Kiwanda cha nyama ya Punda cha wachina kilichoko Shinyanga chafunguliwa kuendelea na uzalishaji

Kiwanda cha nyama ya Punda cha wachina kilichoko Shinyanga chafunguliwa kuendelea na uzalishaji

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2015
Posts
36,902
Reaction score
52,001
Kiwanda cha nyama ya Punda cha wachina kilichoko SHINYANGA chafunguliwa kuendelea na uzalishaji.

Source: Taarifa ya habari CHANNEL 10

Tuendelee kupeleka punda kwa wingi
 
Wakati hatuna ufugaji mkubwa wa punda na punda nchini wanatumika kwa ubebaji mizigo na makabila machache nchini kama vile wamasai wenye jadi ya kutumia punda ni uamuzi mbaya kuruhusu machinjio ya punda.

Machinjio hiyo awali ilishasababisha wizi mkubwa wa wanyama hao toka kwa wenyeji. Wengi wanaouza punda kiwandani sio wafugaji wa punda ila wanawapata kwa watu wa kati wenye kusadikika kuwapata kwa njia zisizo sahihi kama vile kuwaiba.

Hao wachina wenye nia ya kukidhi hamu ya nyama ya punda huko kwao ingekua busara kuwekeza kwanza kwenye mashamba ya ufugaji wa punda kuliko kuleta zogo kwa kiwanda kitakacho wamaliza punda nchini kwa hila za kibiashara na wizi.
 
Nyama ya punda tamu kama NOAH, sema tu nyingi zinawekwa kwenye soseji na baadhi ndo zile za makopo!
 
Èee ndo manake tufanye Biashara watu wetu wapate ajira
 
Nakubaliana na wewe 100% kabla ya kuruhusu kiwanda cha kuchakata nyama ya punda kwanza waanze kwa kufungua ranchi za punda, ufugaji wa punda hapa kwetu ni chini sana hakuna familia hata moja yenye punda 20+ huo uwezo wa kulisha kiwanda utatoka wapi.

Baada ya miaka 2 Tanzania haitokuwa kabisa na punda watakuwa adimu kama faru.
 
Nini kilipelekea hicho kiwanda kufungwa hapo awali na nini kimepelekea hicho kiwanda kufunguliwa sasa?
 
Hatari kubwa imerudi tena kwa wafugaji wa punda. wizi wa punda utafanya uchumi wa kipato kwa wafugaji kushuka.Thamani ya punda ipo kwenye kufanya kazi na siyo kuliwa kama chakula
 
Hapa linatafutwa soko la pikipiki na toyo.

Watu waliozoea kutumia punda lazima wanunue kama wanyama hao wataisha.

Hii ni intelijensia ndogo ya kiuchumi.

Akili ndogo inafikiri kuwa wanatafuta nyama tu.
 
Kiwanda cha nyama ya Punda cha wachina kilichoko SHINYANGA chafunguliwa kuendelea na uzalishaji

Source: Taarifa ya habari CHANNEL 10

Tuendelee kupeleka punda kwa wingi
Kwanini kilifungwa ?
 
Back
Top Bottom