Kituko kingine Wizara ya Afya, Waziri abariki uteuzi wa AMO kuwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu




Kwa mtazomo wangu wewe ndugu unachuki binafsi na Vyagusa mbona hujataja shahada ya MPH aliyo nayo,na kwa taarifa yako mbona wapo ma MDs ni vilaza wakutupa .Sakata la MOI(kichwa /goti) Kwani pale walikuwepo AMOs au nenda Hopspitali za Rufaa uone madactari bingwa wanavyochemka.Mimi nadhani inabidi wewe ndio uwaombe radhi AMO na CO wote, na ndio maana hata mgomo wenu hakufanikiwa kwasababu ya mawazo yenu ya kitoto na kuwabagua AMO /CO ambao niwatendaji wakubwa kuanzia ngazi ya Mkoa, wilaya hadi vijijini
 
Ingefaa pia madaktari wazuiwe kugombea ubunge na wasipewe kazi za uwaziri, iwe wao na wagonjwa tu. Kumuweka prof Sarungi mawasiliano au jeshi ni zaidi ya kufuga kuku ndani ya gali ni sawa na kuchukua vifaa vilivyo takaswa kwa kazi zingine ilhali una wagonjwa wa upasuaji.
 

Pendekezo zuri sana kama kazi ya kutibu ingekuwa inalipa inavyostahili.
 
Labda cheo kibadilishwe na kuwa RAMO (Regional Assistant Medical Officer) na si RMO.Na MO akifika mkoa huo atajengewa mazingira mabaya mpaka akimbie.
 
nimesikitishwa sana na update aliyotupa mleta thread !wana simiyu tuungane kupinga uhuni huu.
 
Mimi nafikiri hata ma-MD mna matatizo, kwa sababu hayo maeneo mkipelekwa huko hamtaki, acha hao wanaopewa hizo nafasi kwa elimu zao mnazoita za kuunga wapewe...
 
Pendekezo zuri sana kama kazi ya kutibu ingekuwa inalipa inavyostahili.

ndo maana kuna medical oficer na health/hospital secretary. Kuna anayehusika na mambo ya afya zaidi na anayehusika na hizo siasa mnazotaka. Kuna vitu ambavyo mtu wa kawaida hawezi kuvijibia vinginevyo awe analazimisha kama magufuli. Kuna wakati inakubidi utumie na theory za darasani na siyo kutumia managerial skills tu, hao mnaoita wanaweza utawala kwenye sekta za watu hawawezi. Ndo maana wahandisi wa mikoa, wilaya ni lazima wawe wamesoma uhandisi. We utachukuaje mtu kasoma arts na kumuita regional/district medical officer? kwani kuna kupiga domo huko?
 

Acheni upuuzi,msishabikie uzembe,naapa huu ni ukaidi na uhaini mkubwa kama serikali ya Mkwere na Mtoto wa mkulima wamebariki ukenge huu basi na serkali yake ni legelege na ni serikali ya kishikaji kwelikweli,inawezekana kweli hili limefanyika kwani mm nilikuwa huko likizo Bariadi makao makuu ya mkoa mpya wa Simiyu mwezi wa Julai 2012,mimi pia niko katika industry na uongozi wa afya kwa miaka 11 sasa angalia vituo vya afya vya Shinyanga a.ka. mkoa mpya wa Simiyu Health Centres zote kama Zagayu HC, hazina uwezo na wataalamu wa kupima hata bakteria wa TB/Kifua kikuu tangu 1961 hadi 2012 ambapo vipimo hivi vinafanyika ktk hospitakli ya wilaya iitwayo Somanda,!!!! huu ni ushenzi tu,hata madaktari bingwa waliopo na maDMOs wa wilaya hizo na za mikoa hiyo pacha waliopo hawajalitambua hilo? pamoja na wafadhili kupeleka inputs na fedha zao huko ili kuwezesha huduma hizo lakini wataalamu hao hawawajibiki kwa hilo,mbona mikoa mingine tunapima TB/HIV mpaka ngazi ya zahanati na resource ni zilezile?, mimi nasema hivi hata huyo AMO anafaa kuwa RMO katika mkoa wa wataalamu wazembe na wasio wajibika kama Simiyu,kwani kwa wale ma MDs na specialist walioko Shinyanya wameusaidia nini mkoa mpya kwani hata kuwajibika kutoa huduma muhimu ya bira malipo ya TB/HIV wameshindwa then mnalalamika kutaka madaraka makubwa wakati bado hamujatimiza majukumu yenu ya msingi???"
 
