Kitwanga atoa ufafanuzi wa suala la Lugumi na uhusiano wake kuhusu kutumbuliwa kwake

Kitwanga atoa ufafanuzi wa suala la Lugumi na uhusiano wake kuhusu kutumbuliwa kwake

kujibu maswali ni taaluma pia labda kwa uzoefu mwenzetu Ana taaluma ya kujibu maswali kwa ufasaha??? Tuanzie hapo kwanza.
 
Nadhani kazi yao ilikuwa kuwauzia serikali hivyo vifaa hivyo wao waliamua kwenda kuvinunua ktk Kampuni ya Dell(inawezekana zipo kampuni nyingi zinazotengeza hivyo vifaa)
Mi naona wamekaa kama madalali ina maana serikali imeshindwa kuwapata hao dell! Ila kama ndo utaratibu wa tenda hapo sawa lakini bado mi naona sintofahamu kibao!
 
wanabahat watanzania sisi ni watu poapoa sio wafuatiliaji wa mambo haya.. kadiri wangelikuwa aware nadhani hali ingekuwa sio nzuri.
 
Hilo suala si wameishalimaliza juu kwa juu bungeni? Kitwanga analizungumzia leo ili iweje? Mbona hakuwa na ujasiri huo kabla? Na hawa waandishi anaozungumza nao sijui kawatoa wapi maana ni kama wamenywea mno!
 
CHARLES Kitwanga, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi amesema kuwa, hajutii ‘kutumbuliwa’ na Rais John Magufuli, anaandika Moses Mseti.
Ametoa kauli hiyo wikiendi iliyopita jimboni kwake Misungwi jijini Mwanza ikiwa ni takribani mwezi mmoja baada ya kung’olewa kwenye nafasi hiyo.

Kitwanga alifukuzwa kazi kwa madai ya kuingia bungeni na kujibu masali ya wizara yake akiwa amelewa.
Amesema kuwa, anamshukuru Mungu kwa kuondolewa katika nafasi hiyo na kwamba, huenda kama angeendelea kuwepo, angepata matatizo makubwa zaidi.

Na kwamba, hatua ya Rais Magufuli kumwondoa katika nafasi hiyo kitamsaidia kuwatumikia wananchi wa jimbo lake kwa ukaribu zaidi tofauti na alivyokuwa kwenye nafasi ya uwaziri.

“Namshukuru sana Mungu kuondolewa katika nafasi hii (Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi) labda ameniepusha na mambo mengi ambayo yangeweza kunikumba na hii itanisaidia kuwatumikia wanamisungwi kwa ukaribu,” amesema Kitwanga.

Kitwanga baada ya kung’olewa katika nafasi hiyo, siku kadhaa baadaye alitimkia nchini Israel ambako inadaiwa kwenda kupumzika ambapo alirejea nchini hivi karibuni. Baada ya kurejea nchini, Kitwanga moja kwa moja alikabidhiana Ofisi na Waziri wa Mambo ya Ndani kwa Mwigulu Nchemba aliyeteuliwa kushika nafasi hiyo. Nchemba alikuwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi.

Kabla ya kutimuliwa Kitwanga alikuwa akiandamwa na kashfa ya Kampuni ya Lugumi iliyopewa zabuni ya kufunga mashine za kutambua alama za vidole katika vituo vyote vya Jeshi la Polisi nchini.
Jeshi hilo liliingia mkataba na Kampuni ya Lugumi Enterprises ili kufunga mashine 108 nchi nzima lakini kampuni hiyo ilifunga mashine 14 tu.
Tangu lini nguruwe ajutie kula uchafu? Ukiona mtu anajuta, ujuwe ana akili timamu.
 
CCM ni ile ile, lao moja!
Kwa nini ajute wakati bingo ya lugumi ni nene kuliko kutumikia u-wizi wa mambo ya nyumbani!
Bado hamshituki tu!
 
CCM ni ile ile, lao moja!
Kwa nini ajute wakati bingo ya lugumi ni nene kuliko kutumikia u-wizi wa mambo ya nyumbani!
Bado hamshituki tu!
Kwa wenye akili tayari tushaligundua hilo
 
Back
Top Bottom