Anatakiwa afahamu kuwa JF siyo ya akina bongolala. Huku kuna wataalam wa kila namna. Mimi mtaalam wa vegetation hilo eneo sitanunua kwa ujenzi siku za karibuni. Labda ninunue for future use wakishajenga majirani. Awe mpole kabisa maana
Watu8 amempa ukweli wote kwa kuwa ni mtaalam wa maeneo mengi Kigamboni na ameyataja kabisa. Hii itasaidia ukifanya kununua unaenda kwanza Manispaa Kigamboni kujiridhisha na majirani pande zote utapata ili wakupe ABC za eneo. Ukitapeliwa siku hizi umeyataka mwenyewe. Mtu wa Mipango Miji siku hizi ni kazi kwa simu tu akiingiza coordinates za eneo akiendakulaza kwa master plan inampa majibu yote. Simple as that. Hivyo mleta mada atulie wataalam wa waliliko eneo watiririke.