Kituko kingine Wizara ya Afya, Waziri abariki uteuzi wa AMO kuwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu

Kituko kingine Wizara ya Afya, Waziri abariki uteuzi wa AMO kuwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu

sijaelewa ili kuwa RMO inabidi uwe na elimu ya form four au six? huyu jamaa amejiendeleza kitaaluma na ndio taaluma inayotakiwa sasa tatizo ni nini hapa?, nahisi tunashabikia mambo tusiyoyajua. basi kama elimu ya form six ndio inayompa mtu u RMO basi wako wengi mitaani tuwape nafasi hiyo. watanzania tukijidhalilisha kwa kiwango hiki hatufiki mbali najua wengi hatujui sifa za watendaji wengi katika mataifa makubwa tunashabikia porojo za kisomo lakini hatujui elimu ni nini.
 
sijaelewa ili kuwa RMO inabidi uwe na elimu ya form four au six? huyu jamaa amejiendeleza kitaaluma na ndio taaluma inayotakiwa sasa tatizo ni nini hapa?, nahisi tunashabikia mambo tusiyoyajua. basi kama elimu ya form six ndio inayompa mtu u RMO basi wako wengi mitaani tuwape nafasi hiyo. watanzania tukijidhalilisha kwa kiwango hiki hatufiki mbali najua wengi hatujui sifa za watendaji wengi katika mataifa makubwa tunashabikia porojo za kisomo lakini hatujui elimu ni nini.

We nawe!
Umeambiwa awe na MD, siyo fom 4, huyo ni AMO, na AMO sio EQUIVALENT ya MD, ni Equavalent qualification ya kusoma MD.

Halafu, wengi mnawaita MD vilaza,
wkt MD ndiyo walimu wa AMO na CO.
Sasa hao wanafunzi wa vilaza, waliokosa direct qualification kusoma MD, na wanapaswa kusoma 6yrs ili wawe MD, mwatarajia wawe bora kuliko walimu wao?
Lazima muwe hamjalewa kwa hakika!
 
Huyu jamaa aliyeleta hii thread ana roho ya wivu na inawezekana ametoka katika ukoo wakimaskini na wachawi ,ukienda kwa ulinganisho huo mbona viongozi waliopo madarakani wanaelimu ya chini kuliko wanao wangoza kwa hiyo ipitiwe orodha yote nchi nzima kufanya hayo mabadliko? Pili hao MDs wanaomaliza chuo kwa sasa mbona ni vilaza wakutupwa,tunaona madudu wanayofanya ya kitaaluma pamoja na ya kiutawala. Kamwombe basi CMO akuteuwe wewe uwe RMO wa huo mkoa mpya. Nikupe mfano kidogo tu pale Bugando Mkurugenzi wa pale ni Specialist wakati walio cnini yake wana Phd.hapo vipi?
mkuu kinachobishaniwa hapa ni ukiukwaji wa taratibu.hivi unategemea mkurugenzi wa hapo bugando anaweza kuwa AMO?kwa lugha nyingine AMO hajakidhi viwango vya kuwa RMO katika eneo au nchi yenye ma DMOs wenye MD-MPH.
niambie kiongozi mmoja anayeongoza tu bila kufuata vigezo vilivyowekwa(Tundu lissu amelipigia kelele jambo hili sioni tofauti yake na hili la mleta thread)
 
Mimi sioni tatizo, kama amepewa uDMO na akaperform mpaka akaonwa anafaa tatizo liko wapi? nadhani tungeuliza na kwenda kuona kuna lolote alilofanya la kumfanya aonwe anafaa?

RMO is just an administrative post of which needs a good administrator like Dr. Vyagusa who will make you MDs and specialists to deliver accordingly.!

With Vyagusa whom I know expect changes in Simiyu in a near future. He is a man of action rather than words, give him time you will admire that been MD or Specialist doesnt work automatically in administration. Mbona wengi hata Wilaya (DMO) na hata kuongoza hospitali zinawashinda na kuhamasisha migomo.

Its high time for people who have proved good perfomers in medical field to be mandated supervisors of others towards perfomance dispite of their accademic qualifications! and to start with lets support Vyagusa to prove this.
 
mimi sioni tatizo, kama amepewa uDMO na akaperform mpaka akaonwa anafaa tatizo liko wapi? nadhani tungeuliza na kwenda kuona kuna lolote alilofanya la kumfanya aonwe anafaa? RMO is just an administrative post of which needs a good administrator like Dr. Vyagusa who will make you MDs and specialists to deliver accordingly.....

