Kitu gani umewahi kuona ukaamini uchawi upo?

Kitu gani umewahi kuona ukaamini uchawi upo?

🤣Si lipo ..watu waliyofanya research zaidi wamepata details zake kuhusu ukubwa, joto, etc. Sasa nani amefanya research akaona uchawi
Unaweza kuleta uthibitisho wa uwepo wa jua humu ndani achilia mbali mechanism zake? Embu jaribu kututhibitishia humu ndani.
 
Nimesema ni hallucinations...Sasa Kama we hutaki hio sababu kwa sababu babu yako aliamini uchawi na we uamini, mi Sina msaada na wewe.
Hakuna mwenye kuhitaji msaada kwako.

Kwa sababu una msimamo wa kwamba hakuna uchawi basi umekariri neno hallucination tu na unataka kila kilichoelezwa humu watu waamini ni hallucinations tu kisa tu wewe unapinga uchawi.

Yani wewe upo huko uliko unatoa jibu jepesi tu kwenye kila tukio linaloelezwa kuwa ni hallucinations na ndio umemaliza. Ukiangalia kuna maeneo ambayo ndio hutokea sana matukio kama hayo, tunasikia sana matukio hayo kutoka kwa madereva magari makubwa,walinzi wa mashuleni na kuna maeneo maalum ambayo hujulikana kwa watu kutokewa na visa kama hivyo.
Sasa sijui wewe msomi unaweza ukaeleza kwanini watu hupatwa sana na hallucinations maeneo hayo?
 
Napinga kwa wanaosema "uchawi Ni imani potovu" niambie kama ulishaona electrons zikisafiri kwenye waya wa umeme! Na uchawi ni vitu ambavyo vipo ila havionekani kwa macho. Amini kama unavoamini electrons zinasafiri kwenye waya bila kuonekana. Sio Imani potovu!! Hebu amini uruke chapchap na ungo mpaka sehemu unayotaka.
 
Bac Baki nao kichwani, usinitishe. Maana mtu anakuja Kuniambia hoo Mara tulia upigwe kizito Mara sijui kia uyaone, mtu haji na hoja yoyote. Mara matusi sijui shoga sijui nipo mjini (mtu hata hajui nipo wapi). Ndo maana nasema Kama uchawi upo, ungekuwa open kwa kila mtu. Lakini surprise ni kwamba ni watu wachache wenye qualities fulani(wajinga au maskini au waliokua katika jamii za kishirikina) ndo wanaamini hivyo vitu. Ila mtu wa kawaida hawezi ona uchawi hata iweje, why. Coz haupo
Wewe umetoa hoja gani hadi sasa zaidi ya kurudia kutaja neno hallucination tu? Kwa muda wote huu umeonyesha hauna uelewa na unachokipinga.

Et uchawi uwe open kwa kila mtu kwamba uonekane kama linavyoonekana jua! Hii inaonyesha wazi kwamba unapinga kitu ambacho haukielewi na haujui kwamba sio kila kitu chenye sifa ya kuonekana, halafu ndio unajiweka kwenye kundi la watu waliyoelimika?
 
Mimi staki mtu yoyote anifate Mimi. Misimamo yangu hauijui. Kuna tamaduni hazina msaada na zinaendelea kupumbaza watanzania. Jamii nyingi ambazo zinaamini uchawi hazijaendelea..hili we mwenyewe unaona..Kuna mtu kasema hapa uchawi ni chanzo Cha upumbavu na umaskini. We unaweza uamini uchawi upo sawa amini, ila unapohusisha na maisha yako...unakuwa tu mtu wa kutafuta kitu Cha kulaumu badala ya kusolve matatizo yako. Imagine wenzetu kila kitu wangesema ni uchawi, unadhani wangevumbua ndege, rockets, satellite etc. Si wangetumia ungo Kama mnavyosema, au kupotea na kutokea sehemu nyingine. Tuweni tu wa kweli katika Hili bana
Hiyo kusema jamii zenye kuamini uchawi haziendelei sijui ni masikini ni hoja isiyo na ukweli, ni kwamba hakuna mahusiano ya umasikini na huko kuamini kwao uchawi. Kama wewe unaona kuna mahusiano basi eleza hapa ni kwa namna gani imani ya uchawi inavyosababisha hadi wanakosa maendeleo na kuwa masikini? Ni kwamba hawafanyi kazi wanategemea uchawi? Au ni kwa vp hasa imani ya uchawi inafanya wawe masikini?

Unaweza kunitajia watu wasioamini uchawi wamevumbua nini hapa Tanzania ili nikubaliane nawe kwamba waafrika tupo nyuma kimaendeleo kwa sababu tunaamini uchawi?
 
