamba/sufi kichwani. Baba akasema hii hatari.Nilizikusanyq zile pamba nikasema akikua ntamuonyesha sasa ni mika 27 imepita na dogo yupo njema ni injinia huko Soudia anapiga kazi.
 
Haina shida. Unataka kila mtu awe bill gates au...Ila kufanikiwa kwa mmoja na kutokufanikiwa kwa mwingine ni mambo ya basic economics tu sio lazma uweke uchawi..kuweka uchawi ni kuforce ujinga katika mada ya kisomi Kama uchumi na income inequality in nations..unakuwa hausolve tatizo kwa kusema tu "ni uchawi" ndo maana nasema approach yako ni ya kitoto
Wewe unaelewa point yangu hapa ni ipi kweli? Wote hatuwezi kuwa kama Bill gate hata kama tutafanya vile vile kama alivyofanya Bill gate tena katika mazingira hayo hayo, na hapo ndio naposema kwamba mafanikio ni zaidi ya kufuata hizo kanuni na juhudi ndio hoja yangu hapa na si uchawi. Mtu anaweza kufanya kazi fulani isifanikiwe japo wengine wanafanikiwa ila akabadili kazi akafanikiwa ndio nachuzungimumzia hapa.
 
Washawahi kuchunguza ndo wakajua it's fake shit. Coz wao pia waliamini. Walikuwa wanachoma wachawi moto miaka ya 1500 mpaka 1700 Ila baada ya technology na elimu kukua wameacha coz wanaelewa. Sasa sisi tuliochelewa ndo tunaamini bado ila na sisi tutapita hio stage ni maendeleo tu... maendeleo sio barabara na majengo Ila fikra na tamaduni pia
Walichunguza vp unaweza ukaelezea? Hata Arabuni kuna nchi ukigundulika unajihusisha na uchawi ni kosa kisheria unahukumiwa na hiyo si kwa sababu wanaona uchawi si kweli.
 
Uchawi upo ndugu zangu.

Kuna rafiki yangu mmoja alikuwa anagombea kiwanja cha babu yake yeye na mjomba wake, dogo babu yake alimkatia eneo kubwa tu na akafanikiwa kujenga.

mjomba wake akajiapiza wewe dogo si babu yako anakupenda sana sasa utaona.

Hivi sasa dogo ni kichaa dah, yaani inasikitisha watu wameangaika sana kumtibu lakini wapi ukumuona utamuonea huruma.
Umeme kuzuiwa kukatisha makaburini Tanangozi Isimila Iringa
 
Embu tazama hawa ni majirani wote ni watu wa arusha ni askari POLISi wote hawana cheo.
Wanapokea mshahara Sawa. Lakini huyu mmoja mbali na ufinyu wa muda, ana vibanda vya huduma za kifedha, ana pikipiki 2 zinazomletea hesabu ana kiwanja sehemu moja ipo chanika inaitwa zingiziwa na huwa anakopesha wenzake kwa riba. Huyo rafiki yake yeye ni pombe na pikipiki anayo lakini anasema hawezi kwenda kazini bila pikipiki Wana mwaka wa3 tangu waajiriwe.

Utofauti ni commitment yaani mmoja yupo radhi kuumia kwa muda mrefu kupata matunda endelevu lakini huyu mwingine hayupo tayari.

swali tutajuaje hao unaosema Wana juhudi na kweli wanaweza kuwa na juhudi kazini lakini wakakosa nidhamu, na commitment kwenye mishahara au pesa wanazozipata? Kwanini useme ni uchawi na tusikirie huenda kuna sababu ambazo ni logical?
Nimesema uchawi kwenye nini?
Hakuna niliposema mafanikio ni uchawi tu ndio unahusika.

Tuelewana kwanza hapo.
 
Nimesema uchawi kwenye nini?
Hakuna niliposema mafanikio ni uchawi tu ndio unahusika.

Tuelewana kwanza hapo.
Rekebisha hakuna mafanikio yenye uchawi kwa namna yoyote ile as long as huyo mtu tayari anafanya kazi
Ondoa "hakuna sehemu niliposema mafanikio ni uchawi tu"
sababu neno uchawi ni stori za kufikirika za miujiza.
 
Embu tupe connection hiyo?
Uchawi ni imagination, means ukitaka unaweza ukajitengenezea wa kwako. Sayansi ni kuleta imagination kuwa reality, na vyote sio rahisi kuvifanya, achana na hii sayansi ya simbampole, ambayo kila mtu ameikariri darasani na bado hatujavumbua kitu chochote. Sayansi ilianza kama mchakato ni fikra za watu wengi lakini moja alikuja kujaribu,ilipoleta matokea chanya ikawa ndo matokeo ya sayansi. Na sayansi si hadi usome shule kama simbampole yeye sio mwanasayansi, yeye ni kama anasoma tu vitabu vya hadithi ili aendelee kuishi.
Kuleta ile fikra kuwa reality kwa akili ya kawaida ya kibinadamu haiwezekani, kuna higher powers ambayo simbampole haamini kama ipo, ndo maana ukifuatilia vizuri unaweza ukaona mbona kama mtu aliyegundua kitu flani aliibatisha tu, kama sio higher powers kila mtu angejigundulia chake, Ni kweli fikra hazifanani mbona fikra zetu hazileti chochote, ni kwamba tumeshindwa kuitumia powers tulizonazo, na tulishafanya mistake kutokea mwanzo.
 