Ministry of health will never agree with u!
Basically they have denied this appointment and all the blaming is upon TAMISEMI.

As usual...no collective responsibility!
 
Katika dunia ya sasa hivi, ambako kuna madaktari wasomi wengi, pengine haikuwa busara kumchagua AMO kuwa mganga mkuu wa mkoa. Lakini tukirudi nyuma, kuna AmOs ambao walichanguliwa kwa cheo hicho na kazi yao ilikuwa exemplary. Kwa mfano aliyekuwa Mganga Mkuuu wa mkoa wa Iringa kwa miaka mingi, Mzee (Dr) Mwakalinga, ambaye utendaji wake ulikuwa mzuri kiasi cha watu kutoamini kuwa alikuwa AMO... Give Dr Vyagusa a chance; let him be tested
 
We nawe!
Umeambiwa awe na MD, siyo fom 4, huyo ni AMO, na AMO sio EQUIVALENT ya MD, ni Equavalent qualification ya kusoma MD.

Halafu, wengi mnawaita MD vilaza,
wkt MD ndiyo walimu wa AMO na CO.
Sasa hao wanafunzi wa vilaza, waliokosa direct qualification kusoma MD, na wanapaswa kusoma 6yrs ili wawe MD, mwatarajia wawe bora kuliko walimu wao?
Lazima muwe hamjalewa kwa hakika!
wewe sasa inamaana wewe mwalimu wako wa msingi hujamzidi elimu mbona alikufundisha sioni sababu ya mwalimu kuzidiwa na mwanafunzi hivyo Amo kumzidi MD hilo lipo tunawaona MD makazini huku hamna kitu hata dozi tu hamna kitu mambo ya ajabu kabisa mkuu mtu unajiuliza hii ndio cream ya 1 na 2 ya PCB mwalimu wangu wa histology aliwahi kuniambia wao wanachagua sana 1na2 lakini wakifika Muhimbili hakuna kitu,lengo lenu la kwenda shule ni kuwatibu Watanzania,

Mkuu hembu tupe tofauti ya kiutendaji ya RMO huyo AMO na RMO MD wengine wanaparform tofauti je RMO huyo AMO utendaji wake ni wahovyo au wivu tu unawasumbua.
 
Radii Mambo mengine ni wivu na choko choko ambazo hazina msingi wowote. Hawa AMO ndio wamejaa katika Hospitali nyingi na ndio wanaotoa tiba kwa sehemu kubwa ya Watanzania. Hawa AMO wamekuwa wakishika nafasi za DMOs ambayo haina tofauti na RMOs. Hii si nafasi ya utabibu ni nafasi ya Utawala ambayo hata Nesi, Afisa Afya au hata Katibu wa Afya anaweza akashika. Mkoa wa Tanga ulikuwa chini ya Afisa Afya akishika nafasi ya RMO kwa muda mrefu sana.

MDs acheni arrogance utawala sio lazima uwe MD???? Badilikeni acheni kuyumbisha Wizara plz.

Kwa haraka haraka unaweza ukawa na mantiki! Lakini ukifikiri kwa undani zaidi kuwa RMO ni zaid ya kuwa Administrator, inabidi uwe na technical capabilities, waliochini yako wakikwama then uweze kutoa way forward. Soma vizuri sifa za RMO, not just being MD, kuna ziada, MD is just a base line! Halafu tukishajiwekea utaratibu ni jambo la busara kuufuata!!
 
Katika dunia ya sasa hivi, ambako kuna madaktari wasomi wengi, pengine haikuwa busara kumchagua AMO kuwa mganga mkuu wa mkoa. Lakini tukirudi nyuma, kuna AmOs ambao walichanguliwa kwa cheo hicho na kazi yao ilikuwa exemplary. Kwa mfano aliyekuwa Mganga Mkuuu wa mkoa wa Iringa kwa miaka mingi, Mzee (Dr) Mwakalinga, ambaye utendaji wake ulikuwa mzuri kiasi cha watu kutoamini kuwa alikuwa AMO... Give Dr Vyagusa a chance; let him be tested