🤣Si ndo hivyo...yaani mkiyatatua mnasema ni kweli, mkishindwa mnaita waganga matapeli. Hamna mganga tapeli wote wanabahatisha tu...ule ni utapeli Kama wa mwamposa tu. Kujaribu kutengeneza hela kupitia ujinga wa watu
Wanabahatisha vp hebu fafanua? Hizi ndio hoja nataka kuzisikia kutoka kwako.
 
Hakuna mwenye kuhitaji msaada kwako.

Kwa sababu una msimamo wa kwamba hakuna uchawi basi umekariri neno hallucination tu na unataka kila kilichoelezwa humu watu waamini ni hallucinations tu kisa tu wewe unapinga uchawi.

Yani wewe upo huko uliko unatoa jibu jepesi tu kwenye kila tukio linaloelezwa kuwa ni hallucinations na ndio umemaliza. Ukiangalia kuna maeneo ambayo ndio hutokea sana matukio kama hayo, tunasikia sana matukio hayo kutoka kwa madereva magari makubwa,walinzi wa mashuleni na kuna maeneo maalum ambayo hujulikana kwa watu kutokewa na visa kama hivyo.
Sasa sijui wewe msomi unaweza ukaeleza kwanini watu hupatwa sana na hallucinations maeneo hayo?
Ni mental activities na brain conditioning. Mtu aliyekulia katika mazingira ya Washirikina is highly likely na yeye kupata hizi hallucinations kuliko mtu ambae hayupo kwenye hayo mazingira. Ubongo ni kitu amazing Sana, unaweza kiaminisha chochote kikakutengenezea picha ndo Sayansi wanaziita hallucinations, lakini they r in the mind. Ndo maana Hadi Leo hatuna video record ya hivi vitu. Na usisingizie sijui mzuka wa kurecord hauna. Dar watu wanarecord mpaka ajali, Kuna cameras za barabarani mbona haonekani..ndo ujue it's just in the mind. Kitu ambacho kipo akilini kitabaki akilini tu..ni kama ndoto. Unajiona ni ukweli baadae unaamka ni ndoto..it's the brain someni hivi vitu jamani walimu hawafundishi coz nao wamekariri tu
 
Napinga kwa wanaosema "uchawi Ni imani potovu" niambie kama ulishaona electrons zikisafiri kwenye waya wa umeme! Na uchawi ni vitu ambavyo vipo ila havionekani kwa macho. Amini kama unavoamini electrons zinasafiri kwenye waya bila kuonekana. Sio Imani potovu!! Hebu amini uruke chapchap na ungo mpaka sehemu unayotaka.
😴Mkuu... tofautisha kitu ambacho kinaweza kufanyiwa tafiti kutokana na umuhimu na athari zake bila hata kuonekana na kitu ambacho ni Cha akilini tu. Utasema sijui nervous system ni uchawi lakini ukipewa dawa si unapona tatizo la nervous system. It means ni kitu ambacho kinaeleweka na wanasayansi sema ni uvivu wako wewe kujifunza. Same as wind. Upepo hauonekani, Ila tunaweza pima speed yake, joto lake, direction yake kutumia Sayansi. So tunakuwa tunajua upepo upo bila hata kuuona.. tofauti na Imani potofu wewe utaona jini, mwingine ataona pepo, mwingine atamwona bibi yake marehemu, yaani kila mtu anaona kitu ambacho ubongo wake umempa aone it's not something we can all see and measure. Ndo maana nasema it's not real
 
Wewe umetoa hoja gani hadi sasa zaidi ya kurudia kutaja neno hallucination tu? Kwa muda wote huu umeonyesha hauna uelewa na unachokipinga.

Et uchawi uwe open kwa kila mtu kwamba uonekane kama linavyoonekana jua! Hii inaonyesha wazi kwamba unapinga kitu ambacho haukielewi na haujui kwamba sio kila kitu chenye sifa ya kuonekana, halafu ndio unajiweka kwenye kundi la watu waliyoelimika?
Nimetoka hoja nyingi Sana fuatilia posts zangu... hallucinations sio hoja pekee..nimeelezea mazingira uliyokulia, jamii inayokuzunguka etc. Na kuhusu kuonekana Kuna vitu havionekani ndio Kama upepo, earth forces, magnetism etc lakini vinapimika. Uchawi ni product of brain...na ndio maana kila mtu anakuja na Cha kwake...
 
Hiyo kusema jamii zenye kuamini uchawi haziendelei sijui ni masikini ni hoja isiyo na ukweli, ni kwamba hakuna mahusiano ya umasikini na huko kuamini kwao uchawi. Kama wewe unaona kuna mahusiano basi eleza hapa ni kwa namna gani imani ya uchawi inavyosababisha hadi wanakosa maendeleo na kuwa masikini? Ni kwamba hawafanyi kazi wanategemea uchawi? Au ni kwa vp hasa imani ya uchawi inafanya wawe masikini?

