Kituko cha utotoni ambacho sitakisahau

Mimi nilikua muoga wa sindano za "Kristapen"sijui zinaandikwa hivo, nikaenda na maza kuchomwa hosp. Ile nimeanza kuchomwa imeingia tu hivi nikaona maumivu ni balaa nikafanikiwa kukimbia nje ya chumba huku nalia balaa na sindano imening'inia kwenye Tako, daah nesi na maza wakanikimbiza na kunikamata hapo nje afu watu ni wengi hapo nje kwenye benchi la foleni wakamalizia kunichoma sindano hapo hapo kwenye benchi mbele za watu, daah nilisikia aibu balaa
 
Wakati unaiba ulikuwa unafikiria nn?
Utundu wa kitoto tu nilitaka kujua kwanini ile hirizi inapumua na nikagundua kuwa mle ndani anaweka vinyonga, sijui walikuwa wanakaa muda gani mpaka kufa
Nilichoshindwa kujua mpaka leo ni je alijuaje kama mimi ndio nilichukua hirizi yake
 
Hahaaaa we bana umenichekesha sana, khaaa!
 
Mkuu 0713 ilibaki salama kweli?
 
Hahaaaa kumbe we hupati shida na ule msema wa ukikubali kuolewa kubali na kulala bila pichu, teh
 
Mitaa ya kona ya Nairobi Arusha kulikuwa na wamama wauza Karanga na maandazi barabarani. Basi nikiwa na Binamu yangu tulikuwa na tabia ya kujifanya tunataka kununua karanga. Basi inabidi muuzaji atupe za kuonja. Tukishaonja tuu tunatoka nduki! Hiyo 1 ya nyingine baadae
 
Kweli hiki kilikua kituko chako cha utotoni.
 
kuna sku kulikuwa na harusi kwa mother mmoja hv sa sisi watoto tukapewa kazi ya kupanga viti ukumbini huku tukiaidiwa pilau,tulipomaliza tukaenda zetu kucheza ilipofika mida ya jioni tukajisogeza ili tupate ahadi yetu lkn hatukupata tuliendelea kusubiri mpk ikafka mida ya saa 1 kuelekea saa 2 usiku.
sasa ktk hilo kundi tuliokuwepo kulikuwa na dogo mmoja tulikuwa tunamzidi umri kidogo kwa wenge la kunyimwa pilau tukaanza kumlazimisha asepe skani lkn dogo akawa mbishi akala kipigo/mitama akaanza kulia huku akiwa chini kwa muda wa kama dk5 hv akuna aliemjali si tukaendelea na stor zetu...
ebhanaeee si kikanuka dogo akapandisha mlio kwa sauti ya kuunguruma akaamka kabeba stone 2 kubwa wacha weee tulianza kukontoza dogo nae nyuma yetu wachache wakauma kona wengine tukaendeleza sasa tulipokuwa tunaelekea ilikuwa ni skani kwetu lkn nlpofka me mwenyewe niliunga na wenzangu coz nliona mpk nkafungue mlango jiwe litakuwa limeshanipata hata la kichwa tukaenda kujificha dogo akala kona...
hili tukio sitalisahau...
 
Hahaaaaa no wonder unauza vifuniko vya asali aisee, hizi mambo kumbe unazo tangu utotoni, duuuh kubikiri sistaako!!
 
Nikiwa form two siku moja sijui nini kiliniwasha ila nilijikuta nimewaropokea madem fulani wawili darasani kuwa break munione niwapeleke breakfast kantini ya shule wakaniambia poa. Mi baada ya dakika mbili nikasahau hiyo habari.

Break ya saa nne ilipofika mi nikatoka na mshkaji wangu tunatembea taratibu nikashangaa navutwa shati kwa nyuma!! kugeuka lahaula ni wale madem na hapo sina hata kumi mfukoni mi niliropoka tu.. nahisi nilitoa haja ndogo sikuile maana nilikosa hata cha kusema na hao ndo madem wakali wa class kwetu. Nilimgeukia mshkaji nikamuangalia kwa macho ya 'leo natamani nigeuke barafu niyeyuke'

Mshaji akatoa noti ya Sh.200/- mpyaa sijui aliiba wapi naye maana naye hana kawaida ya kuwa na mkwanja. Akanipitishia kisirisiri nikawapa wale madem wakasepa.

Jamaa alinipa kichambo cha haja ila niliona kawaida sana hata angekesha ananisema. Ni mshkaji wangu tunasaidiana kwenye shida na raha hadi leo na disemba mwaka jana nimechangia hela ya ng'ombe mzima wakati anatoa mahari
 
nakumbuka nlivyokuwa naenda kutembea alafu baadaye giza narudi na majani ya ng'ombe siku moja hiyo nlitumwa kitu dukani badala nirudi nkaingia kwenye kibanda cha kuonyesha video kwanzia saa 1 usiku nilirudi saa 4 usiku na pesa nliyo tumwa nayo nilitumia kulipa movie na kunywea chai nilivyorudi nilipigwa fimbo za kufa pipo. Na kuanzia wakati huo sikurudia tena hadi juzi juzi ukubwani
 
Basi toka siku ile ukawa uko very interested na kupiga watu fix mtaani ili na wewe uogopwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…