Soma thread vizuri, mleta thread hajasema kuwa huyo AMO ni mtendaji mbaya, ishu ni taratibu na kanuni zinasemaje? Ukweli usiopingika kama hakuna mtu mwenye uwezo elimu zaidi ya huyo AMO ni sawa kwani atafanya kazi kwa kujiamini,

lakin kama kama kuna waliomzidi hao Ma AMO wanatendence ya kupoteza confidence na wanakuwa watu wa visa kwa MDs, hivyo utendaji wao hauwi wa haki na endelevu koz wanajua any time kinanuka na option yao ni kuwa wababe, wabadhirifu, wachawi, majungu, hivyo kuhatarisha afya za wananchi na kuvuruga mfumo mzima wa utoaji wa huduma za afya!!
 
pumba tupu degree is equivalent to advanced diploma au we shida yako n nn?

degree gani mkuu? Md siyo bachelor degree au unalinganisha kama ilivyo kwenye uhasibu? Kwa taarifa yako tu hawa watu hawasomi vitu vingi vilivyo kwenye mtaala wa mwaka wa kwanza hadi wa tatu wa md. Ndo maana na wao wanaenda kuanza upya mwaka wa kwanza wakitaka kusajiliwa na medical council of tanganyika.
 
Huu ni wivu tu, kama amefanya utawala kama DMO kwa zaidi ya miaka kumi na akaperfom na wilaya alizopita ni za mfano in health issues na amewazidi MaDMOs ambao ni MDs in everything tatizo liko wapi?

Afterall RMO ni administrative post na uwezo wa utawala anao na MPH anayo kibindini tatizo liko wapi? acheni roho mbaya madaktari, mwaka huu mtasimamiwa na AMO na kazi mtafanya na migomo msahau kama bado mnaipenda kazi.!!!!

Wajanja anzeni kujipendekeza kwa Vyagusa angalau akisafiri awakaimishe mjifunze kusimamia kazi badala ya migomo na maandamano.Wenzetu wanasema action talks louder than words. Lets give him time you will see great changes in Simiyu,:fish:
 
Huu ni wivu tu, kama amefanya utawala kama DMO kwa zaidi ya miaka kumi na akaperfom na wilaya alizopita ni za mfano in health issues na amewazidi MaDMOs ambao ni MDs in everything tatizo liko wapi? Afterall RMO ni administrative post na uwezo wa utawala anao na MPH anayo kibindini tatizo liko wapi? acheni roho mbaya madaktari, mwaka huu mtasimamiwa na AMO na kazi mtafanya na migomo msahau kama bado mnaipenda kazi.!!!! wajanja anzeni kujipendekeza kwa Vyagusa angalau akisafiri awakaimishe mjifunze kusimamia kazi badala ya migomo na maandamano.Wenzetu wanasema action talks louder than words. Lets give him time you will see great changes in Simiyu,:fish:

ulishawahi kusikia simiyu wamegoma?
 
Mara nyingi tumeshuhudia Waziri wa Afya na hata Mganga Mkuu - Wizara ya Afya ni mwenye Master degree wakati mahospitali kibao ya Rufaa yana Madaktari wenye PhD. Mbona hamjaandamana??

DMO & RMO ni admin position zaidi kuliko kazi ya tiba. Na AMO anaweza kufanya kazi hivyo vyema ilimradi awe na sifa zifuatazo: Stadi za Kiuongozi,kuratibu na mawasiliano yenye ufanisi maana hayo ndio atayafanya zaidi.
 
Katika hali inayoendelea kuonesha uozo ulipo katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Waziri wa Afya, Katibu Mkuu na Mganga Mkuu wa Serikali wamehusika katika kumteua Daktari Msaidizi/ Assistant Medical Officer (AMO) kutoka Singida kushika wadhifa wa Mganga Mkuu wa Mkoa (RMO katika Mkoa mpya wa Simiyu. Uteuzi huu umekiuka miongozo inayosema kuwa Mganga Mkuu wa Mkuu natakiwa kuwa Daktari kamili yaani Medical Doctor mwenye shahada ya kwanza ya Udaktari wa Bidanamu na siyo Advance Diploma. Kwa mantiki hiyo Waziri na Timu yake wanachezea Maisha yawana Simuyu kwa kupelekuwa Daktari wa Mkoa ambaye hana sifa hii ni hatari kwa wananchi wa Mkoa wa Simuyu

=================

The Regional Medical Officer The RMO is the equivalent of to the Director, Regional Health Services, who is the team leader and the overall in charge of coordinating the RHMT as a team, linking vertically to the Regional Administrative Secretary and horizontally with other departmental heads within the Regional Secretariat. The RMO is responsible and accountable to the RAS on a day to day basis on administrative and technical issues and is responsible and accountable on professional / technical issues to the Chief Medical Officer of the MOHSW.


