RMO ni cheo cha uongozi/ utawala sio cheo cha kitaaluma. RMO mara nyingi hatibu anashinda kwenye vikao vya kiutawala vya RAS au mahala pengine hupitisha likizo za watumishi.
Tatizo ni kuwa cadre ya madaktari kila mtu anajiona yeye binafsi ndiyo nshomile kuliko hata mwenzake. Daktari wa madawa ( internal medicine) hujiona bora kuliko wa upasuaji, wa meno bora kuliko wa magonjwa ya watoto mlolongo ni mrefu ili mradi kila mmoja hataki mwenzake aonekane anafaa.
Madaktari husoma udaktari kwa taabu na kwa muda mrefu lakini kama nafasi ya kukwepa kufanya udaktari wangependa sana kuukwepa wakaenda maofisini kupitisha likizo, kazi isiyohusiana kabisa na udaktari. Madaktari Bingwa wanakwepa kufanya kazi daktari Bingwa wanakimbilia kwenye tu NGOs ambako hata 1/8 ya utaalam wao hautumiki.
Ukiangalia kwa makini utaona uongozi halina uhusiano wa moja kwa moja na taluma. Kama ingalikuwa hivyo Profesa Mkandala wa chuo kikuu cha DSM angekuwa Rais, Dr. Lwaitama angelikuwa Waziri Mkuu, Prof. Lipumba angalikuwa waziri wa uchumi. Lakini mambo sio hivyo. Jemadari huchaguliwa vitani, madaktari waache kulalama wafanye kazi wataonekana na watateuliwa tu. Nafasi ya RMO katika mkoa ni moja tu hata wakigombania ni daktari mmoja tu atakayeteuliwa.
Katika mataifa mengine watawala katika sekta za Afya sio madaktari ni watawala, madaktari wako katika hospitali kushughulika na wagonjwa wao. Madaktari wa Tanzania hawapendi kukaa hospitalini wanawakimbia wagonjwa. Ukitaka ushahidi neda wizarani, utakuta madaktari vijana hawajatumikia fani ya udaktari hata mwaka mmoja wapo wizarani kufanya kazi za ukarani huku tuna acute shortage ya madaktari.
Ukifuatilia kwa makini atajiuliza " Hivi mtaala wa fani hii ya udaktari wanafundisha pia kulalamika? Utajiuliza swali hili kwa sababu wanatumia muda mwingi kulalamika kuliko kutibu. Katika hali ya kawaida watu wenye maneno mengi ya kuchunguza hiki au kile hawana kazi za kutosha, kinyume chake hawana muda kuchunguza nani kapata nini au kakosa nini.