Kituko cha utotoni ambacho sitakisahau

Kituko cha utotoni ambacho sitakisahau

Mi nilivyokuwa darasa la nne ripoti iitoka nimefeli kinyama,mwalimu akanipa kwwnye bahasha niipeleke home,mwanaume nikasema ngoja niifungue niicheki,kufungua tu daaaah,kitu nimekuwa wa 67 kati ya wanafunzi 77,nikaona huu ni msala nyumbani,basi nikaifuta ile sita kiustadi sana nikaonekana nimekuwa wa saba,home wakastukia mchezo kwani maksi zilikuwa mbovu halafu eti nimefaulu,weee,nilikula mbata,siwezi kuzisahau kamwe
ha haha mimi nilikuwa wa 13 nikafuta tatu na kuitoboa kabisa kufika home baba anauliza mbona imefutwa futwa nikasema kalamu ya mwalimu ilikuwa imeisha akawa anaitengenezea pale pakatoboka na amesema samahani sana ,,, ha hahaha ndugu yangu niliambulia kibao cha kwenye lips kutoka kwa mother aiseee nilipigwa mpaka nikaumwa
 
Kumbe ndo maana lips zako nyeusi laini eeh
 
Daah, huu uzi umenifanya nicheke hadi naona aibu...kweli stress zote zinaishia hapa kwenye uzi asee! Nimesubscrbe nipate kila kinachojiri,...uwiii! Utoto una vioja duuh!
 
Nakumbuka nilikua na mchezo wa kudandia magali kwa nyuna bila dereva kujua..bas siku moja nilidandia trector nikashindwa kushuka trector lilikua linafata mawe polini mbali kidogo...nlivoona naji yamenizidi ilibidi nijisalimishe tu kwa dereva...dereva akanambie twende wore mpaka anakochukua mawe tutarudi wot,kufika kule alinigonga bakora za kutosha.
Mda wa kurudi trector likaalibika ijabidi tulale ukouko..uku home nako natafutwa sana Aaah keshi yake nilivorudi nlikura njiti za kutosha..
Ha haha ha hii noma
 
ha haha mimi nilikuwa wa 13 nikafuta tatu na kuitoboa kabisa kufika home baba anauliza mbona imefutwa futwa nikasema kalamu ya mwalimu ilikuwa imeisha akawa anaitengenezea pale pakatoboka na amesema samahani sana ,,, ha hahaha ndugu yangu niliambulia kibao cha kwenye lips kutoka kwa mother aiseee nilipigwa mpaka nikaumwa

hahahaaaaaaaaaaaaaaaaa,we nawe ulitoboa vibayaa
 
Nilkua na mtindo wakudokoa vitu kwenye friji soda dada zngu wakiweka au mtu yoyote..siku 1 nimetoka zangu michezoni moja kwa moja kwenye friji nikakuta Coke moja ya kopo baariiid imefunguliwa nikachukua nikagigida yote mwisho akatoka mende mmoja mkubwa
 
Nakumbuka nilikua na mchezo wa kudandia magali kwa nyuna bila dereva kujua..bas siku moja nilidandia trector nikashindwa kushuka trector lilikua linafata mawe polini mbali kidogo...nlivoona naji yamenizidi ilibidi nijisalimishe tu kwa dereva...dereva akanambie twende wore mpaka anakochukua mawe tutarudi wot,kufika kule alinigonga bakora za kutosha.
Mda wa kurudi trector likaalibika ijabidi tulale ukouko..uku home nako natafutwa sana Aaah keshi yake nilivorudi nlikura njiti za kutosha..
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji2]
 
Daaah nakumbuka babu yake na mama alikuja home kutibiwa toka bush, baasi kuna siku mimi na yeye tulitengewa chai mtu mbili mimi na yeye, akanywa kikombe chake kamaliza, chupa ipo upande wake lakini akaniambia nimmiminie chai(as utaratibu mdogo kummiminia mkubwa) heee me nikamwambia, babu we unashindwa kumimina mwenyewe chai. Hakusema pale, alisubiri mpk nilipopata msara mwingine wakati mother ananifokea BABU nae akakumbushia vile nilivyomwambia amimine chai mwenyewe, heeeeeee hizo stick zilikuwa za bundle la mwaka......KINGINE kuna bro angu aliniambia nikamuuzie big G au jojo shuleni kwetu, la kwanza hiyoooo baasi mtu akija kununua jojo au big G, nikimtamani na mimi nakulaaaa, muda mwingine nikawa nakula mwenyewe tu, bro alikuwa anakaa mbali kidogo, siku alipokuja katika lile box la 780 nilimkabidhi tsh 60 tuuuu, ha ha ha hakunifanya kitu ila mpaka leo tukikumbushiana huwa tunacheka mpk machozi
 
