Kitu gani umewahi kuona ukaamini uchawi upo?

Kitu gani umewahi kuona ukaamini uchawi upo?

Umejielezea vzuri ILA umeniangusha kusema kuna namna nyuma ya pazia!

Ulipaswa uthibitishe namna nyuma ya pazia kwa kutupa positive link up na wao kupata mazao mengi zaidi ya wengine regardless wamefata kanuni Sawa.

Shida ninapowashinda ni mimi naelezea jinsi mtu anavyofanikiwa kwa kufanya kazi.

Siwezi kuelezea kilimo sina experience nayo

Njia rahisi ya wewe kuprove wrong nachoongea ni kunipa sababu shida mnaishia kusema nyuma ya pazia.
Hivi nikulize, Mfano mtu ambaye alikua masikini kabisa wa kutupwa na ni mtu ambaye unamfahamu kabisa let's say jirani maana jirani ni rahisi kufahamu life lake kwa sabab ya ule ukaribu mlionao, Sasa huyo mtu unajua kazi zake jinsi zilivyo anazo piga,,,,
Ghafura unashangaa huyo mtu anafanikiwa ananua magari anajenga majumba ya kifahari kazi anayo fanya haiendani na anacho ki project,, je hapo unaweza amini Kuwa uchawi au ni kazi??
Secondly unamini Uganga wa kenyeji?
Third unamini Kuwa Freemason ipo?
Naomba majibu yako
 
Mimi nafikiri mtu ambaye ana uchu wa kujua jambo huwa analifanyia utafiti Alfu ndo anakuja na Fact wewe unasema uchawi haupo huna reason ya kuthibitisha hilo umebaki Wana sayansi sijui wanasemaje fanya mwenyewe acha kubisha hapa!!! Unawafahamu wanajim waulize au nenda kafanye kuhusu unajimu ujue.
YANI KAMA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO HUELEWI BASI NI KAZI BURE KUBISHANA NA AINA YA MTU KAMA WEWE
🤣🤣🤣Nimekuambiaje ..mi nikisema ninapaa..si utataka nione nikipata. Nikikuambia ni ulimwengu wa roho huwezi elewa. Si utaona chizi. Sasa mi ndo navyowaona nyie machizi. Tafuteni elimu nyie. Mna Simu vitabu vyeti lakini mnaongea kama watu wa vijijini ambao hawajasoma. Mi kwa reason na logic zangu nimepinga hypothesis ya uchawi. Tafiti nilizonazo ni kuwa kila kitu kisemachwo ni uchawi sio uchawi bali ni natural occuring. Wewe unayekataa Hilo...nipe mfano halisi wenye uthibitisho wowote nakusubiria hapa nimekaa
 
Ujinga ni kutaka kutumia logic kwenye mambo yasiyo na Logic
Kitu kisicho na logic ndo ujinga. 🤣Ndo maana unaweza insert chochote ukasema ni uchawi. Leo hii naweza kusema Jana nilienda mwezini nikalala na malaika wa kike. Utabisha. Unajua kabisa it's illogical na hamna ushahidi Ila nakuambia hoo ni mambo ya kiroho ya kichawi. 🤣Huu ndo ujinga wenzetu washakataa wanaendelea
 
Hamna kitu Kama kutokewa na marehemu hivi vitu ni hallucinations tu...mbona watu wenye akili timamu na wenye maisha mazuri hawatokewi na hivi vitu. Elimu tu ndo itakukomboa, hivi vitu ni biology sio kila kitu unachokiona ni Cha ukweli ndo maana unaota ndoto. Ubongo una nguvu kubwa na unaweza kukudanganya vingi, kadri jamii inavyozidi kuwa maskini ndo jinsi inavyozidi kuwa ya kishirikina kutokana na ukosefu wa elimu
ukikua utaacha
 
🤣🤣🤣Nimekuambiaje ..mi nikisema ninapaa..si utataka nione nikipata. Nikikuambia ni ulimwengu wa roho huwezi elewa. Si utaona chizi. Sasa mi ndo navyowaona nyie machizi. Tafuteni elimu nyie. Mna Simu vitabu vyeti lakini mnaongea kama watu wa vijijini ambao hawajasoma. Mi kwa reason na logic zangu nimepinga hypothesis ya uchawi. Tafiti nilizonazo ni kuwa kila kitu kisemachwo ni uchawi sio uchawi bali ni natural occuring. Wewe unayekataa Hilo...nipe mfano halisi wenye uthibitisho wowote nakusubiria hapa nimekaa
sasa vitabu vya dini vinathibitisa upo wewe ni nani hadi upinge.
 
Kwahiyo hata wewe unayesema hakuna uchawi yawezakuwa uchawi upo kweli?

