Kiwango cha ujinga cha viongozi wa CCM, mashabiki wao, na raia kwa ujumla, kinatisha!

Kiwango cha ujinga cha viongozi wa CCM, mashabiki wao, na raia kwa ujumla, kinatisha!

Hilo unalolisema nusu na robo ya watanzania hawalijui, hawajui kuwa they have power to remove the president from the office when he/she goes against their will.
Ni CCM ndio imetengeneza hii hali kwa manufaa yao na si kwaajili ya majority ya watanzania. Tuamke
19912c502c337a182567a6954c3c7854.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tena mjinga wa kwanza ni wewe uliyekuwa unatetea ukatili wa magufuli humu.

Kipindi cha msukuma mwenzako ulikuwa unamtetea humu kila siku. Saivi hayupo ndo unaponda CCM kuna ujinga. Wewe ni mbaguzi tu na kila siku hoja zako zinaangalia nani yupo upande wako. Tunaokujua hutusumbui humu
Magufuli nimempinga sana humu. Unabisha?
 
Ukiwasikikiza chawa wa Samia, ni kana kwamba kila kitu kinamilikiwa na Samia, kila kitu ni fadhila na hisani yake.

Si ajabu katika akili zao wanaamini kabisa kuwa Samia anayamiliki hata yale majengo ya ikulu ya Dar es Salaam na Dodoma.

Si ajabu pia wanaamini kwa dhati kabisa zile gari apandazo Samia ni za kwake binafsi.

Sasa kama rudimentary knowledge ya mambo ni mgogoro, je kwa mambo yaliyo changamani hali ikoje?
Huu ni muendelezo wa the anatomy of stupidity!, kitu kizuri kumhusu Rais Samia, intermsy of intellect, and I.Q she is not kivile sana kama yule, Blaza wangu, but she is not stupid!, aliwahi kuwaagiza watoaji haki, Asante Rais Samia kwa kuwasisitiza watendaji wa vyombo vya haki kuwa haki sio hisani, bali ni stahiki. Watende haki, tubadili Katiba kurudisha haki
hivyo tunamshauri asiruhusu na asinyamazie hii stupidity ya wasaidizi wake, kumsifia anapotimiza wajibu wake kwa fedha zetu, wanamuita ni fedha zake!, hata akikopa, wanaolipa ni sisi walipa kodi, ingekuwa na yeye analipa kodi, then kwenye hiyo fedha angeweza kuwa na fedha yake, but very unfortunately yeye ni tax exempted!. Hii ya fedha zetu za kodi zetu ndio zinaitwa zake!, ni stupidity tuu!. Niliwahi kushauri Kuepuka Double Standards ya Kodi, Nashauri Rais Uongezwe Mshahara, Ili Alipe Kodi, Wote Tulipe Kodi!
one good thing about this lovely lady, atatufikisha pazuri!.
P
 
Tena mjinga wa kwanza ni wewe uliyekuwa unatetea ukatili wa magufuli humu.

Kipindi cha msukuma mwenzako ulikuwa unamtetea humu kila siku. Saivi hayupo ndo unaponda CCM kuna ujinga. Wewe ni mbaguzi tu na kila siku hoja zako zinaangalia nani yupo upande wako. Tunaokujua hutusumbui humu
Mkuu Lord denning , ukichukua jina la mtu mashuhuri kama Lord Denning, lazima umuishi na kuliishi hilo jina!. Nadhani JPM alikosolewa na Kanda ya Ziwa kuliko wengine wote!.
P
 
Nchi haiendeshwi kwa kubembelezana ukijifanya kufuata sana sheria sijui taratibu utachelewa sana.
Sasa sheria ni za nini kama huhitaji kubembelezana? Ukiona mtu anatumia nguvu badala ya sheria, ujue hana uwezo, na amepata nafasi hiyo ya uongozi kwa ghiliba, hivyo namna pekee ya kulinda hiyo incompetence ni kutumia mabavu.
 
Mie narusha picha tu kama ushahidi au niweke na ka video?? Hii thread unaweza kuombea Mkopo pale BOT
 
Tusipoamua kujichanganua nchi haiwezi kubadilika kwa lolote.
Nchi hii kuanzia waziri mkuu ni chawa hajitambua, hawezi kuongea kitu kama kiongozi aliyepo kisheria bali kama vile uwaziri mkuu ni hisani.

Kila kitu akitamka lazima antamke rais
Kwa aina ya chaguzi zetu zilivyo za kihayawani, lazima kila kiongozi aongee kwa kujinyenyekeza kwa rais, maana karibia wote hawapo hapo walipo kwa ridhaa ya umma, bali hisani ya rais.
 
Back
Top Bottom