Kituo cha Mabasi cha Magufuli kimegeuka soko kwa sababu ya usimamizi mbaya


Kuna kanjia ukitokea stand ya daladala usipokuwa na miguu mikakamavu unavunja kiuno
 
Sio kila mtu anaweza kula kwa mama ntilie, binafsi nilishindwa nikasafiri na njaa yangu. Migahawa iwepo
 
dah pale magomeni sheli nimekanyaga bahati mbaya viatu chini vinauzwa, yani utaratibu hakuna watu wanaweka vitu sehem yoyote wanayojisikia..
 
Mwenye jina la kituo aliwataka wauze bidhaa popote, ndio wanyonge hao.
 
Kwa kuongezea ni kwamba lengo kuu la kutengeneza hilo kundi la kumuabudu ni angelitumia kuandamana 2025 ili aongezewe muda wa kutawala. Hilo ndo lilikuwa lengo wala sio kwamba alikuwa anawapenda.
 
Waruhusuni basi wapange bidhaa hadi ikulu..ushen.z kabisa huu.

Mji umekuwa kama wa matahira vile..lazima kuwe na taratibu za kufanya biashara..hii kupanga panga kila sehemu ni ujinga mtupu.
Me sijawahi fika huko mkuu ila nina elewa kinacho zungumzwa kwa lugha ya picha sasa kama wataona ni ajira wanaongeza wafanye mpango na Airport pembeni mwa sehemu ya kurukia ndege pana sehemu ya kupanga nyanya pia!
 
😍😍😍🙏
 
Kila nchi kuna kumwaga na sehemu kama hizo! Hata London! Wewe ukiona hapa kufai huko chagua sehemu za posta posta, Agakhan, oysterbay na kwingineko penye watu wachache. Watanzania walio wengi maisha ya miksanyiko ndiyo wanapenda!

Hebu fafanua London mtaa gani uko hivyo? Twende na facts hatutaki porojo
 
Ukishalitoa jini kwenye chupa huwezi kulirudisha.
TZ kila kitu tumegeuza chini juu na ujinga ndio maarifa.
 
Nimegundua wa Tz hatuna utaratibu mzuri wa kutunza miundombinu,kabisa hii stand haijatendewa
haki katika kuboresha mfumo mzuri wa kuwapangia wafanyabiashara wadogo kupata rizki zao.naona viongozi wamekaa
kimya kama haiwahusu ili baadae waje kusema jiwe aliharibu.
 
Tatizo sio usimamizi. Tatizo stand haikustahili kuwepo pale kabisa kabisa kabisa. Tumesababisha usumbufu na hasara isiyo na sababu. Tumshauri rais arudishe stand Ubungo na pale pawe chuo kikuu.
 
Unapotimiza haki yako usiziue haki ya mwingine huwezi fanya biashara service road then watembea kwa miguu wapite wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…