Kitu gani umewahi kuona ukaamini uchawi upo?

Kitu gani umewahi kuona ukaamini uchawi upo?

Hili ni fundisho kwenu kwamba mtu akikueleza matatizo yake uache kujifanya MWANASAYANSI, na badala yake umsikilize kwa MAKINI na umpe msaasa STAHIKI.

Yeah Chief

Ila vitu vingine sio vya kujifanya unataka uvitatue yaani kujifanya tatzo kama lako kabsa, unatakiwa ujitahidi tu unapoweza na uachane nalo

Africa huku tunaumizana bila sababu ukijifanya kimbele mbele sanaa watu wanakutupia wewe hayo mauchawi uangaike na kimbele mbele chako

Hatari aisee
 
Kwani maneno yote tunayotumia humu tumetoa tafsiri zake kwenye kamusi? Unataka kuniambia jinsi ulivyoeleza wewe uchawi umetoa kwenye kamusi? Mimi nimeeleza uchawi kwa jinsi navyojua unavyofanyika.

Kamusi niliyo nayo hapa inaeleza hivi kuhusu uchawi:ni ufundi wa kutumia dawa mitishamba au vitabu maalumu vya uganga ili kuleta madhara kwa viumbe.

Sasa kutoka kwenye hiyo mifano yako ndio unataka kuhitimisha kwamba wasiofanikiwa ni kwa sababu hawajinyimi na hutumia hovyo pesa zao? Na kumbuka sio kila mafanikio yanahusu mali kwamba upate pesa.

Mkuu kamusi zote zipo kwenye mitandao naomba unipatie hiyo kamusi ni chapisho gani na mwaka gani?

mimi nimeeeezea sababu kwa kutumia majirani zangu POLISi wawili embu tuelezee wewe hiyo maana YAKO ya uchawi uliyoandika hapo na kufanikiwa KWA mtu?
 
Ulimwengu wa roho ni software huwezi kuuona kwa macho ya mwili wala kuushika kwa mikono yako...tusichanganye vinavyoonekana na visivyoonekana, tukafanya hiki ndio kile na kile ndio kile
-simu unayo na unafanya mawasiliano yote ninini kinafanyika mpaka umudu kufanya hayo yote?

Akili unayo na ukiulizwa hutabisha je ukiambiwa ionyeshe utaweza?
-Usingizi unao je kufumba macho ndio kulala usingizi?
Ni vema kuelewa kwama uchawi ni sehemu ya ulimwengu usioonekana, upo lakini hauna ithibati za kisayansi kwakuwa huwezi kuushika nk ....

Kuwepo kwa uchawi ni kitu cha kwanza lakini kuwepo na mtu akaweza kuutumia huo uchawi kwa muktadha fulani ni kitu kingine kabisa
Malumbano mengi pia yametokea kwenye kutaka ithibati za kuwepo kwa uchawi! Hizi ni fikra tengefu..

Kama ilivyo nguvu iliyopo kwenye mashine yoyote ana mwanga kwenye taa yoyote ama software kwenye kifaa chochote cha kielectronic...kama ulivyo uhai ndani ya mwili
Tafakari....
By Mshana Jr
 
kwani sayansi yenyewe imetoka wapi, si wa wazungu, huyo jamaa anabishia asili
Mtu anakwambia kabisa kuwa huko wenzetu waliwauwa wachawi hivyo kiasi kikubwa wakatokomeza uchawi na kukaja kuzaliwa kizazi ambacho hakijihusishi sana na uchawi, sasa hapo wanataka tuone et wazungu hawaamini uchawi kwa sababu tu wana elimu. Watu wanarogana na kutibiana afrika halafu mtu anakuja anataka uwe na mitazamo kama ya wazungu na kupinga tu hakuna uchawi kisa wazungu hawaamini uchawi.
 
Naomba unipe reference ya kamusi gani inayoelezea hiyo maana ya uchawi?
Mimi nimejaribu ku compare watu wawili ambao wanakwenda wote kazini, wanalipwa Sawa na bado kuna mmoja anamzidi mwenzake.
Mmoja yupo radhi kumaliza mshahara wake kwenye pombe ILA mwingine yupo radhi ajibane akanunue kitu kitachomazilishia zaidi.

Naomba nipe maana ya uchawi uliyoitoa hapo umeipata KWenye kamusi ipi?
Mkuu naomba nikuambie kitu

Kwangu uchawi naweza kukuambia ni miujiza/magic/maajabu/mazingaombwe yani sioni neno linalofit

Alafu niliona kama umesema wazungu hawaamini uchawi ushawahi kuangalia American Got talent?? Mtafute mdada anaitwa Riana

Kingine inawezekana cicre yako pia au hujatembea...

