Plot4Sale Kiwanja kinauzwa 70 kwa 70 Kigamboni Mwembe Mdogo

We jamaa si muuzaji wa kiwanja. Si kwa lugha hii unayoitumia. Kila la heri kwenye hiyo mission yako nyingine. Hii naona imebuma humu.
 
Kuna maji kweli?? [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Hawa jamaa ni wazushi sana ujue nini unapotangaza biashara unatafuta rizik wengine tumekwama mambo chungu mzima alafu anakuja mtu anatoka kusikojulika nakulete uzushi kwenye tangazo lako sio utani mzuri kabisa nitabia fulani za kichawi huu ndio uchawi kuna watu wanauliza uchawi nini waje hapa wajione aswaaa tena huu uko advanced!!

uwezi jua mtu anauza kitu chake kwasabu zipi au magumu gani anayapitia alafu mtu anakuja kwenye page yako na akili flani za kiuchawi anatisha watu wenye nia ya kununua biashara zako wasinunue, sio kwamba anakujua labda useme unaongovi nae hapana yeye furaha yake ukwame tu ufeli mazima uteseke ukose riziki ufe njaa na familia yako yeye atafurahi sana unajiulia wewe ungekua Mungu ngawa riziki ungeua wangapi??
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ha ha ha huyu kuna nati imelegea kichwani[emoji28][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ni dalali itakua
Muuzaji mwenye Mali angejali wateja
Mteja anapiga simu namba ipo hapo juu sidhani kama kuna mnunuzi wa kiwanja anaweza kutuma msg au kuandika ugoro kwenye tangazo la mtu
 
Mkuu usihofu wateja watakuja tu. Tatizo awamu hii imekaa kiugumu sana maana purchasing power ya watu iko chini sana
Purchasing Power ianakuzuia nini kufungua Thread yako utangaze heka zako nne mbona mnapasua
 
Wewe labda ni mgeni wa JamiiForums..

Hili ni jukwaa huru la watu kuwakilisha walichonacho kama ambavyo wewe umetumia uhuru huo kuweka biashara yako hapa...

Hakuna moderator atayenipiga ban kisa nimekuuliza swali legit kabisa...

Huko K'mboni maeneo uliyotaja hayo Mwembe Mdogo, Malimbika, Vumilia Ukoo n.k kumekuwa na migogoro sugu baina ya wananchi, halmashauri na hao wapimaji kiasi kwamba viwanja vingi havipo kwenye ramani za ardhi...

Sasa wewe kuulizwa swali kidogo tu wageuka mbogo badala ya kutoa ufafanuzi ili wanunuzi uwatoe shaka
 
Sina muda wakupoteza kujibizana na wewe, endelea kufuga majini na kuuza matunguli hapa JF tuone mwisho wa siku utapata nini?
 
Kwa Kigamboni ni vema ununue eneo kipindi cha mvua. Hilo eneo kwa utaalam wangu wa hizo nyasi sitasema sana.
 
Shukrani sana kwa kufungua watu macho. Huo ndiyo ukweli.
 
nimecheka sana kwamba jf imekuwa sehemu ya kukutania wachawi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…