Acheni upumbavu mbona hapa Rombo ma CO wakienda kusoma MDs hawarudi tuna huku vijijini? hawan uzalendo au tuiteje ??/??????????
 

Acha wivu wa kimaslahi wewe,hao AMO ni tegemeo nchi hii,tena wanachapa kazi kuliko hao MD,s.isitoshe AMOs wamekuwa wakiwafundisha hao mds kazi,tofauti ni cheti tu,hao AMO kwa kazi ni hatari wewe
 
hivi ulitaka specialists wakapime makohozi?au ulitaka wasimamie upimaji wa makohozi tena kwenye dispensary?kwa hiyo hutu RAMO wenu ataenda kupima makohozi!

Huo uzoefu wako wa miaka 11 ndio upuuzi tunaopinga hapa,huo uzoefu wako haujaleta tija hapo simiyu.

Kama hamkuwaweka hao specialists kwenye ngazi ya RMO ulitegemea nini?
 
Acha wivu wa kimaslahi wewe,hao AMO ni tegemeo nchi hii,tena wanachapa kazi kuliko hao MD,s.isitoshe AMOs wamekuwa wakiwafundisha hao mds kazi,tofauti ni cheti tu,hao AMO kwa kazi ni hatari wewe

Haha..mkuu kwamba issue hapo ni chetu tu!?..ofcourse wanafanya kazi SI HAKUNA hakuna madaktari wakutosha?!
Elewa tofauti ni nini hasa..na utasemaje, wivu wa kimaslahi huku mishahara yao ni tofauti?
 

Sasa ndo mkate kichwa badala ya mguu??????
 
Mwisho utasema Engeneer wa mkoa/wilaya awe fundi Sanifu/fundi mchundo mwenye FTC, wkt wenye shahada na sifa za ziada wapo......

Arifu usichanganye mambo hapa, inawezekana huku kwenye kada ya uhandisi hupafahamu vizuri. Post yangu ya mwanzo kwenye thread hii nimeelezea lakini nitarudia tena kwa faida yako na wengine wa aina yako.

Mtu mwenye Advanced Diploma in Engineering ni Mhandisi sawa na Mtu mwenye Bachelor of Science in Engineering au Mtu mwenye Bachelor of Engineering.

FTC ni kada ya chini kwa Engineer, kwahiyo usijichanganye na kuilinganisha na Advanced Diploma. Kwenye engineering tunao wahandisi wa wilaya na mikoa ambao wana Advanced Diploma na wanafanya kazi bila bugudha kutoka kwa wenzao wenye Bachelor degrees. Huko kwenye afya sijui mnasumbuliwa na nini!?

Kitu ambacho niliwauliza na ambacho bado hamjakiweka sawa ni kwanini kwenye sekta yenu ya Afya ma MDs mnajiona bora kuliko ma AMOs?

H
izi kelele tunazoziona hapa mnajenga hoja kwamba AMO kateuliwa kuwa RMO ni kinyume na utaratibu kwa kuwa hana sifa za kielimu, mnataka kutuambia kwamba Advanced Diploma is nothing katika sekta ya afya!!??
 
Acha wivu wa kimaslahi wewe,hao AMO ni tegemeo nchi hii,tena wanachapa kazi kuliko hao MD,s.isitoshe AMOs wamekuwa wakiwafundisha hao mds kazi,tofauti ni cheti tu,hao AMO kwa kazi ni hatari wewe

Pole sana utakuwa umevurugwa wewe si bure. Nilichokiandika kiko very clear sasa unapokurupuka kuniambia niache wivu wa kimaslahi wakati mimi taaluma yangu si huko kwenye afya sasa hapo ndipo nashindwa kukusoma.

