Kituko gani alikufanyia mtoto wa mwenyeji wako ulipokuwa ugenini huwezi kukisahau hadi leo hii?

Ile nimefika kwa shangazi mtoto wake ananiuliza, " hicho chakula chote ulichopakua utakimaliza kweli"? Niliishiwa hamu ya kula maana ilibidi kila mmoja aniangalie mimi! Sema dogo alipewa kichapo ambacho hatakuja kurudia ule ujinga.
 
Kwa ex wangu mmoja alikuaga single mother.

Naingia ndani dogo hataki niingie anasema toka we sio baba yangu.

Nilipokaaa dogo anaimba usikalie viti vya baba yangu .

Msosi ulipoletwa dogo anangania hatuli nawewe we sio baba yangu .

Hapo vituko kibao mara misonyo mara anitishie na hiki mara kile

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Na we ulienda kutafyta Nini uliyataka [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Kusikia watoto wa wenyeji wangu wanazizungumzia vibaya na kuzichukulia poa zawadi nilizowaletea kutoka mkoani daah! Hii ilinipa sana hamasa ya kupiga kitabu hatimaye kuweza kujitegemea. Pamoja wakuu
 
[emoji23][emoji23][emoji108]mmeumbiwa mateso
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] alikukomesha haswaaa.
 
Nadhani ulitaka kusema makande....
 
Nilimtembelea rafiki yangu, kuna katoto ka kike like 5yrs , nilivofika nikaweka pochi yangu chumbani anakolala tupo sebuleni, kameingia chumbani kametoa kila kitu kwenye pochi, hela zote(coins nje), na vitu vya kike njee, eti aunt nakupangia vitu kwenye pochi yako, aisee nikajisemea mazoea gani haya na kama ndiyo mnavyopangiana vitu na mama ako huko huko, nikampa kifinyo kizuri tu huku nakaambia usirudie.
Enzi zetu hugusi vitu vya mgeni maana utachezea mabao kwa bi mkubwa hadi ukome.
 
Wewe ni mpumbavu. Pengine hata huelewi radio ni nini. Watu wanamiliki magari ya kifahari na ndani yana radio. Nyumbani kuna Home theater, Subwoofer na hizo zote ni aina ya radio za kisasa.

Acha dhihaka hata kwa anayemiliki radio ndio raha yake.
Ongezea na radio cassete na simu ya kukoroga iendane na akili yako maana ndio raha yako, washamba mnazingua sana
 
Unaonekana una hasira za maamuzi mkuu. Natamani kujua kwanini unajiita Tafuta Hela
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…