Nyakijooga
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 524
- 829
Wiki moja iliyopita, kivuko hicho kilipata hitilafu ya injini na kusombwa na maji kuelekea baharini, ingawa abiria waliokolewa kwa kutumia boti ndogo za fiber, magari yaliyokuwepo ndani ya kivuko yalikwama kuanzia saa moja na yakaja kutolewa hadi saa 6 Usiku
Hili si tukio la kwanza; Wiki mbili tu kabla ya hapo, kivuko hicho kiliacha kufanya kazi kwa zaidi ya wiki nzima.
Kwa sisi Wananchi wa Pangani tumekuwa tukiishi kwa hofu kila tunapopanda kivuko hicho kutokana na hofu ya kupata ajali.
Athari za tatizo hili zimekuwa kubwa sio tu kwetu bali hata kwa Watalii. Kwa mfano, maeneo kama vile Pwani ya Ushongo, ambayo yana hoteli na nyumba binafsi za kulaza wageni, yameathirika sana.
Watalii wanaowasili asubuhi hushindwa kuvuka kwa wakati na hulazimika kusubiri hadi saa 1 usiku ili kutumia daraja la muda linalojengwa na mkandarasi wa Kichina, ambaye ameruhusu magari kupita mara mbili tu kwa siku – saa 12 asubuhi na saa 1 usiku.
Hii ina maana kuwa mtu akifika kivukoni saa 6 mchana, atalazimika kungoja kwa saa kadhaa hadi daraja hilo kufunguliwa kwa matumizi.
Hali hii pia imeathiri usafiri wa mabasi, usambazaji wa bidhaa, na shughuli nyingine za kiuchumi. Mabasi yanakwama kivukoni na kushindwa kuwahisha abiria.
Tunaomba mamlaka husika zitusikie kilio chetu Wanapangani maana mkwamo wa watu ni mwingi na mabasi pia yanakwama yanashindwa kuvuka.
Pia soma ~ Wananchi wa Pangani – Bweni (Tanga) tunatumia Faiba kuvuka baada ya kivuko kuharibika tena