Ok wewe umeweza kuthibitisha mafanikio ya mtu kwa sababu ya kufanya kazi tu? Hebu tuweke uchawi pembeni, kuna watu tunawaona wanafanya kazi na wana maendeleo ila unawezakukuta nyuma ya pazia kuna ujambazi au rushwa na ukwepaji kulipa kodi. Je nikisema huyu mtu mafanikio yake ni huko kukwepa kulipa kodi nitakuwa nakosea?
Si kafanya kitu lakini... ujambazi na rushwa is something ni action. Hata angecheza biko it's still something. Afu we nishaona una shift the goalpost na kumuonea mwenzako. Ye kasema hamna uchawi. Sawa bas sio lazima mtu afinikiwe kihalali lakini hamna uchawi, bado yupo sahihi kwenye main premise yake..we unaignore unakimbilia kumponda kwenye mada yake ndogo
 
Kuna siku nilikuwa natoka kwenye mihangaiko yangu. Sasa kufika maeneo ya njia panda ya Mwenge nikawa navuka barabara. Wakati navuka, kuna jamaa naye akawa anavuka in opposite direction (tukawa tunaangaliana).

Sasa tukawa kama tunataka kupamiana. Maana nikienda kushoto, jamaa nae anaenda kushoto. Nikienda kulia, jamaa nae anaenda kulia, hadi tukawa tumekaribiana kabisa. Nikaganda kidogo ili kumruhusu yeye afanye uhamuzi, then tupishane, jamaa nae akawa kama vile ananisikilizia Mimi ndo nifanye uhamuzi. Haya yote yalitokea kwa haraka sana, ndani ya muda mfupi, na muda huo kuna cruiser ipo speed inatokea uelekeo wa Kawe inakuja uelekeo wetu Mimi na yule jamaa maana tupo katikati ya barabara, na muda huo zimeruhusiwa gari zinazotoka upande wa Kawe kwenda makumbusho na zinazokata Kona kwenda mawasiliano, za kutokea Makumbusho zimepigwa pini.

Baada ya kuona yule jamaa nae kasimama hanipishi, nikaamua kupita kushoto kwake, ili yeye apite kulia, cha ajabu na yeye akaja upande ule ule, tukawa tumekaribiana kabisa. Baada ya kuhisi hapa tutagongwa na Ile cruiser kwa uzembe, nilijikusanya nguvu zangu zote, nikaamua kumpiga push yule jamaa ili wote tuangukie upande wake, maana sikuwa tena na namna.

Ajabu ni kwamba nilivyojipeleka kumpush, nilijikuta napush hewa, alaf nikaangukia upande wa pili, yule jamaa hakuwepo aisee. Kile kitendo cha kuanguka, Ile cruiser ilipita speed, ikanikosa kidogo sana na haikusimama Wala kupunguza mwendo. Watu waliokuwa maeneo Yale walijua nijirusha kukwepa Ile cruiser, kumbe Mimi nilikuwa nataka kumpush mtu, na wao hawakuona mtu yoyote.
Chai
 
Hivi nikulize, Mfano mtu ambaye alikua masikini kabisa wa kutupwa na ni mtu ambaye unamfahamu kabisa let's say jirani maana jirani ni rahisi kufahamu life lake kwa sabab ya ule ukaribu mlionao, Sasa huyo mtu unajua kazi zake jinsi zilivyo anazo piga,,,,
Ghafura unashangaa huyo mtu anafanikiwa ananua magari anajenga majumba ya kifahari kazi anayo fanya haiendani na anacho ki project,, je hapo unaweza amini Kuwa uchawi au ni kazi??
Secondly unamini Uganga wa kenyeji?
Third unamini Kuwa Freemason ipo?
Naomba majibu yako
Kwa sababu hujaniuliza Mimi nitakuomba ruhusa nikujibu? If unataka
 
Kuna imani na hadithi mbalimbali katika jamii ambazo zinahusiana na uchawi, majini, na mapepo. Watu wengine wanasema kuwa wameona au kushuhudia vitu hivi, kama vile kukutana na marehemu, kubadilishiwa sehemu ya kulala, au matukio mengine ya kushangaza. Hata hivyo, ni muhimu kutambua kwamba masuala haya yanahusisha imani za kiroho na utamaduni, na kila mtu anaweza kuwa na maoni tofauti.

Katika kujibu swali lako, ni muhimu kutofautisha kati ya imani za kiroho na sayansi. Elimu ya biolojia inaweza kutoa ufafanuzi wa kisayansi juu ya mambo mengi yanayotokea katika maisha yetu. Kwa mfano, watu wanapokumbana na uzoefu wa kuona au kusikia vitu ambavyo havipo kimwili, inawezekana kuwa hii ni matokeo ya shughuli za ubongo ambazo zinaweza kuathiriwa na sababu mbalimbali kama vile matumizi ya dawa au magonjwa ya akili.

