we gule
Senior Member
- Jun 30, 2012
- 136
- 18
Katika hali inayoendelea kuonesha uozo ulipo katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Waziri wa Afya, Katibu Mkuu na Mganga Mkuu wa Serikali wamehusika katika kumteua Daktari Msaidizi/ Assistant Medical Officer (AMO) kutoka Singida kushika wadhifa wa Mganga Mkuu wa Mkoa (RMO katika Mkoa mpya wa Simiyu. Uteuzi huu umekiuka miongozo inayosema kuwa Mganga Mkuu wa Mkuu natakiwa kuwa Daktari kamili yaani Medical Doctor mwenye shahada ya kwanza ya Udaktari wa Bidanamu na siyo Advance Diploma. Kwa mantiki hiyo Waziri na Timu yake wanachezea Maisha yawana Simuyu kwa kupelekuwa Daktari wa Mkoa ambaye hana sifa hii ni hatari kwa wananchi wa Mkoa wa Simuyu
=================
The Regional Medical Officer The RMO is the equivalent of to the Director, Regional Health Services, who is the team leader and the overall in charge of coordinating the RHMT as a team, linking vertically to the Regional Administrative Secretary and horizontally with other departmental heads within the Regional Secretariat. The RMO is responsible and accountable to the RAS on a day to day basis on administrative and technical issues and is responsible and accountable on professional / technical issues to the Chief Medical Officer of the MOHSW.
Qualification The RMO shall be a graduate in Medical/Dental from a government-recognized university with a postgraduate qualification in Public Health and training in leadership and management. The RMO shall have at least 7 years working experience in district work in a similar position.
Mytake
1. Waziri wa Afya na timu yake wamewazarau wakazi wa mkoa wa Simuyu kwa kuwateulia Mtu ambaye hana sifa kushika nafasi ya Mganga mkuu wa Mkoa
2. Waziri wa afya na Timu yake amewazarau Medical Doctor wote Tanzania wenye sifa ya kushika wadhifa huo na hasa amewadharau Waganga wakuu wa Halmashauri waliopo katika Mkoa wa Simuyu ambao wanasifa za kutosha na kuliko Bosi mteule wa wawaziri na CMO
3 Waziri na timu yake wanamtengenezea mazingira magumu AMO huyo aliyeteuliwa kushika wadhifa wa RMO kwani hataweza kuwasimamia Madaktari ambao wanamdhidi sifa na kisomo na hasa madaktari bingwa katika mkoa huo
4. Jumuia ya Madaktari Tanzania kwasasa inafanya mawasiliano na MoHSW kutengua uteuzi huo na kama wakigoma MDs wote Tanzania wataingia katika Mgogoro na Serikali 5. Huu ni upuuzi mwingine wa wizara ya Afya na OWM TAMISEMI
5. Uteuzi huu unabaraka za JK kama ulivyo uteuzi wa Majaji
6. Waziri aombe radhi kwa MDs wote Tanzania kwa dharau aliyowaonesha
==============================
Kwa mtazomo wangu wewe ndugu unachuki binafsi na Vyagusa mbona hujataja shahada ya MPH aliyo nayo,na kwa taarifa yako mbona wapo ma MDs ni vilaza wakutupa .Sakata la MOI(kichwa /goti) Kwani pale walikuwepo AMOs au nenda Hopspitali za Rufaa uone madactari bingwa wanavyochemka.Mimi nadhani inabidi wewe ndio uwaombe radhi AMO na CO wote, na ndio maana hata mgomo wenu hakufanikiwa kwasababu ya mawazo yenu ya kitoto na kuwabagua AMO /CO ambao niwatendaji wakubwa kuanzia ngazi ya Mkoa, wilaya hadi vijijini