SimbaMpole123 njoo utupe evidence ya sayansi ya kwako, achana na sayansi ya ulaya ambayo unashadadia uhalisia bila kujua chimbuko
 
Ni hivi uchawi ni stori za miujiza ya kufikirika mfano mtu kuyayuka gafla hilo haliwezi kuelezewa. Lakini tukiweza kulielezea haliwezi tena kuwa uchawi ambazo ni ignorance ya watu tu.

Nipe mfano wa mtu aliyefanikiwa kwa uchawi ambaye utajiri wake huwezi kuulezea in a logic form.

Kuhusu kufanya kazi Sawa na juhudi Sawa soma nilichoandika hapo juu

Au unataka nikupe mfano mwingine relevant?
Unachokifanya wewe hapa ni kupinga tu uchawi kwa sababu hauamini tu uchawi ila hautoi hoja za msingi kuonyesha kuwa huo uchawi haupo. Uchawi sio miujiza uchawi ni ujuzi wa kipi ufanye ili kitokee nini au kupata athari gani huo ndio uchawi.

Sasa wewe unataka tukubali kwamba kila anayefanya kazi na mafanikio basi hayo mafanikio ni kutokana na kufanya kwake kazi tu bila kujali kama kama mtu huyo ana matumizi mabaya ya pesa na hana nidhamu ya kazi ila hapo hapo kwa mtu ambaye anafanya kazi kwa juhudi ila hana mafanikio unataka tuamini kuwa itakuwa hana nidhamu ya kazi na ana matumizi mabaya ya pesa.
 
Uchawi ni imagination, means ukitaka unaweza ukajitengenezea wa kwako. Sayansi ni kuleta imagination kuwa reality, na vyote sio rahisi kuvifanya, achana na hii sayansi ya simbampole, ambayo kila mtu ameikariri darasani na bado hatujavumbua kitu chochote. Sayansi ilianza kama mchakato ni fikra za watu wengi lakini moja alikuja kujaribu,ilipoleta matokea chanya ikawa ndo matokeo ya sayansi. Na sayansi si hadi usome shule kama simbampole yeye sio mwanasayansi, yeye ni kama anasoma tu vitabu vya hadithi ili aendelee kuishi.
Kuleta ile fikra kuwa reality kwa akili ya kawaida ya kibinadamu haiwezekani, kuna higher powers ambayo simbampole haamini kama ipo, ndo maana ukifuatilia vizuri unaweza ukaona mbona kama mtu aliyegundua kitu flani aliibatisha tu, kama sio higher powers kila mtu angejigundulia chake, Ni kweli fikra hazifanani mbona fikra zetu hazileti chochote, ni kwamba tumeshindwa kuitumia powers tulizonazo, na tulishafanya mistake kutokea mwanzo.

The whole message is just ad hominem fallacy.
Does science can't explain how the imagination emerge on our brains?

Je unafahamu chemicals zinakuwa released from neurons kama neurotransmitter?
Turudi tena hapa uchawi ni vitu vya kufikirika ambavyo ni vya miujiza na havina ukweli wowote kama kusikia mtu anayeyuka lakini huwezi thibitisha hilo.

exactly tunaanza ku imagine then we put that imagination into reality, tunasikia watu Wanapaa na ndege usiku au na mbweha lakini hizo zinabaki ni imagination tungethibitisha hilo mpaka ingewekwa kwenye uhalisia

Embu tuelezee connection iliyopo ?mpaka sasa sijaona connection
 
Unachokifanya wewe hapa ni kupinga tu uchawi kwa sababu hauamini tu uchawi ila hautoi hoja za msingi kuonyesha kuwa huo uchawi haupo. Uchawi sio miujiza uchawi ni ujuzi wa kipi ufanye ili kitokee nini au kupata athari gani huo ndio uchawi.

Sasa wewe unataka tukubali kwamba kila anayefanya kazi na mafanikio basi hayo mafanikio ni kutokana na kufanya kwake kazi tu bila kujali kama kama mtu huyo ana matumizi mabaya ya pesa na hana nidhamu ya kazi ila hapo hapo kwa mtu ambaye anafanya kazi kwa juhudi ila hana mafanikio unataka tuamini kuwa itakuwa hana nidhamu ya kazi na ana matumizi mabaya ya pesa.

Naomba unipe reference ya kamusi gani inayoelezea hiyo maana ya uchawi?
Mimi nimejaribu ku compare watu wawili ambao wanakwenda wote kazini, wanalipwa Sawa na bado kuna mmoja anamzidi mwenzake.
Mmoja yupo radhi kumaliza mshahara wake kwenye pombe ILA mwingine yupo radhi ajibane akanunue kitu kitachomazilishia zaidi.

Naomba nipe maana ya uchawi uliyoitoa hapo umeipata KWenye kamusi ipi?
 
The whole message is just ad hominem fallacy.
Does science can't explain how the imagination emerge on our brains?

Je unafahamu chemicals zinakuwa released from neurons kama neurotransmitter?
Turudi tena hapa uchawi ni vitu vya kufikirika ambavyo ni vya miujiza na havina ukweli wowote kama kusikia mtu anayeyuka lakini huwezi thibitisha hilo.

exactly tunaanza ku imagine then we put that imagination into reality, tunasikia watu Wanapaa na ndege usiku au na mbweha lakini hizo zinabaki ni imagination tungethibitisha hilo mpaka ingewekwa kwenye uhalisia

Embu tuelezee connection iliyopo ?mpaka sasa sijaona connection
unajuwa hata baadhi ya hoja za kisayansi bado ipo kwenye imagination, means imeshindikana, mfano mtu kuzeeka
 
Back
Top Bottom