Hali duni ya maisha pia inaweza kuathiri jinsi watu wanavyoelewa mambo yanayotokea katika maisha yao. Umaskini, ukosefu wa elimu, na mazingira magumu yanaweza kuchochea imani za ushirikina au kuamini katika vitu ambavyo havina msingi wa kisayansi. Watu wanaweza kutafuta maelezo ya kiroho au ya kichawi kwa matukio ambayo hawawezi kuyaelewa kikamilifu kutokana na mazingira yao.

Hata hivyo, ni muhimu pia kuzingatia kwamba imani za kiroho na utamaduni zina umuhimu mkubwa katika maisha ya watu. Kwa baadhi ya watu, uzoefu wa kuona au kushuhudia vitu vya kiroho ni sehemu ya imani yao na ina umuhimu wa kipekee kwao. Hii inaweza kuwa njia ya kuunganisha na ulimwengu wa kiroho au kuwasaidia kupata maana katika maisha yao.

Ni vigumu sana kutoa jibu la moja kwa moja juu ya iwapo vitu kama uchawi, majini, na mapepo vipo au la. Sayansi haiwezi kukabiliana na mambo yote yanayohusiana na imani za kiroho, na imani za kiroho zinategemea mambo ambayo hayawezi kupimwa au kuonekana kimwili. Kila mtu ana uhuru wa kuamini au kutokubaliana na mambo haya, na ni muhimu kulinda uhuru huo wa kidini na maoni tofauti.

Kwa hiyo, jibu la swali lako linaweza kuwa kwamba imani za uchawi, majini, na mapepo zinaweza kuwa sehemu ya utamaduni na imani za kiroho za watu, na zinaweza kuathiriwa na elimu ya biolojia na hali duni ya maisha. Hata hivyo, ni muhimu kuheshimu maoni na imani za wengine na kutambua kwamba sayansi haiwezi kutoa majibu kamili kwa masuala yote ya kiroho.
kwa hio wewe ni roboti hapa unakubali ila huko nyuma ulishupaza tuu shingo. Wewe unaleta sayansi ya kusomea darasana na maformular yako kwenye maisha halisi sio.
 
Uchawi upo ndugu zangu.

Kuna rafiki yangu mmoja alikuwa anagombea kiwanja cha babu yake yeye na mjomba wake, dogo babu yake alimkatia eneo kubwa tu na akafanikiwa kujenga.

mjomba wake akajiapiza wewe dogo si babu yako anakupenda sana sasa utaona.

Hivi sasa dogo ni kichaa dah, yaani inasikitisha watu wameangaika sana kumtibu lakini wapi ukumuona utamuonea huruma.
Hakuna uchawi it’s science
 
sasa vitabu vya dini vinathibitisa upo wewe ni nani hadi upinge.
🤣Soma posts zangu za kabla kuhusu vitu vingi vitabu vya dini vimekosea. Kifupi
1. Dunia flat
2. Jua kuzunguka dunia, kuweza kusimama na kurudi nyuma
3. Popo ni ndege
4. Sungura kucheua
5. Nyoka na punda kuongea
6. Chuma kugeuka kuwa nyoka
7. Watu kufufuka
8. Mlima wa kuona dunia nzima(coz ni flat na dunia ni ndogo)
9. Magonjwa kusababishwa na mapepo(sio bacteria)
10. Kujipaka damu ya ndege ndo tiba ya magonjwa ya ngozi
11. Dunia kua na ceiling board yenye maji ya mvua juu yanayomwagwa kwa kufunguliwa madirisha ya mbinguni
12. Dunia kuisha wakati wanafunzi wa YESU wakiwa hai
Etc...
Kama hivi vyote ni uwongo na vimeandikwa kwenye Biblia automatically uchawi nao ni uwongo mwingine tu
 
Mimi nafikiri mtu ambaye ana uchu wa kujua jambo huwa analifanyia utafiti Alfu ndo anakuja na Fact wewe unasema uchawi haupo huna reason ya kuthibitisha hilo umebaki Wana sayansi sijui wanasemaje fanya mwenyewe acha kubisha hapa!!! Unawafahamu wanajim waulize au nenda kafanye kuhusu unajimu ujue.
YANI KAMA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO HUELEWI BASI NI KAZI BURE KUBISHANA NA AINA YA MTU KAMA WEWE
Sure, yaani anatumia evidence za wazungu ku- argue shirki za kiafrika, elimu ya mkoloni imem- brain wash, pole yake
 
Shiriki hulainisha mambo yaende.
Mfano kwenye industry ya magari ya usafirishaji daladala au bajaji,
Mnakuwa mmepnga pale foleni, wote vibali vimekamilika, na wewe una gari mpya kuliko wenzako. Wateja wakija kumtafuta chombo ch kukodi, hawaioni gari mpya wanalipia wakimaliza kulipia ndo wanasema aisee mbona Kuna jingine zuri hapa tumeliacha.
Mnaenda road chombo yako traffic anaiona anaipiga mkono na unapigwa bao na traffic kisa kosa dogo tu. Wakati nyuma yako au mbele yako inaspita gari mbovu zaidi ...

