Kitu hiki kimoja unachokosa ndiyo kitakachokuzuia usipate mafanikio makubwa

Kumbuka katika binadamu kuna jambo la kujifunza.
Watu hufikiri kujifunza mpk kwa watu waliofanikiwa km Bill Gates na wengine.
Kuna watu wananjia za kutoboa lkn wameshindwa kutoboa lkn wewe ukazitumia ukatoboa.
Mfano hai
Tanzania ina maziwa, mbunga za wanyama, madini (Tanzanite, Dhahabu, Almasi, makaa ya mawe n.k) na ardhi ya kutosha lkn ni nchi masikini duniani.
Futa mawazo ya kujifunza kwa watu waliofanikiwa tu.
Kingine, acha roho za kiswahili. Umefanikiwa ndiyo lkn haupishani na mtu mchawi.
Jamaa kaandika kitabu, maelezo mazuri kwenye thread lkn wewe uliyefanikiwa umekaa tu hata kuandika kitabu hakuna. Unaweza kufanikiwa lkn bado ukawa na ujinga fulani hivi. Mwenzio kaandika, wewe povu km lote.
ACHA ROHO YA KICHAWI NDUGU. NDIYO MAANA AFRIKA HATUENDELEI KWASABABU YA KUONEANA WIVU. HICHO KITABU JAMAA KAANDIKA ROHO IMEKUUMA SANA?
 
Mtu haujafanya kitu kikubwa halafu unaandika kitabu. Sipendi mimi watu kama nyie. Yani afadhali hata Diamond Platnumz japo na yeye ni feki mara nyingine.. ila ana jina kubwa. Angeandika kitabu yeye ningekinunua.

bahati mbaya diamond hawezi kuandika kitabu maana ukweli halisi anaujua kwamba maisha yana kanuni nyingi sana sio moja kwamba ukiifata hiyo unatoboa.

unawezatoboa na usitoboe vile vile,ukaenda kutoboa ktk njia iliyomzamisha mwingine.

maisha yana kanuni zake yenyewe binafsi,hayaingiliwi kabisa na mipango wala mikakati yetu ya kila siku.ndio maana unawezasoma sana ukapata kazi nzuri sana yenye heshima,halafu tukakuta umefariki chooni ghafla tu.
 
Watanzania wavivu sana wa kusoma vitabu, ndio maana wanamshambulia mwandishi wa hiki kitabu as if kawakosea, jamani mwandishi yupo sahihi ametoa njia mbadala ameonhezea njia nyingine ya kufuata ili ufanikiwe...someni kitabu muuongeze maarifa acheni kumtweza mwamdishi
 
Asante kwa kumujibu mpotoshaji vizurii
 
Umeeleza vyema sana mkuu,
Sina cha kuongeza.
Roho za aina hii ndiyo zinafanya wengi kukwama.
Maana mtu wa aina hii akikutana na asiyejiamini, ni rahisi sana kumkatisha tamaa.
Mtu anaweza kubeza uandishi wa kitabu, lakini mwambie akae chini aandike kitabu cha kurasa 300+ hawezi, hata kama utamlipa.
Wenzetu wanaamini sana kwenye maarifa na yamekuwa na msaada kwao.
Huku kwetu maarifa yanachukuliwa kama kitu kisicho na thamani.
Tunaendelea kubadili hili kidogo kidogo maana wapo wanaoelewa na kunufaika.
 
Mada nzuri sana Makirita Amani

Umeshare vizur knowledge kuhusu kufanikiwa.

Swali langu lipo hapa na ambalo wengi nadhan wanajiuliza.
sio kwako tu, il wanataman kuwauliza kwa Influencers, Mentors na Motivational speakers wengine.

Kwamba ww unajua siri iko hapa kwenye (Ubatizo wa mafanikio una vitu viwili vikubwa; KAFARA NA MASHARTI.)

Pamoja na Sijui how successful you are. ila kama hutojali embu niambie hapa.
umejitoa kwa kias gan kutafuta mafanikio?.
umefanya jambo gan gumu?.
umefanikiwa kwa kias gan?.
Najua ni mjasiriamali, how successful is your business?.

Nina watu wangu wawili wa karibu, baada ya kupata some knowledges kama hizo, wameishia kufungua makanisa na kuhubiri.
na mmoja yuko kwenye marketing business.

Mim nadhan bado connections ya kuwa na mafanikio well being (not spiritial - kama hao wawili niliowatolea mfano) bado haijgundulika haswaa ni nini.

Ingawa naungana na ww kuwa hayo uliosema ni nusu ya njia ya mafanikio.
ila mimi nina consider pia hizo factors zinazowapa mafanikio baadh ya watu na kuwanyima nyingine.

"Success usually comes to those who are too busy to be looking for it."
-- Henry David Thoreau
 
Asante mkuu,
Hapo ndipo wengi hawaelewi.
 
Asante sana mkuu,
Kila kitu kwenye maisha yangu, mpaka kufika hapa nilipo sasa na ukilinganisha na kule nilikotoka, ni hatua na mafanikio makubwa.
Lakini mafanikio makubwa kabisa ninayoweza kujivunia mbele ya yeyote yule ni kuweza kuliishi kusudi la maisha yangu, ambalo ni kuyafanya maisha ya wengine kuwa bora zaidi kupitia kila ninachofanya.
Nimekuwa nafanya hivyo kupitia uandishi, kufundisha, ukocha na kutibu.
Na kutokana na mrejesho ninaopata kutoka kwa wale wanaoguswa na kazi zangu, ni mafanikio makubwa.
Nimejipa sharti moja kubwa la kuandika kila siku mpaka siku ambayo ninakufa.
Na tangu tarehe 01/01/2015 nimeandika kila siku bila kuacha hata siku moja.
Katika mchakato huo nimeweza kuandika vitabu 17.
Na katika muongo huu wa 2020 - 2030 napanga kuandika vitabu 100.
Hivyo karibu sana twende pamoja kwenye hili.
Unaweza kufuatilia kwa karibu kwenye www.amkamtanzania.com na www.kisimachamaarifa.co.tz
Karibu sana mkuu.
 

yaani unatwambia mwandishi ni kama mshumaa,ameamua kuteketea ili wengine wapate kuona njia.

lakini anauza vitabu hatoi bure[emoji3166][emoji3166][emoji3166]

ukiitiwa fulsa.............
NOTE
sina ugomvi na mleta mada
 
Wewe ambaye roho haikuumi na unataka kujifunza mbinu za kufanikiwa kwa ambaye hajafanikiwa kwa nini usipite kimya na kuchukua namba then unanunua kitabu tu bila kupiga kelele
 
Kweli mkuu, ndiyo maana tusipangiane wala kupeana/kuuziana vitabu. Kila mtu ana njia yake. Tambua anayetaka kukuuzia kitabu siyo kwamba ana huruma na wew kutokuwa na mafanikio ila anataka atoboe kupitia wewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…