Daaah nakumbuka babu yake na mama alikuja home kutibiwa toka bush, baasi kuna siku mimi na yeye tulitengewa chai mtu mbili mimi na yeye, akanywa kikombe chake kamaliza, chupa ipo upande wake lakini akaniambia nimmiminie chai(as utaratibu mdogo kummiminia mkubwa) heee me nikamwambia, babu we unashindwa kumimina mwenyewe chai. Hakusema pale, alisubiri mpk nilipopata msara mwingine wakati mother ananifokea BABU nae akakumbushia vile nilivyomwambia amimine chai mwenyewe, heeeeeee hizo stick zilikuwa za bundle la mwaka......KINGINE kuna bro angu aliniambia nikamuuzie big G au jojo shuleni kwetu, la kwanza hiyoooo baasi mtu akija kununua jojo au big G, nikimtamani na mimi nakulaaaa, muda mwingine nikawa nakula mwenyewe tu, bro alikuwa anakaa mbali kidogo, siku alipokuja katika lile box la 780 nilimkabidhi tsh 60 tuuuu, ha ha ha hakunifanya kitu ila mpaka leo tukikumbushiana huwa tunacheka mpk machozi