Kituko gani alikufanyia mtoto wa mwenyeji wako ulipokuwa ugenini huwezi kukisahau hadi leo hii?

Niliitwq sehem kwenye kazi,
Boss alikua ni mwanamke,
Ana kiji ofisi chake nyumbani kwake,

Kama nilijua sikwenda peke yangu,nilienda na moja ya msaidizi wangu wa kike.

Picha limeanza nakaribishwa na mkuta baba mwenye nyumba haitiki salam yangu,

Dakika kadhaa kanakuja katoto,akasalimi wala nini, "toka kwetu"

Hiyo ndio ilikua kazi ya mwisho kufanya na huyo mama.
 
Duh! Familia ya hovyo sana hiyo.
 
Ukute mtoto karithi tabia ya baba,
 
Kuna katoto ka dada yangu nako kanapenda sana simu, kuna siku kamenisogelea kanaomba simu hapo kanakula mikono michafu nikajidai sijaskia kakamfata mama yake et niombee simu kwa aunt mama yake kweli kaja eti mtoto anaomba simu nikaona isiwe kesi nikawapa. Simu imerudi ina shombo la samaki nilikasirika toka siku ile hagusi kabisa vitu vyangu.
 
Na vinakimbiliaga kwa mama zao sijui kwanini[emoji23]
 
Malezi ya kulea watoto kwapani siwafichi ndugu zangu ndio yanayosababisha kuwe na ongezeko kubwa sana la mashoga siku hizi,hizi tabia za kufumbia macho kila wanachofanya kina Junia ipo siku huko mbeleni tutakuja kujuta..Hii nimewachana jana tu kwenye basi wakati natoka Dodoma kwenda Dar kuna vitoto viwili vilikuwa na wazazi wao basi walikuwa hawatulii kelele wao,mara wapande juu ya siti gari ikiwa mwendo kasi,mara wavute nywele wakubwa halafu wazazi wao wanawaangalia tu nilikaa siti tatu kwa nyuma kutoka kwao si ndio mmoja akajitela bwana kujifanya kuja kwangu ananiuliza maswali kuhusu screen zile zilizopo kwenye siti za Shabiby nikawa namjibu fresh tu huku nikichukua tahadhari maana niligundua ni mtundu,eh!!! si akabonyeza ghafla kitufe kimojawapo cha cha screen nikamsukumia ghafla kuelekea uelekeo wa wazazi wao na mineno juu watu wakaniunga mkono "hawa watoto watundu kweli" hapo ndipo nikaanza kupiga madongo kuhusu malezi ya watoto wazazi wao wakisikia..Sema niligundua hata mzazi wake wa kike pia hana malezi mazuri maana mtu mwenye malezi mazuri hawezi kula hovyohovyo alikuwa na rundo la mivyakula mara miwa,zabibu,mayai,tambi,biscuti,juice,sambusa na vyote alikuwa anakula kwa wakati mmoja
 
Hio kitu ni kweli aiseee ?


Binti kama huyu unamtorosha naenda ishi nae uswazi ataelewa tu natia na mimba kabisa
 
Sawa warda [emoji16]
 
Nimesoma hizi, zinafurahisha lakini pia kuhuzunisha.
Nawashauri hasa vijana wa kiume ambao wamemaliza chuo au kurudisha mpira kwa kipa ni heri waende kwao kabisa au kwenda kwa mshikaji wako mkapambane pamoja kuliko kwenda kuishi kwa ndugu

Nakumbuka kipindi fulani miaka hiyo ya nyuma nilikuwa nimemaliza chuo, na nimepambana ila mambo magumu ikabidi nirudi mkoani huko kanda ya ziwa na kufikia manispaa kwa mama mdogo ambae anamfuatia mamaangu. Kiuchumi walikuwa poa sana na mme wake na walikuwa na mtoto wao mmoja darasa la 5 ambae anasoma hizi international school
Nimekaa pale mara zikaanza mambo za kuhakikisha kanakula, mara kuosha vyombo ingawa mfanyakazi yupo mara siku nyingine mpo wote na wazazi wake katoe taarifa ya Habari kanaweka katuni yaani vurugu tu.
Siku niliyoamua kutoenda kwa watu
Ni ile kamerudi shule kakaenda kucheza na nguo za shule halafu mamaake akanifokea kwanini nmekaacha kacheze na nguo hizo aiseee nilikakamata nikakapiga. Kakalia kanasema "uondoke uende kwenu sisi hatukutaki hapa, huku kanagalagala chini" na mzee wake akatoka huku anafoka anasema nani Kampiga mwanangu akamchukua akaenda nae town kukanunulia zawadi. Aiseee nilikaa siku mbili nikaondoka nikarudi dsm nikafikia kwa mshikaji tukapambana tukapata ajira na sikuwahi kurudi tena mpaka ingawa huwa tunawasiliana tu. Hata nikienda kikazi kanda ya ziwa sijawahi fikia kwa hao ndugu ingawa wamejenga sana. Mtoto wao huyo alifika six akazingua wakamfanyia mchakato akasoma chuo wakampa asimamie sehemu kapigisha hasara mpaka mzee wake ana sukari, starehe kwa sana kazi anazingua
Jamani malefic ndio kila kitu. Unajitahidi, unapambana unatoboa halafu wanao unawalea kimayai huwaonyeshi namna hela inapatikana ili wawe na nidhamu eti hutaki wateseke ona sasa unasema eti amepata mental health wakati ulimjengea entitlement ya kila kitu bila kumfanya atake responsibilities kwa kila maamuzi anayofanya.
Ni hayo tu tusijisahau kwenye malezi kisa uzungu
 
Ana miaka mingapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…