Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Hiyo mifumo ya katiba na Bunge la Westminster si yetu.Kichwa cha mada kinajielezea.
Ni zaidi ya ujinga [ignorance]. Ni upumbavu [stupidity].
Rais Samia karuhusu mikutano ya vyama vya siasa.
Rais Samia kavipa vyama vya siasa ruzuku.
Rais Samia kamlipa Tundu Lissu stahiki zake za kibunge.
Rais Samia katoa mabilioni huku na kule.
Watu ambao mtu unaweza kudhani kuwa wana uelewa wa msingi tu wa jinsi ambavyo serikali inaendeswa, ndo wanaoongoza kwa huu upumbavu.
Sasa pata picha ya raia wengine ambao labda hawana uelewa wa kutosha kuhusu elimu ya uraia kwa ujumla.
Kama wale wanaoonekana kuwa na uelewa ndo wanaoongoza kwa upumbavu na ushabiki wa kujitoa akili, nchi hii Ina matumaini gani yaliyo halisi ya kupata maendeleo?
Matakwa ya kikatiba na kisheria siyo fadhila wala hisani ya Rais Samia wala Rais mwingine yeyote yule.
Kama hao chawa wa Samia wanayachukulia hayo matakwa ya kikatiba na kisheria kuwa ni hisani na fadhila ya huyo mama yao, basi huyo mama ni dikteta.
Maana kwenye udikteta huwa hakuna cha katiba wala sheria. Ni mwendo wa amri, hisani, na fadhila za dikteta tu.
Tanzania tuna idadi kubwa sana ya wajinga, wapumbavu, na mazuzu, wakiwemo viongozi wa serikali na vyama.
Na ndo maana si bahati mbaya kuwepo kuwa kwenye hali tuliyonayo.
Tumepandikiziwa tu hivi karibuni.
Hatuja i internalize.
Ni kama mtu anayefanya mtihani kwa ku cram, haelewi somo.
Si CCM tu, all across the board.
Kuna wakati nilikuwa nafanya mazungumzo na wanasiasa fulani. Akaja jamaa mmoja kiongozi wa CHADEMA, akawa anaelezea mambo ya CHADEMA.
Sasa, jamaa mmoja akamuuliza yule kiongozi wa CHADEMA, hivii, katika mirengo ya kisiasa, CHADEMA inasimama wapi? Iko left, right, center? Ni chama cha wafanyakazi? Mabwanyenye? Conservatives? Labor? Chama kipo wapi kimrengo? Ideology yake ni ipi?
Yule kiongozi wa CHADEMA alishindwa kujibu. Mpaka Godbless Lema akaingilia na kuokoa jahazi.
So, hata haya mambo ya vyama tumegeza tu. Waingereza na wazungu wenzetu walipitia stages zile za feudalism, industrial revolution, class differences and struggle, wakapata mifumo ambayo ina uhalisia kwenye siasa zao.
Sisi tumeiga tu. Ndiyo maana hata hayo mambo ya ideology yanaonekana ni ya kidhahania zaidi na watu hawayajui.
Ndiyo maana hata elimu ya uraia na katiba ni ndogo. Watu wamezoea machifu wanagawa largesse.
Ndiyo maana watu wanaona Samia anagawa hela, analeta maendeleo.
Ni kama mtu anajua kucheza soka, unampeleka kucheza tennis.
Hata sheria za tennis hazijui!