ulikula Big G zote hizo! ndo maana umeganda ubongo hadi leo
 
Nakumbuka nikiwa darasa la Tano nilinyakua zawadi baada ya kuwa wa kwanza kati ya wanafunzi 283 wa darasa la tano shuleni kwetu.
Basi kufika home nikapatiwa zawadi ya kupigiwa makofi na kushangiliwa na majirani. Sasa akaja mdogo wangu ambaye alikuwa darasa la pili kachelewa kurudi na ripoti yake mkononi anashangilia ushindi wa kaka yake (mie).

Maza akachukua ripoti ya dogo. kufungua tuu dogo aliambulia kipigo heavy. ni baada ya kuwa wa 71 kati ya 82 wa darasa lao. hiyo ilikuwa double impact. Kicheko/Kilio at once.
 
Mara ya kwanza kabisa kwenda town kwa sistaangu (ila siyo huyu atoto wala Heaven Sent , hawa wa juzi juzi tu wananifuata mimi kwa mbali huko) ndo kukukuta chai ktk maisha yangu, tulizoea kunywa uji tu home kijijini. Basi nikawa nimeipenda sana ile chai ya rangi na ule ushamba wangu wa kijijini. Nakumbuka siku hiyo sista yuko huko uani anafua fua, mi nikaingia zangu ndani taratibu hadi kabatini nikatoa chupa ya chai tulikuwa wenyewe tunaita semosi. Nia yangu niibe chai angalau pafu kidogo, basi kufika nikaifungua ile semosi fasta nikafungua mdogo fasta tupia huko chai weeeeeeeeee niliunguaaaaa mbaya mdomoni, nilishuhudia natema vinyama tu kwa jinsi nilivoungua na chai. Sijui kwanini sikuwaza kuwa ni ya moto, yaani sina jibu zaidi ya utoto!!
 
Hizi Familia zetu za kitanzania nzuri sana maana unakuta mpo nyumba moja na Baba, Mama, Bibi, Babu, n.k.

Basi siku moja Babu aliniagiza Ugoro (Bwimbwi) (Tumbaku) na mie huyoo nikawahi kumletea kwa mmasai flani hapa Chuga.

Basi baba hakuwa anapenda tabia ya babu kula ugoro. So wakati narudi nilipitia mlango wa nyuma unaotokea jikoni kisha sebleni ili kumkwepa maana alikuwa barazani. Nilipofika jikoni nilihisi hatua za mtu basi nikauficha ugoro nyuma ya kikopo cha sukari.

Basi baada ya muda nikiwa nimejisahau, mara naskia mtu anatapika si kutapika, chafya si chafya.... huku akiiita "Mama K hii kawaha ya leo umeitoa wapi?"

Alikuwa baba baada ya kujisevia "kahawa"
 
Nilipokuwa mtoto nilikuwa napenda sana wali maharage na hata iweje ni lazima mimi nipikiwe Chakula hicho.Siku moja hali ikawa ndivyo sivyo nyumbani na bi Mkubwa akaniambia bwana mzee leo hakuna wali utakula ugali tuu jioni. Nikajifanya mimi bingwa wa hasira si nikanyea unga uliokuwa umehifadhiwa kwenye kindoo.Kilichonipata ni Mungu tu anajua.
 
sitasahau nilipokua mtoto nilitumwa sokoni nkakutana na wacheza kamali wa funika funua wakanipa hela njaribu nkala mwisho nkajikuta nataman nkachezea hela ya maza wangu ikaliwa kimbembe ikawa kurudi home maana ningepigwa kishenz ila namshukuru mungu akinpa akili ambayo had leo nashndwa kuamin kama mm ndo nilitumia ule ujanja kwan nilienda mtoni nkajipaka matope mwili mzima afu nkarud nyumban nalia nkamwambia maza kuna watu wamenkamata wamechukua hela wamenpiga mambo yakaisha kiroho safo
 
Sidhani Kama mamayo ana imani na usalama wa mtandao wako.
 
Back
Top Bottom