MchunguZI
JF-Expert Member
- Jun 14, 2008
- 4,011
- 2,185
Si angalao ungejibidisha kuangamuka na kujua/fahamu namna biashara za technical sales and after sales services zinavyofanyika, halafu baada ya hapo utoe comment yako basi! Maana sasa unakera kwa kuaibisha JF. Sio wote tulioko humu ni wajinga. Maana suala hapa siyo nani alipewa tenda ya kufunga vifaa kambi za polisi, la hasha. Ni iwapo utaratibu wa kisheria (PPA) ulifuatwa na kama mzabuni alitimiza wajibu wake kwa mujibu wa mkataba. Basi! Hizo ndio hoja zenye kuwakilisha maslahi ya umma.
Hapa swala ni Infosys..haina uhusiano na Lugumi...mambo ya Lugumi kushinda tenda haina uhusiano na mada husika...
Jambo liko inter-related. Hakuna PPRA inapotoa mwanya wa kampuni ya kishenzi kusambaza bidhaa kwa serikali, labda iwe ni kugawa mbengu za mahindi kwa jirani yako. Serikali ikitoa tender kwa mtu asiye na uwezo/utaalamu, huo ndo upuuzi. Tenda ya vifaa kama hivyo siyo sawa na kugawa pembejeo.
Kama lugumi hakuwa na uwezo, akanunua kwa kushirikiana na mwenye uwezo, mwenye uwezo akatafuta tena atakayefunga, basi ujue hiyo siyo serikali. Yaani moja kati ya katua hizo ikishindwa basi, kazi haifanyiki. Serikali inaweza kuruhusu risk ya bilioni zote hizo? That will be a nonsense government.
Pesa kama hiyo huwekewa kinga za kibenki kabla hata ya manunuzi. leo hii tunaaambiwa hata hakuna kilichofanyika kuhalalisha matumizi kama hayo. The equation is simple; Lugumi, na wote ktk msululu wa makubaliano hayo hadi huyo infosys, wote walikuwa pamoja ktk mbinu chafu! Mbaya zaidi sasa jamaa hajui hata kujieleza.