Qualification The RMO shall be a graduate in Medical/Dental from a government-recognized university with a postgraduate qualification in Public Health and training in leadership and management. The RMO shall have at least 7 years working experience in district work in a similar position.
Mytake
1. Waziri wa Afya na timu yake wamewazarau wakazi wa mkoa wa Simuyu kwa kuwateulia Mtu ambaye hana sifa kushika nafasi ya Mganga mkuu wa Mkoa

2. Waziri wa afya na Timu yake amewazarau Medical Doctor wote Tanzania wenye sifa ya kushika wadhifa huo na hasa amewadharau Waganga wakuu wa Halmashauri waliopo katika Mkoa wa Simuyu ambao wanasifa za kutosha na kuliko Bosi mteule wa wawaziri na CMO

3 Waziri na timu yake wanamtengenezea mazingira magumu AMO huyo aliyeteuliwa kushika wadhifa wa RMO kwani hataweza kuwasimamia Madaktari ambao wanamdhidi sifa na kisomo na hasa madaktari bingwa katika mkoa huo

4. Jumuia ya Madaktari Tanzania kwasasa inafanya mawasiliano na MoHSW kutengua uteuzi huo na kama wakigoma MDs wote Tanzania wataingia katika Mgogoro na Serikali 5. Huu ni upuuzi mwingine wa wizara ya Afya na OWM TAMISEMI

5. Uteuzi huu unabaraka za JK kama ulivyo uteuzi wa Majaji

6. Waziri aombe radhi kwa MDs wote Tanzania kwa dharau aliyowaonesha


==============================

Tatizo hapa ni kwamba aliyemteua waziri huyo wa Afya ni DHAIFU kwani ile CV ya Waziri wa Afya nayo sijaifahamu uzuri na huyu waziri ni Dr wa Mifugo yaani ngombe,mbuzi,mbwa,mapaka,nguruwe nk so hapa kwa U Dr wa binadamu pamekaaje na kuwa waziri wa watu??Hebu nifahamisheni mie kama kweli iko poa hii.Na andio maana naye kamteua huyu Dr ki UDHAIFU kwa kuwa sote twafahamu ukimpata mtu ki UDHAIFU basai naye atafanya hivyo hivyo i mean all of them ni DHAIFU
 
Reasoning yako iko chini sana kwa mtu mwenye akili timamu hawezi kukubaliana na nafasi nyeti ya Mganga Mkuu wa Mkoa ikashikwa na assistant Medical Officer yaani Mganga Msaidizi; Kama unataka apatiwe nafasi hiyo basi jila la cheo hicho kibadilishe na kuitwa Mganga mkuu Msaidizi wa Mkoa.

Aidha unatakiwa kuelewa Afisa Afya au Katibu wa Afya hawezi kuwa Mganga Mkuu wa Mkoa hata kidogo kwani hawana taaluma yeyote ya udaktari.
Mimi ni msomi ninayefanya kazi nje ya nchi, lakini hii ndiyo namna ya kufikiri ya "wataalamu" wetu. Yaani wanagombania kukaa kwenye madawati na madaraka yasiyo na tija yoyote katika "Profession" zao badala ya ku practice na kufanya tafiti mbali mbali.

Wanagombania "Titles" badala ya kuonyesha umahiri uwanjani, matokeo ni kama tunavyoyaona; ni wataalam wa ku copy and paste yale yaliyofanyiwa utafiti na wenzetu. Wanaona ujiko kuitwa vyeo visivyo vya kusomea na vya kusomea vinavyoashiria madaraka au "ukubwa" kama DMO, RMO, Engineer n.k.

Ni wataalamu wa kupika na kupakua majungu zaidi kuliko kufanya kazi! Wanahitaji ukombozi. Hivi inaingia akilini kweli madaktari kugomea nchi nzima kudai madaraka ya u-RMO, nafasi zisizofika hata mia moja nchi nzima?

Tofauti kabisa na wenzetu, wasomi wanahaha kujitanabahisha na tafiti na vumbuzi kadhaa na hawataki nafasi za kubweteka mezani wakihudhuria vikao kujadili vijiji vingapi havijakamilisha chanjo ya surua!

