Sio kwamba wametuzidi ila sisi wenyew hatujiamini halafu tumekuwa wanafki.
Usipojiamini ww mwenyewe hakuna atakayekuamini.
Huku mitandaoni watanzania kila kukicha wanatukana na kudharau viongozi wao lakn hilo Kwa wenzetu hulioni. Hata kama wanakosoa wanakosoa Kwa akili na hekima.
Chukulia mfano kwenye corona. Wakenya wakitoa ripoti kuwa wanawagonjwa 10 watanzania wanasifia kuwa hao wamesema ukweli lakn huku Tanzania wakisema wanawagonjwa 8 watanzania wanaanza kukejeli kuwa wanaficha taarifa.
Let me guess... You're Jiwe Supporter ambao mnadhani uzalendo ni kuficha ficha mambo!!! Btw, ukichukua mfano wa corona, sasa kwanini watu wasikejeli kwamba Tanzania wanaficha wakati hata mtoto wa darasa la pili anafahamu hilo?!
Corona updates kwa Tz, ni hii hapa chini, ambayo tangu May 09, inaonekana hajaongezeka mgonjwa hata mmoja!!
Hivi kuna mtu mwenye akili timamu anayeweza kuamini upuuzi kama huo?! Au ndo mtu ukubali na kupongeza ujinga kama huo ili uonekane mzalendo?
Kinyume chake, KE updates ni hii hapa:-
Again, hivi kuna mwenye akili timamu anayeweza kutilia shaka nia hiyo dhahiri ya KE ya kuweka mambo wazi?!
Mwanzoni mwa hili sakata niliwahi kusema hapa kwamba "COVID-19 ni Janga la Dunia! Hakuna nchi itakayohukumiwa kwa kuwa na waathirika wengi, lakini nchi zitahukumiwa kwa kujaribu kuficha ukweli!! Na kwamba, hata Visitors watakuwa more comfortable kutembelea nchi ambazo ukubwa wa janga unafahamika kuliko kwenda nchi ambayo ukubwa wa janga haufahamiki"
Leo hii Wazalendo Fake utawasikia "US wasitupangie, kwanza nchi yao ndo imeathirika zaidi kuliko sisi!" Hawa bado wanadhani concern ya watu ni nchi gani imeathirika zaidi kumbe concern ya watu ni ukubwa wa janga kwenye nchi husika!!
Hapa tena nakumbushia msemo ule ule kwamba, watu watazingatia usemi wa "Bora ya Shetani unayemjua kuliko Malaika Usiyemjua"!!