Unaweza kunitajia watu wasioamini uchawi wamevumbua nini hapa Tanzania ili nikubaliane nawe kwamba waafrika tupo nyuma kimaendeleo kwa sababu tunaamini uchawi?
Issue sio kuvumbua. Bongo hatujafika hii level lakini we si unaona. Uswahilini huko, sumbawanga, kigoma huko, jamii nyingi zinaamini uchawi. Sijasema kwamba uchawi unasababisha umaskini. Nimesema maskini na kukosa elimu Kuna sababisha uchawi. Na ukiendelea kuamini unakuwa kama demotivating factor kwenye maendeleo kwa sababu unakuwa hujipi kipaumbele wewe katika maendeleo yako Bali unatafuta kitu Cha kulaumu. Siku zote mtu anayelaumu haendelei..
 
Kutokuendelea kwetu wala hakuhusiani na kuamini uchawi, waarabu ni matajiri huko mbona imani za uchawi bado zipo kwao hadi leo?
😂😂😂Hii ni point finyu Sana...only a fraction of waarabu ndo matajiri..na ni cause of mafuta
Before that hizi nchi walikuwa makapuku Kama sisi. Na pia hao maghorofa ma investment mengi ni ya watu wa nje... technology nyingi za huko ni za wazungu. Na pia waarabu nao wamesoma zaidi saa hivi na unakuta wengi tu hawaamini uchawi wamebaki kuamini dini tu coz kutoamini ni swala lingine Tena...so it's wrong kusema jamii za kiarabu zinaamini sijui kurogana uchawi etc unless u prove hiki kitu
 
Wanabahatisha vp hebu fafanua? Hizi ndio hoja nataka kuzisikia kutoka kwako.
😂Kwa Nini wasipatie mda wote. Kwa Nini mganga huyo huyo aliyetatua tatizo la mmoja mwingine akienda anashindwa. Au huyo mwingine hakuwa na Imani...😂ehe tuambie mkuu
 
Naamin uchawi upoo tena upo sana...Naamini mwenyezi Mungu yupo na yeye ni msaada kwa sisi ambao tumeamua kumshtakia haya mazengwe ya kiwanga wangu.

Matatizo haya wewe yasikie kwa watu tuuu wala usiombe yakukute.
HAsa kwa sisi ambao tuna family.Ukiwa huna dependants ni rahis kutoamin kwakua u have less to worry about
 
😁Mi sio NASA, kwanza jua na upepo wapi na wapi.. 😴au tumesoma Sayansi tofauti
Hata kusoma vizuri bado hujui, halafu unataka kuzungumzia vitu vikubwa. Ni wapi nimetaja Upepo?

LETE UTHIBITISHO WA KISAYANSI WA MECHANISM IFANYAYO UWEPO WA JUA, huo Uthibitisho ulete humu ndani kama wewe unavyotaka tukuletee uthibitisho wa Uchawi humu ndani.

Wewe uliwezaje Kuthibitisha madai ya NASA juu ya Jua kuwa kweli? Au umeamua kuwaamini tu kwa sababu ni Wamarekani wamesema? Je, una tofauti gani na watoto wanaoamini uwepo wa zimwi kwa kuambiwa tu kwenye hadithi!

Huna akili!
 
Naamin uchawi upoo tena upo sana...Naamini mwenyezi Mungu yupo na yeye ni msaada kwa sisi ambao tumeamua kumshtakia haya mazengwe ya kiwanga wangu.

Matatizo haya wewe yasikie kwa watu tuuu wala usiombe yakukute.
HAsa kwa sisi ambao tuna family.Ukiwa huna dependants ni rahis kutoamin kwakua u have less to worry about
Mungu na Uchawi hakuna tofauti, ni Nguvu ileile, shida ni nani anapokea matendo yake.
Simba anapomfukuza Swala, anaomba Mungu amsaidie Kumpatia mlo wake wa siku hiyo, huku Swala akimuomba Mungu kumuepusha na huyo mwovu simba.

Nguvu ni Nguvu tu, ila ni Uchawi au ni Nguvu ya Mungu kulingana na angle uliyosimamia. Ni suala la Mihemko/Hulka zako tu.
Nje ya Mihemko hiyo hakuna Tofauti.

Na mtambue, Mihemko hiyo ilianza kabla ya Maandiko ya Vitabu vyenu vya Sayansi, Biblia, na Quran, nk.... Ninyi wengi Leo ni wahanga wa Mihemko ya waandishi wa vitabu vya Imani yenu.

Mungu/Sayansi/Uchawi/Nguvu/Asili, nk ni Kitu Kimoja.
 
Back
Top Bottom