Benz Petrol
JF-Expert Member
- Nov 22, 2012
- 504
- 196
Sasa kama lugumi hakua na uwezo wa kufunga hivyo vifaa alishindaje tenda?? Wasilete story story hapa. Wamepiga dili na huo ndio ukweli.
Hayo ndio mambo iwapo yatazungumzwa kwa ushahidi wa takwimu usiotia shaka.Mkuu utaratibu haikufwata..Haiwezekani tenda itangazwe leo kesho watu wawe wameshasainishana tenda..Huyo jamaa hakuwa na uwezo na ilikua ni dili tu hilo.
Sasa kama lugumi hakua na uwezo wa kufunga hivyo vifaa alishindaje tenda?? Wasilete story story hapa. Wamepiga dili na huo ndio ukweli.
Haya wandishi kanjanja endeleeni kumuuliza. Sababu za kutenguliwa uteuzi wake upo wazi na ulikuwa unajua halafu leo unakuja kuuliza kitu hichohicho. Hongera Kitwanga Jibu mujarabu kwa waandishi mufilisi.Aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani Charles Kitwanga akiongea na waandishi wa habari leo amezungumzia suala la Lugumi leo baada ya kutumbuliwa kwake
Amesema Lugumi aliingia mkataba na kampuni ya marekani ambayo ina uwezo wa kufanya kazi na polisi, kampuni hiyo ikanunua vifaa Dell na na kampuni hiyo ikaiomba Dell vifaa hivyo ivifunge Tanzania, Dell wakamchagua Inforsystems hivyo Infosys haina uhusiano wowote na polisi wala Lugumi bali ilikuwa inafanya kazi kwa niaba ya Dell
Pia akijibu swali la kuhusu kutumbuiwa kwake kama linahusiana na Lugumi Kitwanga alitumia majibu aliyedai kuwa ya Hayati Mwalimu Julius Nyerere kwa waandishi jijini Nairobi Kenya kwa kuhoji ''Hivi mtu akikuuliza mimi ni mume wa mama yako utakubali?'' na kutaka asiulizwe tena swali hilo
Ila alivokuwa anaongea sina uhakika kama ndio ongea yake au alikuwa 'ametupia' tena
Kwa hiyo umeridhika kabisa na maelezo ya Kitwanga.Dili gani tena...of course Kitwanga amejibu vizuri sana, hakuna dili hapo...hayo ni mambo ya biashara, na kama inforsystems walifanya lobbying wao ndio wafunge vifaa hivyo, hizo ndizo mbinu za biashara...sasa kama vilikuwa havijafungwa wa kuulizwa ni LUGUMI na kampuni ya DELL na siyo KITWANGA...tuache longo longo, leo KITWANGA nimemwelewa...Watanzania wengi tumejaa umbea, wivu, majungu na fitina...hawataki mwenzao afanikiwe...Mimi naichukia tabia hii ya sisi watanzania yaani muda wote kulalamika tu na kuleta habari ambazo ziko half cooked...Sasa waandishi wa habari walishindwa vipi kutueleza kama alivyofanya KITWANGA???
Kiasi chake, ila bado yapo maswali yanayohitaji ufafanuzi bahati mbaya hatuna waandishi wa habari wazuri...kwa mfano wangemuuliza hiyo Infosystems ilipewa muda gani kufunga...na mkataba wa kufunga vifaa hivyo ukoje...Lakini waandishi wa habari nao wameandamwa na mihemuko kama ilivyo wananchi...wanatafuta sensational news tu na siyo kufanya analysis ya issues kwani hawana uwezo huo, sitashangaa hata kidogo kama baadhi ya magazeti yatakuja na stori ya 'KITWANGA ajifananisha na Nyerere'...Kwa hiyo umeridhika kabisa na maelezo ya Kitwanga.
Swala la mkataba kusainiwa siku moja baada ya tenda kutangazwa sio ishu kwako?? Kampuni ikiomba tenda ni vigezo gani lazima vifwate ili iweze kupata?? Je Jeshi la polisi lilijirisha kuipa Lugumi tenda siku moja baada ya kutangaza tenda?? Hiyo mikataba ya Lugumi na kampuni ya kimarekani,Dell na Infosys ilikuwepo kwenye mkataba kati ya Lugumi na Jeshi la polisi?? Kama haikuwepo kwa nini izungumziwe na wakati serikali imeingia mkataba na Lugumi?? Kwa nini Lugumi alipwe 99% ya fedha zote na wakati amefanya kazi kwa 10% na alikua hajamaliza vuzuri katika hiyo 10%??Kiasi chake, ila bado yapo maswali yanayohitaji ufafanuzi bahati mbaya hatuna waandishi wa habari wazuri...kwa mfano wangemuuliza hiyo Infosystems ilipewa muda gani kufunga...na mkataba wa kufunga vifaa hivyo ukoje...Lakini waandishi wa habari nao wameandamwa na mihemuko kama ilivyo wananchi...wanatafuta sensational news tu na siyo kufanya analysis ya issues kwani hawana uwezo huo, sitashangaa hata kidogo kama baadhi ya magazeti yatakuja na stori ya 'KITWANGA ajifananisha na Nyerere'...
Kwa hio Chadema ni Jamvi la Wageni ?huyu bora ajiunge na CHADEMA tu..maana ameshachanganyikiwa
Eti "Mtu Akikuuliza Mimi ni Mume wa Mama Yako Utajibuje..."
ahahaha