Kizazi cha sasa ni kizazi jeuri na kiburi

Kizazi cha sasa ni kizazi jeuri na kiburi

Tatizo lingine ni hili hapa

Unakuta mshangazi anatoka na kiben teni,sasa hicho kiben teni heshima inashuka kuwaheshimu kina Mama,anaona kama vile nao anaweza kutoka nao tu,

Unakuta kabinti kanatoka kimapenzi na Baba mzima mwenye familia yake,sasa hapo hicho kibinti heshima inashuka kuwaheshimu wababa wote,

Hakuna haja ya kumtafuta mchawi bali lawama ni kwetu sisi na sio kwa hicho kizazi cha leo.
Hili ndio tatizo kubwa.
 
Kuna sehemu nilikwenda majuzi, dah vitoto sio vioga kabisa mzee. Yaani wageni tumekaa sebuleni watoto wanafanya vituko tu mara apande kwenye sofa akurukie, mara akupande kichwani, mara akushike ndevu, mara akuone unatuma sms au kupokea sim atake kukunyang'anya, mara atake kukulazimisha umuangalie akiwa anacheza muziki na hapo ametoa channel uliyokuwa unatazama ameweka katuni halafu anakuoforce utazame au usikilize makatuni yake.

Hapo wazazi wao wanajifanya wapo busy tu hawana time na kuwa observe mienendo yao au vile vitu wanavyofanya hapo. Yaani ni upuuzi kwenda mbele.

Sasa unabakia kujiuliza hawa watoto na hawa wazazi wana ajenda gani aisee. Huu utomvu wa nidhamu mbona kama umepitiliza? [emoji848]
 
Achana na kusalimia, hawana aibu, haya wala staha. Mfano mzuri ukipanda daladala mida ya jioni utaona viwanafunzi vinaongea ujinga tena kwa nguvu bila kujali, careless
Ukitaka kujua chanzo ni nini then nenda kwenye familia zao halafu utazame aina ya malezi inayoendelea.
 
Unasema kusalimia?
watoto wa siku hizi sio waoga kama zamani, watoto wa zamani walikua wakiiba sukari wanafuta mdomo na kuupaka vumbi kabisa ili wasisanikiwe..Ila awa wa sasahvi aibi sukari wao wanaila mbele yako, na haumwambii kitu...
 
ndo nikimsalimia ananiuliza nataka kumnyima nini
Mtu anayekwambia hivyo itakua wewe ndio umempa nafasi ya yeye kuweza kukwambia hivyo,inategemea pia na jinsi ulivyojiweka na jinsi unavyodeal nae,

Mtu mzima anayejiheshimu na ambaye hana mazowea ya hovyo na wewe,hawezi kukwambia maneno kama hayo,

Jaribu kuchunguza,hapa tatizo ni wewe na sio hao wanaokwambia hivyo.
 
Hivi umegundua watoto wengi siku hizi ni wagumu sana kusalimia mtu. Yani wamjue, wasimjue, ni mpaka mzazi amwambie salimia anko, salimia anti.

Bila hivyo!

Vinauchuna kama kichuguu. Morals zilienda na mafuriko. Wazazi tufungue macho, Masikio na midomo.
Tatizo ni wazazi na walezi

Tunazaliana bila kuwa na maandalizi ya malezi
 
Mimi mtoto wa miaka 15 - 25 asiponiamkia sawa mana anajutambua na ndo maisha aliyoyachagua ya kukosa adabu na sisi dada zao huwa siumizi kichwa najua tu huyu mshenzi wala hayuko mbali na uhalisia atakuja kupata funzo karibuni.

Wanaoniudhi mimi ni kwanzia 4 - 14 hawa mi naona bado hawajalelewa vizuri kujitambua
Unakuta umawanunulia zawadi umewapa wengi tu wa mtaani 5yrs mpaka 8yrs wanapokea tu afu basi unakuta sasa wazazi wao wanahaha mwambieni Aunt asante! Huwa haileti picha nzuri ni dosari kwa mzazi kwamba kuna namna malezi hayako sawa ijapokuwa mm wala si- mind mana natoaga kama sadaka.

Kama wakina mama watafundisha adabu watoto kama wanavyokaa kutwa kujadili uchungu wa kuzaa hizi mada zisingekuwepo kabisa!!!
 
Back
Top Bottom