Kituo cha mabasi ya mkoani Mbezi Louis chakamilika, kufunguliwa rasmi 25/02/2021, Ubungo kufungwa rasmi Jumatano

Kituo cha mabasi ya mkoani Mbezi Louis chakamilika, kufunguliwa rasmi 25/02/2021, Ubungo kufungwa rasmi Jumatano

Najiuliza bus za songea zinazopita njia ya kusini had kufika mbezi lol.
Tanroads walitakiwa watengeneze barabara two way kuanzia vikindu kupiti Gongolamboto hadi Mbezi ujenzi wake ungeenda sambamba na staendi kuwaondolea kero wananchi
 
Tumechoka na ahadi hewa.
Rais alitaka iwe November 30,
Wakasogeza mpaka December 20
Wakaingia mitini
Juzi wakasema jumaatatu Feb 22
Leo wamesogeza Tena?
SGR Dar Moro ilikua iwe Nov 2019
Wamezogezaaa mpaka aibu. Just imagine kilomita 200 na technolojia ya leo. Bado tunazunguuka mbuyu.
Turkey is not a European country.
Kimara Kibaha kilomita 19 tu
Wakati wale wazungu walijenga Chz Sgr km 174 ndani ya miaka 2 na chenchi ilibaki.
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Aboubakar Kunenge amesema ifikapo Alhamisi ya February 25 mwaka huu Kituo Kipya Cha Mabasi yaendayo Mikoani na nje ya Nchi cha Mbezi Luis kitaanza rasmi kutoa huduma na Kituo cha Mabasi Ubungo kilichokuwa kikitumika awali hakitotumika tena...
hv huwa mnatumia sim ya aina gan mbona una weka kitu ambacho ni bandiko tayari.?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duu ni wakati wa kuhamia kwenye malori.

Nafungashaga mizigo k.koo nakodisha carry mpaka ubungo nawahi gari za mchana nikichelewa naiwahi Mwenge.

Sasa kuitafuta Mbezi ni mtihani na automatic gari zinazopitia njia ya mwenge hazitakuwepo.
kwa kweli iatabido kwa baadaye serikali iangalie kujenga stendi sehemu kama vile Boko ili kuhudumia magari ya njia ya kaskazini, vilevile kule Mbagala kunatakiwa kuwepo na stendi kwa ajili ya magari ya njia ya kusini.
 
Nilikuwa na mgeni wangu nampandisha bus leo asubuhi pale ng'ambo nje ya kituo nikawa na mazungumzo na wale wakatisha tickets nikamuuliza mbona hiko kituo hakifunguliwi akasema kilicheleweshwa kutokana na kutitia kwa ajili ya zile mvua mbili zilizonyesha wiki mbili au tatu nyuma zilizopita.

Hii stand imekimbizwa mno hasa kwenye finishing hawakutulia kabisa na hii ni kwa sababu ya kelele za wanasiasa.
Acha uongo bhana hakuna panapotitia pale wale wachina wamejenga acha masihara..barabara ilikuwa Bado aijakamilika..
 
Back
Top Bottom