Yaelekea mtoa mada ni mtoto sana au ukabila unakusumbua sana.
Ngoja nikuelimishe kidogo, miaka Fulani ya nyuma kwenye 70's baba wa taifa mwalimu Julius kambarage nyerere aliwahi kuwashauri wachagga wasigombee ardhi ndogo iliyoko Kilimanjaro Bali waende kutafuta ardhi kwingine maana Tanzania ni kubwa na ardhi ni nyjngi.
Kwenye mchakato huo alitoa ardhi Rukwa, sehemu ambayo kwasasa ni mkoa mpya wa katavi, kuna kijiji ambacho wakazi wake asilimia 90 ni wachagga kutoka mkoa wa Kilimanjaro, eneo hilo liliwahi kuonyeshwa na Tanzania safari channel kuna mto unaitwa mto mapacha!
Pia kuna maeneo ya mkoa wa morogoro ambayo wachagga waliwahi kupewa ardhi sikumbuki ni eneo gani kwajina, kwahiyo utaratibu wa kuomba na kupewa eneo la ardhi sio mgeni wala sio shida,
Jifunze historia mkuu kabla ya kutoa lawama au kulaumu! Ni bora ungeuliza kuliko kujifanya much know kumbe ni tabula rasa!