Asalaam wadau!
Kauli ya Mh. Rais Jana ni kauli yenye kosa kuubwa saana LA kiufundi ambalo litagharimu saana raia ama taifa.
Yaan kavita ka wiki mbili unatamka kataleta mfumuko wa bei zaidi ya huu. Mama kuwa makini na wanaokushauri.
Unajua kwanini kiufundi umekosea?
Kauli yako yoyote unayoitoa uwe na furaha saana ama hasira saana hio ni amri... Na wahusika wataji activate katika hilo fast hata kama litavunja sheria au kuumiza pasipo ulazima.
Mama Jana umetamka tuu Leo mkeka wa bei mpya Zanzibar umetoka sasa tunasubiri bara, sa na huduma zingine muhimu sijui itakuaje?
Yaan nchi inakuaa kama haina stock yaan pakitokea changamoto kidogo tuu basi reactions hasi hutokea Mara moja ila kurecover huwa tunakua wa mwisho.
Mh. Rais nilitegemea useme kwamba pamoja na vita inayoendelea inaweza kutuathiri lakini serikali yetu imejipanga kuhakikisha haituathiri saana na madhara yake"
tofauti na kauli yako ambayo ni sawa na umefungulia mbwa wabweke na kufanya watakavyo kwakua mfugaji wao umewaruhusu.
Tuonee huruma sisi watanzania wengi maskini, matajiri ni wachache saana.
Nawasilisha.