Kitwanga: Kuna kundi linalomshauri vibaya Rais Samia

Kitwanga: Kuna kundi linalomshauri vibaya Rais Samia

Rais anaweza kuonekana dhaifu lakini anapoamua kushughulikia watu kwa mamlaka yake huwa tunakuja humu jukwaani na kuanza kulialia tukisema rais huyu ni dikteta,

Hayati JPM aliamua kutokuwa dhaifu na mpaka miaka miwili akiwa kaburini bado wapo watu wanaoulalamikia uongozi wake.

SSH sio dhaifu kama tunavyodai, ameruhusu uongozi wake uheshimu demokrasia na amewapa watu uhuru wa kufanya kazi kwa mujibu wa taratibu.
Well said, wengi mambumbumbu, hawajui hata nini maana ya kuwa na serikali. Serikali lazima itishe wahalifu, wazembe na wanafiki
 
Mkuu shughuli za kilimo Tanzania huzijui kabisa. Kwamba wauze mitandaoni? Hakuna kitu kama hicho.

Sehemu kubwa ya wakulima Tanzania wanalima ili kuishi, kujikimu, ni wachache wenye uwezo wa kulima, kuvuna na kuhifadhi kutafta soko, na hao hawalimi wananunua kwa wakulima.

Kilimo Tanzania ni changamoto kubwa, hadi mazao yanamfikia mlaji yamepita kwenye mikono ya madalali ama watu kati karibu 9.
Mimi nakwambia tubadilike tutoke huko unakosema, twende kilimo smart, halafu wewe unasema kilimo cha Tanzania sikijui?

Katika dunia ya leo ya smartphone, mkulima ana excuse gani ya kutegemea middle man?
 
Back
Top Bottom