Kiukweli Wanachadema walimtia aibu Mwenyekiti Mbowe


Wamasai wana imani Moja inayoeleweka.

Vivyo hivyo HAMAS, Hezbollah au wa Houthi.

Watu wanakuwa tayari kufia Imani zao.
 
Tatizo ni kuwa na association isiyojua inaamini au inasimia nini:

Mbowe, Lissu wafundeni wafuasi Falsafa ya Chama

Matokeo yake ni kubakia kulaumu wengine Hadi Simba na yanga huko.

Hilo ndîo tatizo
Bado CHADEMA haijajenga kitu inaitwa ITIFADI Kwa wanachama wake.

Simba na Yanga hizô NI timu z Mpira Huwezi kuzilaumu na kulaumu washabiki wake Wakati haohao washabiki unatakiwa kuwashawishi ili wajiunge na Chama Chako.

Angalia Chama cha Hammas n Hezbollah, Dunia nzima Iko opposite na waô lakini Mwaka WA 30 huu Dunia inashindwa kufuta vyama hivyo zaidi ya kuishia kuita vyama vya kigaidi
 
Mtiberi wetu mwandamizi, kwanza hongera kwa kupata tuzo humu JF kwa kazi yako nzuri.

Mkuu kuhusu hili hutendi haki kusema hivyo, wapinzani wale waliandaa maandamano ya amani. Viongozi wao wote walikamatwa mapema asubuhi, wafuasi wao wangefanyaje kwa tishio lile la askari kote Dar.

Ni ajabu watu kuitisha maandamano ya amani wakati huo polisi wanatishia amani ya maandamano hayo!!!

Labda Mtiberi mwenzangu ungesema wapinzani wakaze kuendelea kuandamana ili polisi watande mitaani tulale, maana usiku ule hakukatiza kibaka hata mmoja.

Kwa kweli hakuna haja ya kuwa na sungusungu sijui ulinzi shirikishi mitaani kama wapinzani wakiwa na utaratibu wa kukomaa kuandama namna ile kila usiku!!!

Kumbe polisi wapo wa kutosha na wanaweza kutuliza Jiji hili!! Tunahitaji kuanza kudai haki ya kulindwa. Kazi ya polisi kuwinda wapinzani kama digi digi porini sio kazi yao!!!

Watulinde kila usiku!!!
 
Tatizo lao wanarukiarukia ajenda, hata haileweki unaandamana kwa sababu ipi hasa.

Hivyohivyo wanachadema wangetakiwa kuonyesha umoja waô. Wanajambo Lao.

Sasa waô wanasema wanachama wa Wengine kama Simba na Yanga kushawishi Watu
Au Wafuasi wa Mwamposa.

CHADEMA hili waliangalie
 
Nilikua nakuchukulia poa ila kwa post yako hii nimekubali utaikon wako. We jamaa ni bonge la mwandishi na usije kujichukulia poa fasihi yako.
 
Nikubali uwasilishaji wako wa hoja
 
Mtiberi wetu mwandamizi, hutendi haki kusema hivyo, wapinzani wale waliandaa maandamano ya amani.

Mkûu Hapa naongea ukweli wa kilichotokea.
Kama yalikuwa ya Amani wangejitokeza tuu ili hao Polisi na serikali ya Samia iwafanye hicho itakachowafanya lakini walimuacha Mbowe na viongozi kadhaa.

Mbona Wamasai wameandamana Nonstop Kwa Amani tenà Wengine wakaumizwa na kujeruhiwa lakini walibaki na Msimamo. mpaka wametoboa


Kwa hîyo Kila CHADEMA wakisema wanaandamana kudai Haki Fulani alafu Polisi na serikali ikisema itatandaza Askari kîla Kona hawataandamana tenà?
Basi Hapo Kazi Ipo.

Kwa kweli hakuna haja ya kuwa na sungusungu mitaani kama wapinzani wakiwa na utaratibu wa kukomaa kuandama namna ile kila siku!!!

Hakuna haja ya waô Kutoa matamko ya maandamano huku wakijua wakutosha kidôgo hawataandamana.
Inawashushia ushawishi katika medani za Kisiasa.
 
Watu kuchagua AMANI sio wajinga.
Ccm wajifunze kuls na kipofu.wasidhani watu kila siku watabaki hivi hivi.
Ipo siku kitakuja kuchafuka alafu hawataamini.mnatakiwa mshukuru upole huu wa wananchi maana kama wangetii basi mjue hali ingekuwa mbaya.
 
Kwani Freeman Mbowe hakufanikiwa kuongea na waandishi wa Habari na kufikisha Ujumbe?

Usiwe na thinking ya kizamani bwashee 😂😂😂😂

Siasa ni sayansi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…