Kituko gani alikufanyia mtoto wa mwenyeji wako ulipokuwa ugenini huwezi kukisahau hadi leo hii?

Mimi kukaa kwa ndugu hapana unakuwa huna uhuru

Bora kwenu hata kama njaa kali
 
Aloooh!! Eti halagi nini? Na hela mnampa!!
Nilitembelea sister nikakuta binti eti hafanyi kazi yoyote nyumbani. Dada wa kazi anaamka yeye anaendelea kulala ataamka muda anaojisikia. Weeeh mbona nilimnyoosha. Hadi naondoka anafanya kila kazi. Huwa akiniona tu anajua hakuna ujinga.
 
Mmenikumbusha enzi za utoto wangu .Chakula nilichokuwa napenda sana ni wali ndondo na lazima ndondo lipikwe daily kwa ajili yangu.Sasa ikafika kipindi no wali no ndondo.Sasa kwa kuwa nilikua sitaki ugali nikaamua kuunyea unga uliokuwa umehifadhiwa safi kabisa kwenye kilindo.Jiweke kwenye nafasi ya mzazi unatoka kwenye mihangaiko yako unakuta mwanao kanyea unga.Simu ni moja tu tukutane benki.
 
Mimi mpaka wife ananipiga mkwara kuwa mtoto wetu ndio wa mwisho hazai tena kwa sababu "sipendi" watoto. Ila sio kwamba sipendi watoto, sipendi upuuzi wa watoto. Tena upuuzi wa makusudi.
Sipendi ujinga kabisa.
 
Mjukuu wa mama mwnye nyumba ana miaka kama 3 hivi. Siku hiyo kametoka huko kalikotoka kakaja kunitukana umbwa wewe… aiseeee nilivua lapa nilikapiga halafu nikakabeba nikakapekeka kwa bibi yake nikamwambia nimempiga mjukuu wako huyo hapo. Tangu siku hiyo akiniona ni shikamoo tuu kapuuzi kale
 
Mimi nilikuwa nimeenda kujitambulisha ukweni(nyumbani kwao demu wangu)
Sasa kama ujuavyo familia za kishua tunavua viatu mlangoni tunaingia na kukaa sitting room ghafla kuna katoto ka miaka kama 7 hivi kakarudi kutoka shule kalipofika mlangoni kakachukua soksi zangu kakazibana na kijiti kakaingia nazo sebureni kanauliza kwa sauti "eti mama hizi soksi za nani chafu zimechanika halafu zinanuka vibaya kama mavi ya fungo"
Sebure nzima walicheka kwa sauti yaani niliaibika sana siku hiyo
 
Mwaka flani wageni walikuja nyumbani mtoto akamuomba mama ake simu acheze game mama yake akamwambi imezima chaji na hapakuwa na umeme toka asubuhi

Mama wa huyo mtoto akanambia mpe Basi simu yako acheze game maana ataanza sumbua hapa..nikamjibu haina ilioko ni ya kutumia akili sana sio game last kitoto ..mama yake akasema kuliko Alie we mpe ashindweπŸ€”

Au mpe a download anajua kutafuta game zake...nikamjibu mwache Alie hii sio PS
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…