Kiufundi, Rais Samia umepotoshwa kuhusu mfumuko wa bei kutokana na Vita na ukapotosha

Kiufundi, Rais Samia umepotoshwa kuhusu mfumuko wa bei kutokana na Vita na ukapotosha

Ni sawa ila lengo langu usimamizi uzingatiwe sio ishu pesa imfikie mwananchi Bali ilete Tina kwenye kupunguza umaskini.
Nadhani unafaham pesa hizi hatakurudishwa serikali ni ishu watu wanapita Nazi mbele... Mfano kwenye Katz yangu ni vikundi 6 tuu vilipata na ni kimoja tuu kimerudisha mwaka wa pili sasa haieleweki. Ndo mana tunasema bila usimamizi wa fedha tutajaza maji kwenye net.
Mkuu, hizo pesa zipo mtaani ila si kwenye hivyo vikundi. Kuna watu wanazo wanazizalisha, na ndilo lengo la kwanza la serikali, pesa ziwe kwa wananchi. Ila upo sawa kuhusu kuongeza udhibiti.
 
Asalaam wadau!

Kauli ya Mh. Rais Jana ni kauli yenye kosa kuubwa saana LA kiufundi ambalo litagharimu saana raia ama taifa.

Yaan kavita ka wiki mbili unatamka kataleta mfumuko wa bei zaidi ya huu. Mama kuwa makini na wanaokushauri.

Unajua kwanini kiufundi umekosea?

Kauli yako yoyote unayoitoa uwe na furaha saana ama hasira saana hio ni amri... Na wahusika wataji activate katika hilo fast hata kama litavunja sheria au kuumiza pasipo ulazima.

Mama Jana umetamka tuu Leo mkeka wa bei mpya Zanzibar umetoka sasa tunasubiri bara, sa na huduma zingine muhimu sijui itakuaje?

Yaan nchi inakuaa kama haina stock yaan pakitokea changamoto kidogo tuu basi reactions hasi hutokea Mara moja ila kurecover huwa tunakua wa mwisho.

Mh. Rais nilitegemea useme kwamba pamoja na vita inayoendelea inaweza kutuathiri lakini serikali yetu imejipanga kuhakikisha haituathiri saana na madhara yake"

tofauti na kauli yako ambayo ni sawa na umefungulia mbwa wabweke na kufanya watakavyo kwakua mfugaji wao umewaruhusu.

Tuonee huruma sisi watanzania wengi maskini, matajiri ni wachache saana.

Nawasilisha.
Gesi ya Ntwara vipi?! Hata kama imeuzwa ingekuwa mbadala haswa…
 
Hii kauli ya kusema anapotoshwa kwakweli inachosha sana kwani Rais yeye hana uwezo wa kufikiri au kuona? Hivi Rais hajui kuwa bei ya nondo,bati na mafuta ikoje toka mwaka jana?

Hivi Rais hajui kauli zake zina madhara gani? Yani Rais anasema wazi bidhaa zote zitapanda bei na maisha yatakuwa magumu halafu unasema amepotoshwa na mtu? Yeye hajui kufikiri?
Tunatofautia kwenye kufikiri ndo mana anakua na washauri binafsi na baraza LA mawaziri... Kwakawaida lazima tuanze kuwatupia lawama hawa aliowaamini kwasababu wanaweza wakawa na ajenda binafsi zidi yake
 
Uongo mbaya, Rais Samia hatoshi, ni vyema kwa kulinda heahima yake 2025 asigombee
Mmmmmmm! Kwa jinsi anavyoonekana, yupo tayari kwa lolote, ili tu, arudi tena hiyo 2025. Alishasema, kwa sasa yupo hapo kwa nguvu ya KATIBA tu, ila anataka Mwanamke aje kuwa Rais kwa KURA!
 