Ndio maana nikakupa pole kwa kuvurugwa kwakuwa baadae ulichokuja kuandika haukupinga hoja yangu bali umeishadidia kwa kuelezea huduma bora tunazopata kutoka kwa ma AMOs.
 
Mkuu Mwita Maranya,..hatusemi sisi "binafsi" bali ni utaratibu na hivyo hilo ndilo nadhani lililojadiliwa sana hapa!Yaani he should have a Bachelor of MD, na MPH, 7yrs experience..Na kama ndivyo equating ya Diploma ni sawa na MD,..inakuwaje AMO mwenye EXPERIENCE bado arudi shule tena ili awe MD, If masomo, na cheti kina usawa??

Ukweli ni kwamba, AMOs na MDs kuna UTOFAUTI(ambao watu wameshachangia kabla) lakini kiutendaji wanategemeana!

Pili inategemea katika sera na utaratibu wenyewe, kwamba katika level gani anakuwepo nani, wangapi, wakitoa huduma kwa watu wangapi na chini ya usimamizi wa nani..Hii huanzia katika Dispensary(Zahanati), Health Centre/Kituo cha Afya, Hospitali(Wilaya, Teule, Mkoa, Rufaa, Taifa).

Binafsi nadhani, kuna udhaifu uliopo katika sekta ya Afya, ikiwa ni utofauti wa wazi kati ya MDs na AMOs.(ingawa si sehemu zote)..mfano(mkuu japo nilisoma Ufundi Civil Engineering sijui katika taaluma yenu huko ukoje)..tulikuwa tunafundishwa(shuleni) "HIVI NDIYO INAPASWA" na si kwanini tunapaswa kufanya hivyo...yaani unaweza
ukakuta watu wanabishana the mason v/s foreman..na hii ndiyo hasa tatizo huku kwenye sekta yetu ya Afya...wengine kufanya kwa mazoea na wengine kuhitaji utaratibu ufuatwe!
 

AMO ni Assistant Medical Docta?!
 

Ninachokiona hapa ni muendelezo wa siasa tu katika taaluma, hali kama hii ilipata kuwepo siku za nyuma kwenye taaluma ya uhandisi, ambapo kulikuwa na ubaguzi wa hali ya juu sana kwa wahandisi wenye advanced diploma lakini baade mambo yalikuja kuwekwa sawa, na baada ya kuanza kutolewa kwa shahada ya uhandisi (Bachelor of Engineering) ya miaka mitatu ndipo mzizi wa fitna umekatwa kabisa. Mara nyingi kinachogombewa ni majina tu lakini kitaalamu unakuta wote wanafanya kazi zile zile.

Kwa mtazamo wangu huu ugomvi wa MDs dhidi ya AMOs ukiachwa uendelee bila kupatiwa ufumbuzi itakuwa ni hatari kwa ustawi na maendeleo ya sekta ya afya nchini, na bahati nzuri watanzania wengi tunapenda misifa na utukufu, na zaidi ya yote tunaamini zaidi katika majina ya vyeti kuliko utendaji kazi kwa uhalisia wake.
 
Mjinga sana wewe mtoa mada, na haina mantiki yoyote ile, hili ndilo tatizo la kusomea vyeti na si ujuzi....watanzania mnatakiwa kubadirika sana na kuondokana na ujinga huu. Hata kama hana vyeti kwani hakuna on job training? by the way yeye kuwa mganga mkuu wa mkoa kwa sehemu kubwa anachokifanya ni administration kuliko kutoa huduma za kitabibu.
Well: Hebu tuambie wale waliofanya operation ya kichwa badala ya mguu na mguu badala ya kichwa wana elimu gani? au nao ni kina Vyagusa? As much as i know, ni mtu mwenye uwezo mdogo sana kufikiri na kutathimini mambo ndiye anaweza kukubaliana na ujinga huu.

By the way i don't believe in this stupid papers called "Certificates" we have so many **** so called educated, wanasheria waliofanya degree zao Havard, Oxford na kwingineko katika taaluma lakini wamelisaidia nini taia zaidi ya upuuzi na ushenzi uliopitilza.....
Acheni ujinga ujinga wabongo msio tumia akili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…