Kituo cha mabasi ya mkoani Mbezi Louis chakamilika, kufunguliwa rasmi 25/02/2021, Ubungo kufungwa rasmi Jumatano

Kituo cha mabasi ya mkoani Mbezi Louis chakamilika, kufunguliwa rasmi 25/02/2021, Ubungo kufungwa rasmi Jumatano

Vipi kuhusu miundombinu ya kusafirisha waenda mikoani wanaoishi Gongo la mboto, Chamazi, mbagala, Buguruni, Kawe, Tegeta, Bunju ili wawaahi mabasi yao saa 11: 00 alfajiri. Ubungo ilikuwa rahisi kwao. Sasa huko Mbezi watakiona cha mtemakuni.
 
Msafiri gani gharama zake zitakuwa kubwa? Hujui kuna wengine wa Kimara, Kiluvya, Mbezi, Goba, Tabata, Malamba Mawili, Madale wamepunguziwa safari. Kila kitu kina faida na hasara....
Ni kweli wakati iko Kisutu na msimbazi mji ulikuwa haujakuwa ila population kubwa ya watu haiko huko ila nakubaliana na wewe na mimi naunga mkono stand kutoka Ubungo watu watazoea tu, sipingi hii move na itafungua fursa kwa wengine.
 
Kuna umuhimu wa wizara ya Tanroad kuhakikisha kuwa mbezi inafikika kwa haraka na wakati.

TANROAD wanapaswa kuhakikisha barabara zote Muhimu mfano; kutokea kisarawe kupitia/kutokea kiluvya inajengwa ili kurahisisha wakazi wa maeneo ya kisarawe wanafika stendi kwa wakati na bara bara zingine.
 
Duu ni wakati wa kuhamia kwenye malori.

Nafungashaga mizigo k.koo nakodisha carry mpaka ubungo nawahi gari za mchana nikichelewa naiwahi Mwenge.

Sasa kuitafuta Mbezi ni mtihani na automatic gari zinazopitia njia ya mwenge hazitakuwepo.
 
Nilikuwa na mgeni wangu nampandisha bus leo asubuhi pale ng'ambo nje ya kituo nikawa na mazungumzo na wale wakatisha tickets nikamuuliza mbona hiko kituo hakifunguliwi akasema kilicheleweshwa kutokana na kutitia kwa ajili ya zile mvua mbili zilizonyesha wiki mbili au tatu nyuma zilizopita.

Hii stand imekimbizwa mno hasa kwenye finishing hawakutulia kabisa na hii ni kwa sababu ya kelele za wanasiasa.
 
Tuwekeeni ramani ya eneo lote la stand na namna ya kupita maana kawaida yenu tunaifahamu mnatusubiri tupotee mtukamate ili mchukue faini.
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Aboubakar Kunenge amesema ifikapo Alhamisi ya February 25 mwaka huu Kituo Kipya Cha Mabasi yaendayo Mikoani na nje ya Nchi cha Mbezi Luis kitaanza rasmi kutoa huduma na Kituo cha Mabasi Ubungo kilichokuwa kikitumika awali hakitotumika tena.

RC Kunenge amesema hatua hiyo imekuja baada ya kukamilika kwa miundombinu yote muhimu ikiwemo majengo, maegesho, barabara na ofisi za kutoa huduma.

Kunenge amesema tayari Serikali imekutana na Wadau wote husika ikiwemo chama Cha Wamiliki wa Mabasi TABOA na wote wamejiridhisha kuwa kituo kimekamilika na kipo Katika hali nzuri ya kutoa huduma hivyo wapo tayari kutoa huduma.

Mkurugenzi wa Jiji la Dar es salaam Sporah Liana amesema ifikapo siku ya Jumanne watafanya kikao na Wafanyabiashara wote watakaokuwa wakitoa huduma ndani ya jengo na siku ya Jumatano watakutana na Wamachinga, Baba lishe na Mama lishe ili kuwekeana mikakati ya biashara.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam Lazaro Mambosasa amesema Jeshi la Polisi limejipanga kuhakikisha abiria wote wanaosafiri au kuingia kituoni hapo hawapati usumbufu wa aina yoyote.
 
Bado mtakusanya zile jero jero kutoka kwa wasindikizaji/wapokeaji na abiria ambao hawana tiketi?
 
Vipi kuhusu miundombinu ya kusafirisha waenda mikoani wanaoishi Gongo la mboto, Chamazi, mbagala, Buguruni, Kawe, Tegeta, Bunju ili wawaahi mabasi yao saa 11: 00 alfajiri. Ubungo ilikuwa rahisi kwao. Sasa huko Mbezi watakiona cha mtemakuni.
Hapo ndo mtihani sasa.
 
Aidha, RC Kunenge amesema tayari Serikali imekutana na wadau wote husika ikiwemo chama Cha Wamiliki wa Mabasi TABOA na wote wamejiridhisha kuwa kituo kimekamilika na kipo katika hali nzuri ya kutoa huduma hivyo wapo tayari kutoa huduma.
Wapiga debe siyo wadau!!!?
 
Hapo ndo mtihani sasa.
Kule Tanga makampuni yameweka mabasi kwenye ofisi zao za mjini, abiria wanareport kwenye ofisi hizo kisha wanapakiwa kwenye bus moja kupelekwa stand kuu
 
Kule Tanga makampuni yameweka mabasi kwenye ofisi zao za mjini, abiria wanareport kwenye ofisi hizo kisha wanapakiwa kwenye bus moja kupelekwa stand kuu
Najiuliza bus za songea zinazopita njia ya kusini had kufika mbezi lol.
 
Kule Tanga makampuni yameweka mabasi kwenye ofisi zao za mjini, abiria wanareport kwenye ofisi hizo kisha wanapakiwa kwenye bus moja kupelekwa stand kuu
Hata hapa kuna mabasi yana ofisi zao manzese mfano Shabiby Dar express, Dar Lux nk...nk
 
Back
Top Bottom