Yoyo Zhou
Senior Member
- Jun 16, 2020
- 199
- 322
Ripoti hiyo imesema tafiti zimeonesha kuwa ukosefu wa ajira kwa Wamarekani wenye asili ya Afrika kwa muda mrefu umekuwa juu kuliko wastani wa Wamarekani. Wakati soko la ajira linapokuwa na nguvu, kwa mfano kabla ya janga la COVID-19 na mwaka 2022 na 2023, pengo hili hupungua, na wakati soko la ajira ni dhaifu, Wamarekani wenye asili ya Afrika wanakabiliwa na kiwango cha juu zaidi cha ukosefu wa ajira. Ripoti hiyo ilimnukuu mtafiti mkuu wa timu ya utafiti wa uchumi katika Tovuti ya Kutafuta Kazi ya Glassdoor, Chris Martin, akisema, wakati uchumi unapodorora, Wamarekani wenye asili ya Afrika ndio wa kwanza kuathiriwa.
Takwimu kutoka Idara ya Kazi ya Marekani zinaonyesha kuwa kiwango cha ukosefu wa ajira nchini Marekani kilikuwa asilimia 4.3 mwezi Agosti, ambalo ni ongezeko kidogo kutoka asilimia 4 mwezi Januari. Katika kipindi hicho, kiwango cha ukosefu wa ajira kwa Wamarekani weupe kilikuwa asilimia 3.7, ambacho ni asilimia 0.2 tu ya juu kuliko Januari. Wakati huo huo, kiwango cha ukosefu wa ajira kwa Waamerika wenye asili ya Afrika kilifikia asilimia 7.5 mwezi Agosti, ambacho ni ongezeko la asilimia 1 kuliko mwanzoni mwa mwaka.
Nchini Marekani, kuwa na kazi nzuri kunachukuliwa kuwa njia kuu ya kujipatia fursa mwenyewe na kwa vizazi vijavyo. Ripoti kuhusu haki za binadamu za Wamarekani wenye asili ya Afrika iliyotolewa na Muungano wa Kitaifa wa Mijini wa Marekani inasema, Wamarekani wenye asili ya Afrika wana asilimia 73.9 ya fursa ya Wamarekani weupe, wakiwa na hadhi ya chini ikilinganishwa na watu weupe katika ajira, mali, afya, elimu, upatikanaji wa mahakama, na ushiriki wa kisiasa. Ukosefu wa usawa wa ajira ni mbaya zaidi. Zaidi ya hayo, Wamarekani wenye asili ya Afrika wanakabiliwa na kutotendewa haki katika nyanja mbalimbali, ikiwa ni pamoja na ujasirimali, uwekezaji, ajira, kupanda vyeo na nyongeza za mishahara. Ukosefu huu wa usawa hatimaye huchangia pengo kubwa kati ya masikini na tajiri. Takwimu zinaonesha kuwa kaya ya Wamarekani weupe wa daraja la kawaida ina utajiri mara nane ya kaya ya kawaida ya watu weusi nchini Marekani.
Ubaguzi wa rangi katika uchumi wa Marekani umekuwepo kwa muda mrefu, na ukosefu wa usawa katika nyanja mbalimbali za jamii, hasa katika sekta ya ajira, umechangia kuenea kwa umaskini wa Wamarekani wenye asili ya Afrika. Marekani inadai kuwa ni mtetezi wa “haki” na “usawa” duniani, lakini haiwezi kuondoa ubaguzi wa rangi nchini humo.