Hakuna mahali popote alipopotoshwa

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
Ni ameamua mwenyewe??
Kaka sijui unaishi Dunia gani??? "kavita ya wiki mbili"??
Kavita yako imetosha kupandisha bei ya mafuta ya magari huko Ulaya kutoka Euro 1.60 wiki mbili zilizopita kufikia Euro 2.05 leo, itaendelea kupanda. Dizeli iumeshkuwa ghali kuliko petroli mara ya kwanza katika historia kule.
Sasa uanamini badiliko hili la bei kwenye soko la Dunia halitaathiri nchi kama Tanzania??? Bei ya mafuta haitapamda hapa????
BAsi endelea kuota ndoto!

(pamoja na hayo: Ukraine ni kati ya nchi zinazopeleka nafaka nyingi kama ngano kwenye soko la Dunia. Sasa inakwisha. Hivyo bei ya vyakula kwenye soko la Dunia imeanza kupanda. hakika itaathiri nchi nyingi za Afrika. Hii ni njia mojawapo jinsi gani mkorofi anaweza kusababisha vifo vingi)
Kwanza tukubaliane mama alishafeli angalau kutolea ufafanuzi juu ya mfumuko wa bei uliopo,
Ninafahamu mazara ya vita lakini si kwakubweteka kusubiri madhara yakufike.
Mfano mbona tuliamua kutumia njia tofauti kwenye corona tukatoboa??
Jiulize je importation yetu asilimia kubwa inatokea urusi na ukrani ? Mpaka tukimbilie madhara kwa haraka ivo?
 
Ni ameamua mwenyewe??

Kwanza tukubaliane mama alishafeli angalau kutolea ufafanuzi juu ya mfumuko wa bei uliopo,
Ninafahamu mazara ya vita lakini si kwakubweteka kusubiri madhara yakufike.
Mfano mbona tuliamua kutumia njia tofauti kwenye corona tukatoboa??
Jiulize je importation yetu asilimia kubwa inatokea urusi na ukrani ? Mpaka tukimbilie madhara kwa haraka ivo?
Yaani Kama mam Yuko huku heshima yangu kwake imeporomoka amebariki mfumuko wa Bei Bila kujuwa adhari itakuwa kubwa kuliko anavyodhani
 
Unaweza ukawa na point ila uwasilishaji! Kikubwa tutafute namna yankuokoa taifa letu
Huu upole wako unaotaka utumike ndiyo umelifikisha hili Taifa kuwa Taifa la mazombi,Taifa la watu waoga na la watu kama misukule wasiokuwa na ujasiri wa kukemea uchafu katika Taifa hadi Rais anafikia hatua ya kuhamasisha ufisadi katika Taifa na watu kukemea inaonekana ni kukiuka miiko yetu ya upole.


Taifa halitajengwa na watu wapole na waoga bali litajengwa na watu wenye ujasiri wa kukemea maovu,uzembe,madhaifu ya Serikali na wenye uthubutu wa kuhoji.
 
Ni ameamua mwenyewe??

Kwanza tukubaliane mama alishafeli angalau kutolea ufafanuzi juu ya mfumuko wa bei uliopo,
Ninafahamu mazara ya vita lakini si kwakubweteka kusubiri madhara yakufike.
Mfano mbona tuliamua kutumia njia tofauti kwenye corona tukatoboa??
Jiulize je importation yetu asilimia kubwa inatokea urusi na ukrani ? Mpaka tukimbilie madhara kwa haraka ivo?
Mkuu hujaelewa maana ya soko la dunia. Tanzania haina njia kuepukana na kupanda kwa bei. Samahani, hili ni hoja la kitoto kidogo. Usipopata nchi iliyo tayari kukupa zawadi, bei ya juu inafika hapa pia.
Ukijua njia mbadala, sema ! Kama huwezi kusema, isitangaze hapa Eti rais alifanya kosa kusema. Maana yeye anaelewa soko la dunia ni nini, anaonya kuhusu yale yanayokuja. Hajui njia mbadala.
Kama wewe unayo, umwambie, atakupa uwaziri bila shaka!!!
 
Back
Top Bottom