Binafsi nampongeza sana Daktari huyo kama ni kweli ametokea Darasa la saba hadi kufika alipo, ni kichwa hasa! Ipo kasumba inayoendekezwa ya kutotambua muendelezo wa elimu wa watu ambayo inachochewa na watu wemye, awazo kama ya huyu jamaa aliyeleta mada hii.

Hivi kweli mtu aliyemaliza Darasa la saba, akasoma miaka mitatu masomo ya cheti, kufanya kazi miaka kumi, kisha kwenda tena kusoma miaka mitatu kupata Diploma, na baada ya kufanya kazi tena miaka mitano au zaidi kwenda kusoma tena miaka miwili na kupata Advanced Diploma; bado tunamhesabu Darasa la saba?

Huu ni wivu wa kijinga, ni wazimu na arrogance isiyo na maana yoyote. Mwisho nampongeza waziri kama ni kweli ndiye aliyefanya uamuzi huo.

Wazo la kusema ati huyo Daktari alitembeza rushwa ni majungu, uongo na kiwenda wazimu kwani yeye si wa kwanza kushika nafasi hiyo, wapo walioshika hata nafasi za uwaziri, sembuse u- RMO?

 
yule naye kaunga unga, lakini at least ana masters ya utawala. Huyu wanayemsema kama hana kigezo kingine zaidi ya amo ni ukiukwaji wa sheria na taratibu zilizo wekwa
Mimi si Daktari, lakini sivumilii udhalilishwaji wa ma AMO namna hii. Wapo ma AMO wenye uwezo mara kumi ya hao wanaojiita ma MDs. Na ndiyo wanaowafundisha wanapotoka vyuo vikuu.

Acheni wivu wa kike! Ninavyofahamu nafasi za DMO na RMO zimekaa kisiasa zaidi na si kitaalamu. Kama sheria na taratibu zilizowekwa ni za kuhakikisha ni ma MDs tu ndiyo wanakuwa ma RMO basi sishangai kwa nini huduma zinaendelea kuzorota hadi watu wanapelekwa India kutibiwa mafua, kwa maana "madaktari" wetu wako bize kusaka vyeo vya kuendesha vikao na si kufanya tafiti na mazoezi.
 
Tatizo hapa ni kwamba aliyemteua waziri huyo wa Afya ni DHAIFU kwani ile CV ya Waziri wa Afya nayo sijaifahamu uzuri na huyu waziri ni Dr wa Mifugo yaani ngombe,mbuzi,mbwa,mapaka,nguruwe nk so hapa kwa U Dr wa binadamu pamekaaje na kuwa waziri wa watu??Hebu nifahamisheni mie kama kweli iko poa hii.Na andio maana naye kamteua huyu Dr ki UDHAIFU kwa kuwa sote twafahamu ukimpata mtu ki UDHAIFU basai naye atafanya hivyo hivyo i mean all of them ni DHAIFU
Acha porojo za kipumbavu wewe, waziri haandiki dawa na si lazima awe Daktari. Mbona madaktari wanapoteuliwa kuwa wabunge na wakuu wa mikoa na hata mawaziri katika wizara zisizohusiana na udaktari hamlalamiki? Kumbe kusoma si kumaliza ujinga eeh?
 
Kweli kunaweza kuwa na matatizo katika uteuzi wa huyu jamaa. Lakini vilevile haitakuwa vibaya kumzungumza huyu jamaa. Hivi inachukua miaka mingapi kwa mtu asiyepitia channel za four 4 -> four six -> Medical doctor kuwa daktari?

Hivi miaka yote huyu jamaa aliyosoma hawezi kuwa daktari? Yeye kuishia darasa la saba na kujiendeleza kwa kutumia channel zingine tayari kunamfanya awe second citizen kazini kwake.

N kweli serikali imeshindwa mambo mengi. Lakini rushwa zingine tunazikaribisha kwa sababu mfumo sio fair. Nyie mliopitia four 4, four 6, University jaribuni kufungua milango ambayo itawafanya watanzania wengine kujiendeleza. Digrii zenu zisizibe njia.

Yaani mwanzilishi wa post hana aibu kusema Jamaa alisota kuwa tabibu msaidizi. Kuwa tabibu msaidizi sio kusota ni kufanya kazi.

God bless America.
 
Back
Top Bottom