Mimi staki mtu yoyote anifate Mimi. Misimamo yangu hauijui. Kuna tamaduni hazina msaada na zinaendelea kupumbaza watanzania. Jamii nyingi ambazo zinaamini uchawi hazijaendelea..hili we mwenyewe unaona..Kuna mtu kasema hapa uchawi ni chanzo Cha upumbavu na umaskini. We unaweza uamini uchawi upo sawa amini, ila unapohusisha na maisha yako...unakuwa tu mtu wa kutafuta kitu Cha kulaumu badala ya kusolve matatizo yako. Imagine wenzetu kila kitu wangesema ni uchawi, unadhani wangevumbua ndege, rockets, satellite etc. Si wangetumia ungo Kama mnavyosema, au kupotea na kutokea sehemu nyingine. Tuweni tu wa kweli katika Hili bana