SimbaMpole123
JF-Expert Member
- Apr 23, 2023
- 5,501
- 4,956
This is the effect of superstition SasaTarehe 10/07/2023 asubuhi ya saa moja na dakika kadaa watoto wangu wawili darasa la sita na mwingine la kwanza, walianza kupiga kelele kama kushangaa. Kitendo kilichokera mama yao na mimi pia. Kutoka wananionesha bundi aliye kuwa akidodoka kutokea juu ya bati/ paa ya nyumba yangu. Alipo fika chini alionekana amekufa miguu juu yaani alikufa akiwa chali. Hivyo nikaishia kushangaa tu. Nikawaelekeza watoto wasimwambie mtu yeyote tendo lile. Mwezi mmoja nyuma njiwa poli alikutwa amekufa upenyuni mwa nyumba yangu kubwa amabayo imebakia marumaru na baadhi ya vitu ikamilike. Nilichunguza nikagundua njiwa alijigonga kwenye alminium/ kioo cha dirisha akafa. Sikujali ila niliwaelekeza pia watoto wasiongelee lile tukio.
Sasa huyu bundi baada ya kuonekana amekufa nikarudi ndani kuoga na kujiandaa ili tuelekee kazini na watoto waelekee shule. Sasa mke wangu ana mtoto mwingine wa tatu mwaka mmoja na miezi miwili. Tumemuajiri binti wa jirani anakuja kumchukua na kushinda naye halafu mke wangu anamchukua anapotoka kazini mida ya saa tisa au kumi jioni.
Hivyo alikuja kumchukua mtoto kama ilivyo ada. Kwa kuwa niliwataka watu wasijue mke wangu alipo sikia kengele ina gonga akaniambia yule binti atakuwa ameijia mtoto kwa hiyo nikamtoe yule bundi ili asione ikajulikana kwa kuwa nimeamua iwe siri yetu.
Kweli nilitoka nikamtupe nje ya fensi. Cha kushangaza nilipo msogelea akainuka kama anataka kuruka. Nikachukua fimbo ya ufagio wa ndani nikampiga nayo kwa nguvu mara moja tu akaonekana amekufa. Nikashika bawa lake moja na kumrusha nje ya fensi. Nikaondoka kazini kama kawa.
Kilichofuata mida ya saa nne asubuhi kulitokea kutoelewana na mke wangu kwa kiasi kikubwa na kila nikielezea sababu ya ugonvi huo ndugu wananishangaa kuonesha eti mimi ndiyo mwenye makosa. Ila kiukweli toka hiyo siku sijisikii kumkubali wife hii hali napambana nayo kwa kiasi kikubwa na ninaona speed yangu ya kufanikisha malengo yangu inapungua sana na ninakosa ule umotomoto wa hamasa ya maendeleo kutokana na chuki kwa wife. Hata leo nimeamka na hali ya kutompenda wife, bila sababu ya msingi kwa kukelwa na kosa alilotenda siku hiyo nashindwa kusamehe, japo alikosea sharti langu la kumtaka asiwe anapakizwa na watumishi wenzie wa kiume sipendi na ndicho alifanya. Japo alieleza sababu ya kutenda vile nimekuwa mzito kusamehe.
Sasa wanajamii forum niwaulize sababu ni huyu bundi au ni nini? Hali yangu kwa sasa nimbaya kutokana na sonona takribani mwezi huu wote siko sawa kabisa. Najisikia kukata tamaa.
..wote humu mmeona...sorry kwa kinachotokea na mke wako.. ila it's better wote muongee vizuri muelewane what's wrong kuliko kumsingizia mnyama kuhusu ndoa yako...that doesn't solve the problem