Sio kwa uchawi unapunguza ufanyaji kazi, hapana unabweteka, ni unaingia mzigoni mida sawa au wewe unawazidi kidogo. Ila wakiwa wandewa wanasema gari chafu ikaoshwe inga'ae.

Kingine kwenye uchawi ni rahisi sana kukopeshwa spare part na mfanya shiriki kuliko kutofanya shirik kabisaa. Kwa hiyo hata kama umekwama ukisema jina na wakitazama nyotq wanaelewa huyu mwenzetu atatusaidiq

Bado Kuna michezo ya barabarani, Ili tuoate au kuharibikiwa jina la kampuni una shangaa gari inapata ajali ambazo hazina kichwa wa miguu , gari inasumbua abiria wamejaa level siti ngoma inatoka mbezi tu kufika kibaha compressor za brake zinafeli, clutch inatema, gari inakuwa nzito tuu kama umeweka kitu
nlishakaa na mzee mmoja mwenye mabasi ya kahama to dar haahaa alinipa somo hilo nlishangaa
 
Kuna jamaa alikua anatembea na mam mweny nyumba wake, baadae akamuacha akamchukua bint yake alikua anasom form 2 mwishowe akaacha kwa ajili ya jamaa. Baada ya muda akamuacha ten bint akachukua mw'ke mwingine.
Baada ya muda kupita jamaa mashine ikawa taratibu inadorora, mwishowe
haisimami kbs kbs kbs hata kwa kukojoa tu. Amekula kila dawa, lkn wap.
Akavumilia had likizo, akaliweka wazi kwa familia. Wamezunguka nchi nzima kutafuta tiba, wakafika mtwara kwa bibi mmoja!
Bibi baada ya kufanya yake, cku ya 3 akawajibu hakuna namna! Ni wao tu ndo wanaweza kujua nin cha kufanya, tafuteni namna nzuri ya kuwaendea.
Bibi akatoa ushauri rudi ukamtongoze tena huyo bint had akubali, akishakubali usijifiche, jioneshe kwamba uko nae, utangaze ndoa, na iwe ndoa kweli uoe. Ukioa wao(mama mkwe) ndo watajua wafanyeje!
Huko ndo kupona kwake, ilikua ni 2006 hadi mara ya mwisho tunaonana 2016 alikua bado ni mkewe wa ndoa!
Aisee... Kuna watu wengine hawachezewi
 
Mm nakushauri nenda google andika hiyo ndege iliyopotea usome habari yake then uje hapa,,
Alfu Kingine kama hutaki kuamini unasema ni Fiction,, hivi mtu anakwambia vita ya kwanz ilipigana wewe unaminije Kuwa hiyo vita ilikuwepo na wakat wewe hukuwepo isipokua tu unaisoma na wew unamini why usiseme hiyo ni habari, acha kuonyesha kwa jinsi gan kichwa chako hakifanyi kazi,, tarifa huwa zinarekodiwa kwa ajili ya kizaz na kizazi kama kumbukumb ya vizaz vijavyo basi kama hiyo huamini
Pole sanaa
🤣 Oral tradition isn't a good way of historical information. Unajua mchezo wa telephone. Mi nikikuambia kitu umwambie mwingine amwambie mwingine tayari story nyingine imekuwa. Vita za dunia umezisoma kwenye vitabu, zipo kwenye museums, zipo kwenye archives, zipo kwenye credible sources Kama Wikipedia AI zote na etc. Niambie hio ndege yako ipo kwenye credible news source gani. Kama ni gazeti, TV, Radio, website au media ambao ni reliable kwa taarifa halisi..itaje ni ipi.
 
Nipo wilaya ya Mbarali ambapo shughuli kuu ni kilimo Cha mpunga. Ekari Moja ukiihudumia vzuri kabisa inaweza kukutolea gunia 25-28 za debe Tisa. Ila Kuna miamba inakutolea Hadi 40 ukizingatia kwamba kanuni za ulimaji ni zile zile hakuna mpya Yani unachofanya wewe na Mimi nafanya vilevile au kukuzidi kabisa.
Mara nyingi Hawa jamaa unakuta wanakuwa wa mwisho kutoa mazao Yao shambani, mtatoa woooote yeye anakuwa wa mwisho. Hii kitu sikuwahigi kuielewa but ukiwaza vizuri unaona kabisa kwamba Kuna namna nyuma ya pazia, nayo ni hallucination??

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
Fata watu wa kilimo Bora wakuelimishe acha uvivu na ujinga.
 
Back
Top Bottom