Pengine umeadithiwa au una ujinga kichwani ambao hautaki kuutoa, hebu kasome tena historia, hilo jimbo la kaskazini, kabila gani lilikuwa linatawala mkoa wa arusha.
Nenda kajifunze tena kuhusu historia ya wameru, ujue kwamba wachagga wapo kwa sehemu zao, wachagga wa rombo, marangu, old moshi, kibosho, uru, machame, masama na siha, kugawanywa kwa mji wa arusha kuliwagawa wachagga wa meru, ambao baadae waliitwa wameru kutokana na mlima meru, lakini kimantinki hakuna kabila la wameru, maana wameru ni moja ya sehemu ya wachagga na wameru na wachagga hasa wa machame wanasikilizana pure. Hata wao wameru wanajua fika kuwa asili yao ni wachagga asilia. Ni sawa na kuugawa mji wa machame kisha uwaite kabila la wamachame ambapo kimantiki ni makosa ya kijiografia. Au wamarangu alafu uwaite kabila la wamarangu. Hivyo ukiongelea mji wa arusha unaongelea wakazi wake wa asili wameru ambao kwaasili ni sehemu ya wachagga. Utaniuliza kuhusu wa arusha, kabila la wa arusha sio kabila ni wamaasai ambao waliacha kuchunga ng'ombe kwa kuhama hama wao wakaanza kulima mazao, kimila wamaasai hawalimi wala kuchimbua ardhi hata mtu akifa walikuwa hawamziki Bali wanamtelekeza ndani ya boma na kuhama, sasa basi baadhi ya wamaasai wenzao walioamua kulima na kuwa na makao ya kudumu walitengwa na kuanzisha kabila lao ambalo waliita waarusha. Lakini kimsingi waarusha sio kabila kiasilia Bali ni wamaasai walioacha kuchunga na kuanza kulima na kujenga permanently, wengi wao hawa walistaarabika sana.wanaishi arusha .asili hasa ya wamaasai ni maeneo ya monduli, ngorongoro na maeneo ya huko, sio arusha mjini. Kwahiyo bado kumegwa mji wa arusha (meru) na kuwa makao makuu ya mkoa wa arusha kulifanyika kwa kulimega kabila la wachagga na sehemu zake hasa meru kisha wale wachagga wameru wakaitwa wameru kutokana na mlima meru, rudi kasome historia acha kupuyanga ovyo!
Sio wameru tu hata wapare (chasu) wa ugweno, au wagweno asili yao ni uchaggani, kiasi kwamba hawa usikilizana sana na wachagga kwalugha hata koo usishangae ukakuta koo za minja, kesi au kimario/kimaro(na koo nyingine nyingi za asili ya wachagga) huko ugweno. Ambapo wachagga waliamia huko na kuanzisha makazi miaka mingi sana. Sasa kwaupeo wako mdogo usiofahamu historia ukarupuka tena kukanusha. Rudi kasome historia.