Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
Kichwa cha mada kinajielezea.
Ni zaidi ya ujinga [ignorance]. Ni upumbavu [stupidity].
Rais Samia karuhusu mikutano ya vyama vya siasa.
Rais Samia kavipa vyama vya siasa ruzuku.
Rais Samia kamlipa Tundu Lissu stahiki zake za kibunge.
Rais Samia katoa mabilioni huku na kule.
Watu ambao mtu unaweza kudhani kuwa wana uelewa wa msingi tu wa jinsi ambavyo serikali inaendeswa, ndo wanaoongoza kwa huu upumbavu.
Sasa pata picha ya raia wengine ambao labda hawana uelewa wa kutosha kuhusu elimu ya uraia kwa ujumla.
Kama wale wanaoonekana kuwa na uelewa ndo wanaoongoza kwa upumbavu na ushabiki wa kujitoa akili, nchi hii Ina matumaini gani yaliyo halisi ya kupata maendeleo?
Matakwa ya kikatiba na kisheria siyo fadhila wala hisani ya Rais Samia wala Rais mwingine yeyote yule.
Kama hao chawa wa Samia wanayachukulia hayo matakwa ya kikatiba na kisheria kuwa ni hisani na fadhila ya huyo mama yao, basi huyo mama ni dikteta.
Maana kwenye udikteta huwa hakuna cha katiba wala sheria. Ni mwendo wa amri, hisani, na fadhila za dikteta tu.
Tanzania tuna idadi kubwa sana ya wajinga, wapumbavu, na mazuzu, wakiwemo viongozi wa serikali na vyama.
Na ndo maana si bahati mbaya kuwepo kuwa kwenye hali tuliyonayo.