Tuliosoma shule za bweni wengi Tushaona/Kusikia vitu vingi vya kutisha miss corridor,Mtu mrefu ambae mwisho humuoni,Vimbilikimo... binafsi sitapenda kuviongelea kwa upande wangu maana hata nikikuambia hutaamini na najua hutaamini kwasababu haukuona wewe
 
Mtu anakwambia kabisa kuwa huko wenzetu waliwauwa wachawi hivyo kiasi kikubwa wakatokomeza uchawi na kukaja kuzaliwa kizazi ambacho hakijihusishi sana na uchawi, sasa hapo wanataka tuone et wazungu hawaamini uchawi kwa sababu tu wana elimu. Watu wanarogana na kutibiana afrika halafu mtu anakuja anataka uwe na mitazamo kama ya wazungu na kupinga tu hakuna uchawi kisa wazungu hawaamini uchawi.
Don't Watch Sacred Riana If You're Scared Of The Dark - America's Got Talent 2018 / America's Got Talent
Screenshot_20230803-103443_YouTube.jpg
 
Mkuu naomba nikuambie kitu

Kwangu uchawi naweza kukuambia ni miujiza/magic/maajabu/mazingaombwe yani sioni neno linalofit

Alafu niliona kama umesema wazungu hawaamini uchawi ushawahi kuangalia American Got talent?? Mtafute mdada anaitwa Riana

Kingine inawezekana cicre yako pia au hujatembea...

Tuliosoma shule za bweni wengi Tushaona/Kusikia vitu vingi vya kutisha miss corridor,Mtu mrefu ambae mwisho humuoni,Vimbilikimo... binafsi sitapenda kuviongelea kwa upande wangu maana hata nikikuambia hutaamini na najua hutaamini kwasababu haukuona wewe
Nionyeshe niliposema wazungu hawaamini uchawi?

Nimesoma boarding na hiyo stori ya miss corridor nimeandika post za juu huko nikimjibu jamaa kuhusu hallucinations.

Ndio maana nasema uchawi ni stori za kufikirika hazina uthibitisho.
Asante kwa kunielewa.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Aaah kmk, si mmelala, Sasa usingizi ni uchawi jamani..story zingine bana
Acha uchawi dogo, siku zenu zimefika mwisho.

Ngoja unyofolewe miguu na watu wenye hasira kali [emoji23][emoji119]
 
Mimi Iko hivi ila mpaka Leo sijui ni mauchawi au Nini huko Moshi vijijini!

Kipindi Niko around 12 Mimi na machalii zangu tulikua na tabia ya kuiba parachichi nyakati za usiku kwa lengo la kuuza siku ya soko kujipatia shilingi mia Tano au buku mbili!

Lengo lilikua kupata pesa ya daftari,kalamu,soksi wali nyumbani na extra pro max mandazi!

Tulikua watatu tunaamka usiku saa mbovu (tulipendelea nyakati za mbalamwezi tuone vizuri) mmoja kazi yake ni Kuokota parachichi, mwingine kujaza kwenye kiroba alafu mwingine ni Mimi msoma gepu(anayeangalia usalama)

Iyo siku sitasahau tulivuna parachichi za kuzidi,nakumbuka kulikuwa na mbalamwezi (full moon) kutizama kwenye Ile nyumba tunayoiba parachichi niliona kitu kirefu cheupe kimechongoka juu kama mshale kinatufuata huku kikiyumba na kilikua kama kinabadilika rangi za bluu!

Nilichofanya Sasa nilikimbia na wale machalii wote walikimbia kivyao!

Tulikutana uwanja wetu asubuhi hio hio,Kuna alie umia na miba mwingine kapoteza ndala!

Mpaka Leo hii sisi ni madingi tukiwa tunakula bia nikiwakumbusha wanacheka tunajikuta tunaagiza bia zingine
 
Mkuu kamusi zote zipo kwenye mitandao naomba unipatie hiyo kamusi ni chapisho gani na mwaka gani?

mimi nimeeeezea sababu kwa kutumia majirani zangu POLISi wawili embu tuelezee wewe hiyo maana YAKO ya uchawi uliyoandika hapo na kufanikiwa KWA mtu?
Ni Kamusi ya kiswahili sanifu ya 1981, Isbn 0195723694.

Nimekuuliza maswali haujajibu.
 
Nionyeshe niliposema wazungu hawaamini uchawi?

Nimesoma boarding na hiyo stori ya miss corridor nimeandika post za juu huko nikimjibu jamaa kuhusu hallucinations.

Ndio maana nasema uchawi ni stori za kufikirika hazina uthibitisho.
Asante kwa kunielewa.
Ni wapi nimesema nimekuelewa??

Nimejaribu kukuelewesha nani anatakiwa kumuelewa mwenzake?
 
Watakwambia hiyo kama movie tu zinatengenezwa.
Binafsi siwakatalii...Kuna vitu kama hujavishuhudia ni vigumu kuamini

Ila tatizo lao ni kujihisi wanajua pale ambapo hawajui kama hawajui

Maana halisi ya watu wa dizaini hii tunawaita wajinga
 
Ni Kamusi ya kiswahili sanifu ya 1981, Isbn 0195723694.

Nimekuuliza maswali haujajibu.

Nimejibu na kukupa mifano ya POLISi majirani zangu wawili.
KWA muktadha wa tafasiri yako tupe connection ya mtu kufanikiwa kwa uchawi?
Mimi nimekujibu na nimetolea mifano mingi ambayo watu wote wamefanikiwa kwa kufanya kazi. Nipe mfano wa mtu aliyefanikiwa kwa uchawi?
 
Back
Top Bottom