Kiwanda cha nyama ya Punda cha wachina kilichoko Shinyanga chafunguliwa kuendelea na uzalishaji

Kiwanda cha nyama ya Punda cha wachina kilichoko Shinyanga chafunguliwa kuendelea na uzalishaji

Hii ni hatari baada ya miaka 2 hakutakuwa na punda Tanzania.
Mbona kuna kiwanda kikubwa cha punda Dodoma (Nyama ya punda )

Mimi nilienda Dodoma 2016 kilikuwepo na kinafanya kazi.
 
Bei ya punda mzima mwenye afya ni sh 80,000 mpaka 100.000. ngozi ya punda ni sh 80,000. haya kipi bora hapo. punda afanye kazi au uuze kitendea kazi kwa malipo hayo.
Ni wewe mwenyewe ndie unatakiwa kutafakari suala hilo kwa sababu nilikuuliza, ina maana hao wananchi unawaona hawana akili?!

Umedai mkokoteni wa punda unaingiza 20K to 50K kwa siku! Na hapa tena unadai punda mwenye afya anafika hadi 100K!

Sasa tu-assume mwananchi ana punda mmoja anayemtumia kwa biashara ay mkokoteni! Sasa unataka kusema huyu mwananchi hana akili hadi auze punda kwa 100K wakati anajua anaweza kupata hiyo 100K kwa muda usiozidi siku 5?!
 
Nilikaribishwa chakula kwa Wasomali, katikati ya kula pilau mama alisema yaani tulisubiri hii nyama mpaka kukata tamaa maana ni duka lile tu ndo wanauza nyama ya farasi.

Baada ya hii sentensi nilijikaza nisitapike, nilimaliza salad kwenye sahani nikaongeza na matunda kwa ustaarabu nilitoa shukran kwa chakula.
Duh, ka nmimi, ningepanic noma! 🤣 🤣 🤣 🤣
 
Punda ndio mbadala wa mikokoteni ambayo ni gharama, punda ndio msaada wamama na watoto wa kike kwenye familia za wafugaji.

Nenda kongwa jimboni kwa Spika uone jinsi punda wanavyosaidia wanawake na watoto wanaotafuta maji ambali mrefu.

Bila punda ni mateso kwa wakina mama hasa familia za wafugaji.
Unataka kuniambia tuko nyuma kiasi icho? Yani karne hii tunajisifu kutumia punda kama means of transportation? Kweli kunatatizo mahali.

Sent from my 601SO using JamiiForums mobile app
 
Wakati hatuna ufugaji mkubwa wa punda na punda nchini wanatumika kwa ubebaji mizigo na makabila machache nchini kama vile wamasai wenye jadi ya kutumia punda ni uamuzi mbaya kuruhusu machinjio ya punda.

Machinjio hiyo awali ilishasababisha wizi mkubwa wa wanyama hao toka kwa wenyeji. Wengi wanaouza punda kiwandani sio wafugaji wa punda ila wanawapata kwa watu wa kati wenye kusadikika kuwapata kwa njia zisizo sahihi kama vile kuwaiba.

Hao wachina wenye nia ya kukidhi hamu ya nyama ya punda huko kwao ingekua busara kuwekeza kwanza kwenye mashamba ya ufugaji wa punda kuliko kuleta zogo kwa kiwanda kitakacho wamaliza punda nchini kwa hila za kibiashara na wizi.
Mchina ale punda ???
Yani yeye labda apeleke ngozi huko kwao..

Nyama tunakula sie wabongo, mfano mashuleni wanafunzi wanakula sana bila kujua
 
Wizi wa mafuta ya transfoma ya kukaangia chipsi vumbi utaanza kukithiri tena

Jakaya Kikwete is running the country by proxy
 
Back
Top Bottom